Niliyoyashuhudia Jeshini

SEHEMU YA 12
4. KARATE

Niliulizia kwa kuruti wenzangu waliopo karate ni yupi mkuu wa kitengo? Wakanionyesha alikua afande mpemba mfupi hivi nikamsoma nikaona sio mkali.

Kwanini nilitaka kumuona kabla?

Sababu nilijua karate ndo option yangu iliyobaki vitengo vingine sijafit hivyo sitakiwi kuleta mchezo
Kwa kusoma attitude ya mwalimu nipate mwanga kama huko nitaweza pia au lah!.

Siku ikawadia nikaenda kitengo cha karate baada ya kutoka mabio alfajiri.
"Aya jipangeni tuanze kazi" afande mpemba akasema
Kuruta wakajipanga na mimi nikaunga.

"Mbona naona sura mpya?"
Mimi afande nimekuja kujiunga na karate
"Sawa hamna tatizo hapa sifa wepesi na ustahimilivu kuruti! Fungua moyo jipe morale Wazii kuruti"
Waziii afande
Alivyonipokea niliridhika nikaona hapa nitadumu nikajikuta nimeipenda tu karate kabla hata ya kuona mziki wake.

Yule afande alikua mtulivu mstaarabu anafundisha kwa upendo hata ukikosea hakupi madoso wala mabanzi.

Style zikaanza pale afande anatupa mafunzo kwa upendo nilijikuta nimeweza zile style za siku ya kwanza japo changamoto kubwa ilikua kwenye balance lakini niliweza.

Siku zikaenda nikawa style zote nazishika naenjoy kua kitengo cha karate.
Sikua nanga wala bora nilikua katikati tu. Nakumbuka styles nyingi kama Kibadanch, zekidanch stans, Heiki danch, kosa dach na musubu danch.

Nikiulizwa nipo kitengo gani, najibu kwa kujiamini na smile lote "Mimi nipo karate"

Kitengo cha karate kilikua na serengeti wachache (serengeti - wasichana) hivyo ikijulikana wewe serengeti ni karate ilikua pride flani nzuri sana.

Hadi namaliza mafunzo mimi ni karatee!!

Itaendelea......

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
 
Angalau Ulipata pa kuenjoy kidogo.
 
Hukupiga hata moja ukaua mijusi tuu😅😅

Kwata sawaa raha ila unawajua KO wewe

Wazee wa Kazi ovyo ovyo😃😃

Nyie mnakula mchana mnalud uwanjani kupiga kwata wao wanaenda Hangani kuoga mkitoka Amala kuludisha silaha mnakuta wenzenu wapo wanasimuliana movie 😅😅😅😅ililkuwa inakera.. anyway jeshi sifa wepesi hatukosekani wa kujila😅😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…