Naona hii nachingwea jkt kabisaNi Mafinga au Dom?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona hii nachingwea jkt kabisaNi Mafinga au Dom?
Mkuu, huyu mtoa mada ni KeHasira lazima niwe nazo. Una jina la kiume unaandika kwa sauti ya kike.
Ni lastborn na yuko very emotional maana kila kituo kwake ni Kulia...Mleta Uzi ni ke jamani,mbona anamwambia kabisa rafiki yake ni Anna?msichoelewa hapo Nini?
short-sightedUligeuza JKT kuwa danguro? JKT ni guest house au danguro? Ndicho kilikupeleka JKT ?
🤣🤣🤣🤣Rudia aisee damau anaimba🤣🤣🤣 niache me nirudie kusoma Mara tatu na sijaelewa 🤣🤣🤣
Kateseka sanaNi lastborn na yuko very emotional maana kila kituo kwake ni Kulia...
🤣🤣🤣Bibi atakufinyaaaa😀😀 Bibi siyo mimi. Kuna mtu kaandika hivyo na mimi nikamtania ila lengo lake alitaka kuandika bla bla.
Mambo bibi?
Ila wewe 🤣WAla si mkorofi sipendi watu wakughasi. Nmegundua we ni binti nipo hapa kukulinda. Nione mtu anakutingisha. Kwa kweli nitamchapa nao sana. Sasa uwe na amani nipo hapa kukulinda. Hakuna wa kukubebesha tranka tena. Na usimsumbue mama. Sawa eeeh?
Wee namtania tu hawezi kunifinya😘🤣🤣🤣Bibi atakufinyaaaa
NangaHabari!
Nilipomaliza form 6 zikatoka nafasi za kwenda jeshi wanaita "kwa mujibu" basi nikaangaza macho yangu kwenye orodha nikaona "Ephen - Rukwa"
Basi nikafurahi sana, furaha haikua kwasababu naenda jeshi hapana! Hata mpango nayo nilikua sina ila tu niliona ni bahati jina langu kua kwenye list sababu sio wote uchaguliwa.
Nikawasiliana na marafiki zangu kuna baadhi walichaguliwa pia lkn hakuna niliyechaguliwaa nae kambi moja, nikaanza kusikia story plus video za status, instagram watu wanaeka makuruta wanavyogaragara kwenye matope, mazoezi magumu hadi wanalia, nikapata uoga hapo ikawa mzozo nikasema mimi jeshi siendi kwanza kunyoa kipara hapana.
Mzee akaniambia lazima uende, huko Rukwa mkuu wa kambi ni rafiki yangu hivyo wewe mateso hutoyapata nikafikiria nikaona huyu mzee ananipiga fix ili nijae mimi jeshi siendi.
Ila nikawa nataka sitaki na kilichokua kinanitatiza kwenda ni yale mateso tu niliyokua naona kwenye video.
Kuna siku rafiki yangu akanipigia simu kunishawishi twende ila akaniambia "Ephen twende kambi ya mkoa X achana na Rukwa huko wana mazoezi makali sana" nikamwambia kama hivyo fresh acha nijiandae tutaenda next week sababu deadline ilikua bado. Rafiki yangu nampa jina Anna.
Anna ana kaka ake ni mjeda sasa akawa anatupa tips muhimu za kuzingatia mojawapo alisema tranka tutakalobeba tusijaze vitu vingi tuweke vitu vyepesi ikiwezekana vitu tukanunue kambini hukohuko.
Mimi niliona usumbufu yaani nitoke na tranka tupu vitu nikanunulie kambini? nikanunua vitu vyote nikajaza kwenye tranka. Kumbe yule mjeda alikua na maana yake Aisee bora ningemsikiliza.😂
SIKU YA SAFARI
Tukatoka zetu na Anna tukapanda gari tunaenda kambi ya mkoa X japokua tumepangiwa kambi tofauti kila mtu.
Tupo kwenye gari nina furaha naenda kupata experience mpya pia nilifurahi kwenda mkoa mwingine sababu nimezoea dar tu, safari ilichukua almost masaa 7 tukafika huo mkoa X mjini, gari ndo mwisho.
Sasa wote hatujui nini kinafata hapo Anna yeye tranka lake niseme lipo tupu kabeba vitu muhimu tu, mimi nimejaza hadi kubeba linanishinda.
Tukamfata konda kumuuliza, "Sisi tunaenda kambi X tunaomba utupe muongozo" akatuambia pandeni bajaji hadi kituo flani mkifika kuna hiance zinaenda huko jina la kambi ndo jina la kituo cha kushuka.
Tukafanya kama alivyotuambia, tumeingia kwenye hiance asilimia kubwa wana vipara hivyo nikajua wote tunaenda kambini.
Kule tuliposhuka na gari nilipapenda sana ni kuzuri panavutia hamna pilikapilika nyingi nakumbuka nilimpigia simu mama, akaniuliza umepaonaje nikamjibu kwa furaha ni pazuri nimepapenda akaniambia "ukifika kambini nijulishe lkn ukiona huko mateso yamezidi nipe taarifa nikufate urudi nyumbani"
Basi tulivyokua kwenye Hiance tunaenda huko wilaya yenye kambi mwanzoni nasmile na Anna wangu ghafla akili yangu ikavurugika tuliingia barabara ya vumbi sijawahi ona, gari zima hatuonani, kila mtu kwenye gari katapakaa vumbi hadi kope zote nyeupe ndani ya pua nywele vumbi hapo nikapata sign ninapoenda sio pazuri.
Safari ilichukua kama masaa 3 tukaambiwa wale wa kambini mmefika.
Katika maisha yangu bad moment niliyowahi kuexperience ni hii siku, Tumeshuka tu nikaona njia ya vumbi imekata kulia ni ndefu kama 2km nikasikia sauti "Hapohapo wote chuchumaa tranka kichwani ruka kichurachura uelekeo huu hapa kwenda kambini"
Kudadeq ndo nikajua kwanini niliambiwa niende na tranka tupu
Anna yeye chap kachuchumaa tranka kichwani, mimi machozi yashaanza kunitoka nikamwambia Anna mimi nimeghairi siendi narudi nyumbani, hata sijamaliza sentensi nishakula bao la mgongo kutoka kwa mjeda akaanza kufoka wewe bila shaka umetoka Dar naongea tii Amri kwanini umesimama ? Aya tranka kichwani kuruka uelekeo huu.
Akaja mjeda mwingine akanitwika tranka kichwani hapo nishachuchumaa sikuweza kuimili kuruka na tranka.
Anna akaniambia lete nikusaidie chukua langu, yule mjeda aliona tu hata akinipiga ule mzigo siuwezi na Anna pia hauwezi akamwita mjeda anayejitolea chukua hili tranka wasaidie, basi nikapona hivyo.
Kimbembe kikawa hiyo kichurachura nikiangalia mbele sioni geti, ni mbali almost 2km ndo niruke kichurachura? Hapo machozi yananitoka nalia nkamwambia Anna "mimi namwambia mama anifate siwezi hizi mambo" Anna nae analia Ephen usiondoke ukaniacha mwenyewe bora hivi tupo wote Afadhali.
Nilihisi miguu inawaka moto inataka kupasuka, msafara tupo wengi hadi wanaume wanalia, sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia.
Itaendelea......
[emoji2][emoji2]Hivi huwaga unasoma comment zako kabla hujatuma [emoji3][emoji3][emoji3]
Watu wameshavurugwa na stress za maisha[emoji1787][emoji1787][emoji1787] we Soma hata nyuzi zake sijui anatype huku anatembea [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
😃Unaona bra au blah?? 🤔
Ulivyo mjeuri wala hupendezei kudekaMbona mko serious hivi?
Mimi mpaka chuo nikiumwa mama atanipeleka hosp, na nikiwa najiskia vibaya vibaya nalia kabisa.. na sio kudeka, sijui ni nini uwa.
Hiyo ni oljoroWewe sasa ndo umepatia![emoji122] mojawapo hapo mkuu...
Angelia kilugha chao huyo , umebanwa ku***nya, ila kuchuchumaa huezi unabaki kulia kikwenu tu, RTS ni habri nyingineSasa dogo hiyo ni kozi ya mujibu tena mnafundishwa uzalendo tu kwa miezi yenu mitatu then mnarudi kitaa huku mkirashia rashia MK, UP, Shabaha na Pori then Gwaride wengi mkiangukia vitengo vya ngoma coy, KO na Singe wengine Gwaride na kuondoka zenu. Sasa ungeenda kozi ya kujitolea au RTS ungesemaje?😄😄
Bibi mkalii😁😁😁Wee namtania tu hawezi kunifinya😘
Sahizi yupo Kisemvule anakoromaBibi mkalii😁😁😁