MarkHilary
JF-Expert Member
- Feb 8, 2015
- 1,813
- 2,188
Duh
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawasawa...Hivi kwanini hawaruhusu kukumbatiana/ kukumbatia raia na combat ila wakiwa huko ni ruksa kukatika na combat 😂
Hivi kuna Combatant asiyekuwa na matusi? Hawa watu ni kisima cha matusi.
Miaka hiyo walikuwa wachache sababu population ilikuwa ndogo na Kambi zilikuwa chache na hakukuwa na succession planMzeee wangu Moja siku nilikuwa na piga nae story anasema siku hizi ma brigedia wamekuwa wengi sana njia ya mwenge una weza pishana na gari Tano au Saba zote za ma brigedia .....anasema Enzi zao wako kazini wapya , jamaaa amekaaa kazini miaka 2 ajawahi kuonana na brigedia siku amekuja Kumuona alipagawa jinsi kachafuka vyeo Kwa wenge,alipiga saluti mikono yote miwili
.😂😂 alikuwa mzito nini? Au tu uvivu.. kuna ule mwendo wa kurusha miguu usawa wa kifua sjui vile’ ulinisumbua pia, nikawa nanga, ila sio nanga pro max.
🤣🤣🤣🤣..
Uko kwa wapi jirani...tukuone🤣Haha sahivi nishakuwa mdada mkubwa.. nimepunguza viuvivu/ kulia lia.
Habari!
Nilipomaliza form 6 zikatoka nafasi za kwenda jeshi wanaita "kwa mujibu" basi nikaangaza macho yangu kwenye orodha nikaona "Ephen - Rukwa"
Basi nikafurahi sana, furaha haikua kwasababu naenda jeshi hapana. Hata mpango nayo nilikua sina ila tu niliona ni bahati jina langu kua kwenye list sababu sio wote uchaguliwa.
Nikawasiliana na marafiki zangu kuna baadhi walichaguliwa pia lkn hakuna niliyechaguliwaa nae kambi moja, nikaanza kusikia story plus video za status, instagram watu wanaeka makuruta wanavyogaragara kwenye matope, mazoezi magumu hadi wanalia, nikapata uoga hapo ikawa mzozo nikasema mimi jeshi siendi kwanza kunyoa kipara hapana.
Mzee akaniambia lazima uende, huko Rukwa mkuu wa kambi ni rafiki yangu hivyo wewe mateso hutoyapata nikafikiria nikaona huyu mzee ananipiga fix ili nijae mimi jeshi siendi.
Ila nikawa nataka sitaki na kilichokua kinanitatiza kwenda ni yale mateso tu niliyokua naona kwenye video.
Kuna siku rafiki yangu akanipigia simu kunishawishi twende ila akaniambia "Ephen twende kambi ya mkoa X achana na Rukwa huko wana mazoezi makali sana" nikamwambia kama hivyo fresh acha nijiandae tutaenda next week sababu deadline ilikua bado. Rafiki yangu nampa jina Anna.
Anna ana kaka ake ni mjeda sasa akawa anatupa tips muhimu za kuzingatia mojawapo alisema tranka tutakalobeba tusijaze vitu vingi tuweke vitu vyepesi ikiwezekana vitu tukanunue kambini hukohuko.
Mimi niliona usumbufu yaani nitoke na tranka tupu vitu nikanunulie kambini? nikanunua vitu vyote nikajaza kwenye tranka. Kumbe yule mjeda alikua na maana yake Aisee bora ningemsikiliza.😂
SIKU YA SAFARI
Tukatoka zetu na Anna tukapanda gari tunaenda kambi ya mkoa X japokua tumepangiwa kambi tofauti kila mtu.
Tupo kwenye gari nina furaha naenda kupata experience mpya pia nilifurahi kwenda mkoa mwingine sababu nimezoea dar tu, safari ilichukua almost masaa 7 tukafika huo mkoa X mjini, gari ndo mwisho.
Sasa wote hatujui nini kinafata hapo Anna yeye tranka lake niseme lipo tupu kabeba vitu muhimu tu, mimi nimejaza hadi kubeba linanishinda.
Tukamfata konda kumuuliza, "Sisi tunaenda kambi X tunaomba utupe muongozo" akatuambia pandeni bajaji hadi kituo flani mkifika kuna hiace zinaenda huko jina la kambi ndo jina la kituo cha kushuka.
Tukafanya kama alivyotuambia, tumeingia kwenye hiace asilimia kubwa wana vipara hivyo nikajua wote tunaenda kambini.
Kule tuliposhuka na gari nilipapenda sana ni kuzuri panavutia hamna pilikapilika nyingi nakumbuka nilimpigia simu mama, akaniuliza umepaonaje nikamjibu kwa furaha ni pazuri nimepapenda akaniambia "ukifika kambini nijulishe lkn ukiona huko mateso yamezidi nipe taarifa nikufate urudi nyumbani"
Basi tulivyokua kwenye Hiace tunaenda huko wilaya yenye kambi mwanzoni nasmile na Anna wangu ghafla akili yangu ikavurugika tuliingia barabara ya vumbi sijawahi ona, gari zima hatuonani, kila mtu kwenye gari katapakaa vumbi hadi kope zote nyeupe ndani ya pua nywele vumbi hapo nikapata sign ninapoenda sio pazuri.
Safari ilichukua kama masaa 3 tukaambiwa wale wa kambini mmefika.
Katika maisha yangu bad moment niliyowahi kuexperience ni hii siku, Tumeshuka tu nikaona njia ya vumbi imekata kulia ni ndefu kama 2km nikasikia sauti "Hapohapo wote chuchumaa tranka kichwani ruka kichurachura uelekeo huu hapa kwenda kambini" Kudadeq ndo nikajua kwanini niliambiwa niende na tranka tupu
Anna yeye chap kachuchumaa tranka kichwani, mimi machozi yashaanza kunitoka nikamwambia Anna mimi nimeghairi siendi narudi nyumbani, hata sijamaliza sentensi nishakula bao la mgongo kutoka kwa mjeda akaanza kufoka wewe bila shaka umetoka Dar naongea tii Amri kwanini umesimama ? Aya tranka kichwani kuruka uelekeo huu.
Akaja mjeda mwingine akanitwika tranka kichwani hapo nishachuchumaa sikuweza kuimili kuruka na tranka.
Anna akaniambia lete nikusaidie chukua langu, yule mjeda aliona tu hata akinipiga ule mzigo siuwezi na Anna pia hauwezi akamwita service man (mjeda anayejitolea) chukua hili tranka wasaidie, basi nikapona hivyo.
Kimbembe kikawa hiyo kichurachura nikiangalia mbele sioni geti, ni mbali almost 2km ndo niruke kichurachura? Hapo machozi yananitoka nalia nkamwambia Anna "mimi namwambia mama anifate siwezi hizi mambo" Anna nae analia Ephen usiondoke ukaniacha mwenyewe bora hivi tupo wote Afadhali.
Nilihisi miguu inawaka moto inataka kupasuka, msafara tupo wengi hadi wanaume wanalia, sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia.
Itaendelea...
Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
Haha ndio naliona hili swali aisee Mshamba unataka nijibu hapa mbele ya kadamnasi kama wewe ulivyouliza?🤣🙌Shem Lovie Lady umemfungia wapi au ndo basi tena imebaki stori😅
Kwa sasa unasoma au unafanyakaz
ndo maana unafunga pm🤣 ushakua miss jfMbona sipo tayari kuliongelea hilo.
Usigofu jf ni kisiwa cha uhuru na amaniMbona sipo tayari kuliongelea hilo.
Sijakulazimisha sweetheart. Na hata sitafanya kutokuelewa uhuru wakoNdiyo lakini nimechagua kutosema
YeaAsante.
Nilikulia jeshini(kota) kama mtoto wa mjesh binafsi sipendi kuwa mjesh, nilikataa miaka ya 90. Enzi zile hata la 7 unaenda ki urahisi. Ila nawapend sana wanajeshi....yaan wakipiga kwata parade hunitumi dukani. Baba alikuwa mstar wa mbele kwa hiyo nilikuwa kwenye sherehe nakaa mbele kabisa hata kofia ikianguka naiokota namvalisha, I like soldiers. So so much.Asante.
JEshi ni kipaji sio kila mtu anawezaNilikulia jeshini(kota) kama mtoto wa mjesh binafsi sipendi kuwa mjesh, nilikataa miaka ya 90. Enzi zile hata la 7 unaenda ki urahisi. Ila nawapend sana wanajeshi....yaan wakipiga kwata parade hunitumi dukani. Baba alikuwa mstar wa mbele kwa hiyo nilikuwa kwenye sherehe nakaa mbele kabisa hata kofia ikianguka naiokota namvalisha, I like soldiers. So so much.
Japo baba alipend niende na wkt huo nikiwa la 7 kwenda form 1 .. nikaenda ilboru mzee akajaa kimya hadi leo hanikumbushii
Kwani nilazima kukaa kambini Ndugu Mwandishi!?? Mbona wengi tuko nao huku Buhongwa na Draft pamoja na Shimhaa tunapimianaJEshi ni kipaji sio kila mtu anaweza
Kwanza kukaa kambini ndo kitu kinanifanya nisivutiwe na jeshi
Japo napenda MP sanasana wa kike wakiwa kwenye uniform zao jinsi wanavyowaka.