Niliyoyashuhudia Jeshini

Kunywa maji punguza hasira mkuu!
 
Course ya kujitolea nisingetoboa
haina utofauti na yenu...wao pia ni short course tu... syllabus yenu na yao haijatofautiana...hivyo unge toboa...

ndio maana Mujibu, na Wazalendo huwa kufa kwenye mazoezi ni nadra sana labda mtu awe alikuwa tu na maradhi yake mwenyezi Mungu akampenda.

full course ndio Balaa ili wakufunzi waonekane wamefanya kazi lazima askari wakate moto...!😭😭😭

 
Usiku wa kuamkia sherehe ulikua mzuri, nilipata kombati na buti kama nilivyotamani
Siku ya sherehe niliperform vizuri karate

Nilifurahi nimemaliza course, kesho nikapanda kwenye gari kurudi home hapo nikapata hisia a huzuni nikahisi kumiss jeshi kabla hata ya kufika nyumbani.

Nilivyoshuka ubungo sista angu alikuja kunipokea, naongea nae kwenye simu kumuelekeza nilipo aje kunifata

Nikashangaa mtu amefika nilipo halafu ananipita, nikamuita "dada" alivyogeuka akaanza kucheka "Aisee ndo umekua hivyo! Unajua sikukujua kabisa umebadilika"
Nilivyotoka jeshi nilikua mweusi sana

Mama alifurahi kuniona
Mwanzoni walikua wananishangaa jinsi nilivyochangamka nimekua mchapakazi.

Wadogo wa kupiga nao story kama
ulivyouliza sikua nao, mimi kwetu ndo lastborn.
 
Kila baada ya page ngapi huwa unaendelea
 
Story nishaandika nimemaliza
Safi hongera sana nitakutafuta unisimulie na unioneshe makovu. Wale askari wabaya sana wana roho mbaya wanakutesa binti hujazoea shida? Toka juzi sijalala nawafikiria. Naweza pata majina yao? Pole sana ephen_ ni mijitu tu yenye roho mbaya inafanyia hivyo wenzao.

Pole pia kwa kuandika. Vidole vitakuwa vinauma. Nikupeleke Hosp? Wakaangalie visije kuvimba au kukakamaa. Pole. Next time utaniambia nikutafutie mtu wa kukusaidia kuandika.
 
Aisee! Unajua kuapologize
Asante kwa hizo offers...
 
Aisee! Unajua kuapologize
Asante kwa hizo offers...
Ooooh... Kweli? Nisamehe kama nilikukwaza. Ni mabhangi tu haya napovuta sometimes yes sometimes no. Dr. Kanishauri nikivuta bhangi nisiwe nawasiliana na mtu.

Karibu sana. Je unakunywa wine? Nimtume mtu akuletee. Pole pia kwa uchovu maana kusoma hizi text kunachosha pia.
 
Yale yaishapita sina kinyongo na wewe,
Nilichukulia unachangamsha genge.

Bhangi sio nzuri kwa afya punguza ukorofi, kwani wewe hauogopi kupigwa na watu wenye hasira kali?

Mimi wine situmii, Asante hata hivyo!
 
Yale yaishapita sina kinyongo na wewe,
Nilichukulia unachangamsha genge.

Bhangi sio nzuri kwa afya punguza ukorofi, kwani wewe hauogopi kupigwa na watu wenye hasira kali?

Mimi wine situmii, Asante hata hivyo!
Kupigwa siogopi. Mi huwa naogopa kupiga tu. Vijana wa siku hizi hawana kitu nale nale sana. Mi huwa nawatandika tu vibao. Ila nitapunguza ukorofi kama ulivyonishauri. Mi wala si mbishi. Ila wakinichokoza nitawatandika makofi na nimeshawapa warning pia wasikusumbue. Wananielewa huwa sipendi upuuzi. Ukiwa na tatizo lolote lile nijulishe.
 
Noted
 
umekuja kula hapa
 
Ngoma coy aka nengu nengu,wanakuwaga walaini sana watoto wa michezo coy.

Kuna jamaa angu alikimbilia nengu nengu baada ya mziki wa kombania kuwa mgumu.

Jeshini kitengo mura,ukiwa na kitengo shuruba zinakuwa chache,kama ukipata nafasi ya kujichanganya kwenye kitengo nenda,iwe ujenzi ,iwe ngoma,iwe mpira au sanaa yoyote

Kukaa bila kitengo ina maana utakuwa kombania mda wote,na kombania haipumziki ,kila kazi zinatazama kombania,kwa hiyo ukiwa kombania kila kazi utafanya,iwe kubeba magogo,kupasua kuni,kubeba tofari,kung'oa visiki,kulima ,kuvuna nk.

Na vibangala vya watu wetu vinakuga na usimamizi sana ,unakuta maafande wapo zaidi ya mmoja mana mnakuwa kuruta wengi hivyo usimamizi unakuwa sio wa mtu mmoja,hali kwenye vitengo usimamizi unakuwa wa viongozi wa kawaida au hakuna kabisa ni kujisimamie wenyewe tu,

Watoto wa kota huwa wanaenda jeshini wana abc za kutosha ,hiyo husaidia kukabiliana na upepo wa kule.
Jeshini ubishi hakuna ,kila kitu ndio afandee hata kama kinakukera moyoni, utafanyaje ,ndo mana unaambiwa fungua moyo

Kumaliza ukuruta ni kazi ngumu sana ,hadi ndege wa angani wakipita wana wahurumia .
Utapauka,utakonda,ngozi itabadilika,wana kutoa umaarufu,hata kwenu ni mambo fresh lakini utakuwa sare tu na mtoto wa mkulima[emoji1][emoji1][emoji1]YAANI NDO MAANA HALISI YA KUKUTOA URAIA NA KUWA ASKARI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…