SEHEMU YA 6
NIKAFUNGUA MOYO
Nilifungua moyo niliona sina jinsi pale siwezi kutoka, mateso upande wangu yalipungua kuna ratiba za jeshi nikaanza kuzipenda hivyo sikuons mambo tena kama mateso ila njia ya kujifunza.
Kwanza, saa 10 alfajiri filimbi ikilia nawahi kombania inapigwa rokoo.
Baada ya pale wanaita wagonjwa njoeni upande wa huku, wazima pangeni mistari mabio yanaanza uelekeo road kuu. (Mabio- Jogging)
Nilikua nakimbilia mabio bila kulazimishwa nilikua naenjoy zile chenja sababu zinaongeza morale na My favourite ni hii; (Nimesahau maneno ila anayekumbuka naomba aniandikie)
🎶Kimbwekombweko cheza!
Kimbekele cheza....🎶
WEEK 6
Nakumbuka tulikua kombania usiku tumekaa chini kwenye vumbi bakabaka ana dumu na fimbo akipiga 1 tunasimama akipiga 2 tunachuchumaa akipiga 3 tunalala chini zoezi, push up za kutosha ila hapa girls tulikua tunachekesha sana hizo pushup zetu! Tulikaa mpaka saa 5 tukaenda kulala
Mimi nilikua nikirudi Angani naenda kuoga, kupiga mswaki na marafiki zangu tukirudi tunavaa nguo kabisa ndo tunalala ili filimbi ikipigwa hiyo saa 10 alfajiri ngoma uelekeo kombania.
Basi alfajiri ikafika kila mtu kafunga kikombe chake kwenye pitshort sababu tuliambiwa kuna dharula hivyo kila mtu aende na kikombe kakifunga kwenye pitshort angani kutafungwa hivyo hakuna atakayeweza kuingia.
Kama kawaida mabio umbali kutoka Gongo la Mboto hadi Airport nilikua naenjoy mabio.
Tumerudi kushakucha! tukaambiwa tupange foleni kazi imeanza.
Nilijuta upya kwenda jeshi, Bakabaka wakaanza kurutaaaa fungua moyo kazi imeanza! wote kichurachura uelekeo huu hapa basi tunawafata kwa kichurachura huku wanatuonyesha maeneo ya jeshi kama nyumba zao, jikoni, utawala, mazingira yote. Vuta picha kambi za jeshi zilivyo kubwa sasa tunazunguka kwa kichurachura, mkichoka mnaroll.
Tukachukuliwa hadi kwenye bonde tukaambiwa aya lala chini roll mpaka darajani! Huwa nahisi kambi nyingi zina madaraja chini mteremko wa maji.
Tulikua kimafungu hivyo ni rahisi kusimamiwa na kila mtu anafanya kwa uangalizi mkubwa.
Wazee nikaanza kuroll mpaka darajani nilihisi dunia chungu, kilio sio cha nchi hii njia yenyewe ina kokoto, vumbi.
Tumefika darajani kuna mteremko wa maji yanapita njia bakabaka akasema aya tumbukieni humo ndani ya daraja, muoge sababu tokea mnekuja hamjaoga Sawa kuruti?? Tunaitikia "Ndio sawa afande"
Aisee tukatumbukia fasta sababu ukiremba cha moto utakiona
Wakatuambia hakikisha umejipakaza poda ya kutosha mwili mzima umekua mrembo ndo utoke (poda- vumbi, matope).
Sasa katika harakati za kujipaka matope kuna kitu kikanichimba gotini sijui mpaka leo ni nini damu zikaanza kumwagika kama zote goti linauma
Ikabidi wanitoe nikapelekwa zahanati kufungwa bandage hiyo siku ikawa ponea yangu
Ila wenzangu walisota sana.
Mchana sasa muda wa kula tukaambiwa kila mtu akachukue tofali kituoni dakika 5 uwe usharudi kuchukua msosi.
Mimi nina kidonda nikajua nitaonewa huruma kumbe holaa nikaenda kubeba tofali tunabeba kwenye kipara, wengine wakaeka ngata ya box!
Tulivyofika jikoni wakaanza kukagua walioeka ngata wakakusanywa wakapewa trip zingine wabebe matofali ndo wachukua msosi.
kuruta wengi tulikua tushafungua moyo, vilio malalamishi yalipungua sana.
Baada ya msosi kuruta wote uelekeo shambani hamna kupumzika.
Mjeda namesake akamfata bakabaka "Naomba mabinti wachache wakasafishe maeneo ya mkuu wa kambi
Basi na mimi nikachukuliwa ikawa ponea yangu, mkuu wa kambi alikua anaishi pale.
Jioni tukaenda kula after filimbi uelekeo kombania uwe umemaliza kula ama lah, nikaenda
Tukaanza kufundishwa kwata hapo usiku tunafundishwa zile nyepesi za mwanzo
Hapa nilipata mtihani mpya!😂 nilikua Nanga hatarii mkono siwezi kutupa ipasavyo usiku ule nilichezea mapanzi ya kutosha.
Kwanini wanaojitolea ni wakatili vileee?
Itaendelea.....
Muendelezo soma
Niliyoyashuhudia Jeshini