Niliyoyashuhudia Jeshini


Yaani falsafa ya jeshi ni kutotabirika🤣🤣🤣.

Wakati wewe unadhani umefanya la maana kuliko wenzako,unachukuliwa kama mbinafsi.

upo wakati linafanyika kosa mkiwa kikundi,mnaanza kupewa adhabu,ole wako unyanyue komwe eti unamtaja aliyetenda kosa,utafurahi.
 
Kuna jamaa yangu nilisoma nae o level, mi Niko chuo udsm nimepanga zangu gheto akawa anakuja kuncheki, yeye kamaliza diploma hakuenda advance, katika kusaka ajira jamaa akaenda jeshi... Hapo hajaniambia nashangaa tu jamaa hapatikani hewani... Basi bana inapita kama miezi mitatu nashangaa tu siku jamaa huyu hapa gheto, kakonda kapauka Kawa kituko namuuliza jamaa vipi? Ananiambia man acha tu nimetoroka jeshini...

Jamaa alikua Kambi Tanga sijui ni ipi hasa, ananiambia jeshi pamemshinda amekimbia, anadai ashazimia kama mara mbili anajikuta anazinduka hospitali ya jeshi, akampiga mahesabu mara ya tatu hii itakua mazima.... Jamaa ananiambia sijui alipataje upenyo akawa ametoroka anatembea tu porini hajui hata Yuko wapi... Anadai alitembea kama siku mbili anahangaika tu akawa anahofia akitokea baharini itakuaje...

Au akishikwa si mtahisi labda alikua spy, yaani hofu kama zote, baada ya hizo siku akatokea Kijiji flani hajui hata ni wapi, hapo ana mavazi ya kuruta bado anahisi atashikwa tu, akaenda duka Moja akaomba kuazimwa simu akampiga mama yake akamuelezea yote, akatumiwa hela ndo akanunua nguo zingine na kuulizia mambo ya usafiri ndo mpaka kurudi dar... Akawa anaogopa kurudi kwao watamtafuta... Akawa anakaa gheto kwangu


Jamaa alikua ananipa visa vya kuchekesha sana na aliapa hatakaa akanyage jeshi tena, uzuri baada ya kama miezi 6 alipata zake ajira serikalini mpaka Leo Yuko kibaruani anakomaa
 
Mambo kama haya matam sana mkuu
 
Shukran
 
Mmh.wengine bado wana moyo wa kiraia asee
 
Exactly mtoto wa kota Ana advantage kubwa hao watu amekaaa nao Kwa muda mrefu
 
Kuna uzi kwa kijeshi kwa vijana walio pita jeshini ,kwa miaka ya 1970s-1990s ni wa moto sana ,utafute hutajuta simulizi zilizomo
Mzeee wangu Moja siku nilikuwa na piga nae story anasema siku hizi ma brigedia wamekuwa wengi sana njia ya mwenge una weza pishana na gari Tano au Saba zote za ma brigedia .....anasema Enzi zao wako kazini wapya , jamaaa amekaaa kazini miaka 2 ajawahi kuonana na brigedia siku amekuja Kumuona alipagawa jinsi kachafuka vyeo Kwa wenge,alipiga saluti mikono yote miwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…