Niliyoyashuhudia Jeshini

Nakumbuka nilienda kambi ya Kanembwa Kigoma kulikuwa na afande wanamwita " Cyborg" yule mwamba alikuwa hacheki alooh na anaogopeka balaa.

Mazoezi ya kule acha tuu kuna afande alikuwa anaitwa John Magesa na mwingine Dakanyama walifanya maisha yetu ya jeshi yawe magukumu.

Nilipata rafiki basi kwenye mchakamchaka alikuwa anapenda sana kuniimba " Sio lako Trudie la mchina hilooooo, umechoma sindano la mchina hilooooo, umepaka mafuta la mchina hiloooo" Nimekumbuka mbali sana
 
Mimi nadhani jeshini philosophy muhimu ni kuufanya mwili uondokane na uvivu! Kiasili mwili ni mvivu kufanya kazi na hapo ndo wengi wanafeli. Kwa mfano! Ili ufaulu mitihani ya darasani lazima usome! Ukitaka kusoma mwili hautaki unakuletea usingizi! Ili ufaulu inakutaka uamke asubuhi saa 11 kufanya maandalizi, n.k. kwahiyo nadharia ya kuushughulisha mwili jeshini ni muhimu! Mambo ya maharifa na technolojia utakuta darasani/shuleni
 
kabla ya kuingia kambini nilifuatilia vitu vingi kuhusu maisha ndani ya kambi jeshini, hvyo nilifungua moyo kabla hata ya kugusa lango la kambi ,nilifurahia kila kitu jeshini isipokiwa kitu kimoja tu mkianza rasmi zile wiki 6 mwendo wa kuruti huwa unabadilika mnatembe kwa mwendo wa (kunyanyukua) kuinua goti usawa wa kidevu huku ukiimba UP, UP, UP, UP. yaani hiko kitu ndo kilikuwa mateso makuu kwangu
 
KUNA COMMENTS ZINALALAMIKA HAWAJAONA UMUHIMU WA JESHI KATIKA STORY NI KAMA VILE MTOTO ANAPOTEZA MUDA...
Sikuainisha umuhimu nilijua wote kwa kusoma story A to Z mngeona umuhimu watoto tunaoupata kule.

FAIDA WATOTO WANAZOZIPATA KULE
1. Ukakamavu na utimamu wa akili na mwili; Nyakati ngumu kule zinaimarisha akili zetu uwezo wa kufikiria mambo kwa upana. Mazoezi kama viroba, mabio inaupa mwili utimamu.

2.Kuongeza nidhamu na utii; Kwa wazazi waliopokea watoto baada ya kutoka jeshi watakua shahidi wa hili, tukirudi tunakua wasikivu zaidi ya mwanza kabla ya kwenda jeshi.

3. Kujifunza kazi za mikono/kazi za nyumbani
Mfano mzuri mimi, nina uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila kuhisi kuchoka. Experience hii nilianza kuipata jkt mtu unapewa uwanja ufagie ukubwa kama nusu ya kiwanja cha mpira.

4. Ukitoka jeshi unakua na uwezo wa kuishi na watu wenye tabia tofautitofauti.

5. Inaongeza uzalendo na uelewa mpana kwa nchi yetu.


6. Inakuza vipaja na mafunzo mapya kwenye sanaa.
Mfano, Anna anapenda kuimba kipaji chake kilizidi kukuzwa, kuna walimu wa mziki kule ngoma coy.
Mimi nilipata mafunzo mapya ya karate kitu ambacho sikua nacho kabla ya kwenda jeshi.

7. Inaongeza ujuzi wa kujilinda dhidi ya adui na uwezo wa kulenga shabaha.
Kupitia mafunzo ya silaha kule range.
Asilimia kubwa ya waliotoka jeshi wapeni silaha muone kama hawajawafyatua.

8. Inatoa mafunzo ya kilimo
Kwenye mashamba/ bustani zao zinazopatikana kambini.
Mfano mimi nyumbani nina bustani yangu ya matembele, nimepanda na mahindi.

9.Inampa mtoto uwezo wa kujitegemea.
 

Aisee mi ningeitoa mapema sana uwiii
 
Nishajiapiza, nikipata mtoto wa kike mzurii yani ule uzuri wa kila mtu lazma ageuze shingo halafu akawa laini na moyo wa ustahimilivu hana.
Jeshi hatoenda labda waje wamchukue wakiwa na mitutu mizito

Kwanini mkuu
Mdogo wetu wa mwisho ni pisi kali rangi ya mtume akienda huko nna wasiwasi wajinga wasije muharibu uwiii[emoji2304]
 
@
Nakubusu
 
Kwanini mkuu
Mdogo wetu wa mwisho ni pisi kali rangi ya mtume akienda huko nna wasiwasi wajinga wasije muharibu uwiii[emoji2304]
Kama ni mpambanaji haina shida na wala usiogope sana kwa sababu mahusiano ni sehemu ya maisha ila tu yasifanyike kama namna ya kutaka favour. Kwa hiyo kuna watoto wa kike wenye mentality ya kuutumia mwili kuepuka shurba, hiyo ndio maana yangu

Hata hivyo, jeshini warembo ni wengi tu kama uraiani na wanakaza fresh tu. So, usiogope πŸ˜πŸ™πŸ½
 
Umesema ukweli mtupu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…