Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Binafsi sijui ila naona JKT hasa hawa Mujibu naona ni upotevu tu wa muda kwa kupima Faida zaidi naona hakuna cha maana ni kupoteza pesa kwa kuwahudumia!!!Unafikiri ulifundishwa uzalendo jeshini, kuijali nchi yako?
Kwanini hawana sera za kufundisha kilimo cha kisasa, umwagiliaji, kutumia trekta, mbolea, mbegu bora au wanavyo?
Inatakiwa kijana akitoka pale awe mzalendo, mchapakazi, anaweza kujitegemea na kuwa na ujuzi.
Mkuu fikiria vizuri kama ulichosema ni sahihi.Binafsi sijui ila naona JKT hasa hawa Mujibu naona ni upotevu tu wa muda kwa kupima Faida zaidi naona hakuna cha maana ni kupoteza pesa kwa kuwahudumia!!!
May be wale wa kujitolea naona at least!!
Daaa Poleee sanaa kwa siku hii ambayo pia uliwaponza wenzako ephenSEHEMU YA 8
Nikafanikiwa kutoroka hadi jikoni, kule maeneo mengi giza ndo maana sikubambwa
Nikanunua maandazi nikanywa na chai haraka, sasa nikawa naona kuruta wanakimbia wameruhusiwa kwenda kulala
Sasa nikawa nasuuza kikombe fasta na mimi nikalale
Kwa mbali namuona bakabaka anakuja na service man ( wanaojitolea) wetu
Basi service man akasema "Ephen mwenyewe yule pale" moyo ulishtuka ukaenda kasi sana
Nilipokea mvua ya matusi kutoka kwa yule bakabaka halafu mwanamke "Wenzako wapo kombania wewe huku unafanya nini? Nikaongezewa bao la mgongo
"Kuruta naongea unanitizama badala ya kupunguza urefu?'
"Punguza urefu haraka!"
Basi nikachuchumaa ndo kupunguza urefu.
Pembeni kulikua na bomba la maji nikapelekwa pale yakafunguliwa nikaloa chapachapa
"Aya roll uelekeo kombania"
Ilikua ngumu kwangu njia ya kuroll ina kokoto, mimi nina kidonda kibichi gotini kinaniuma na nimefungwa bandage.
"Afande naomba unibadilishie adhabu nina kidonda kibichi"
kuruta unanidindia?
Nikaona huyu anataka kukuza mambo! Nikaanza kuroll goti maumivu kama yote damu zikaanza kutoka na afande hanionei huruma
Kulikua na umbali hadi kombania ila nikafika!
Wenzangu walivyoniona wakaanza kunisonya wanalalamika.
Kombania zipo A hadi D kama sijakosea, A, C na D wakaruhusiwa kwenda kulala muda mrefu tu.
Na kombania B wanaume waliruhusiwa pia kasoro wasichana ndo hawakuruhusiwa sababu hawakutimia
Nani hakutimia ni mimi hapa.
Jeshini ikitokea kuruta ametoroka kwenye kombania hamuendi kulala hadi apatikane.
Muda huo saa 7 usiku damu zinatoka gotini maumivu hadi nalia.
"Sasa sikieni! Leo mnakesha na mimi hapa! mpaka asubuhi!
Nyie si hamjaiva, mlimtuma mwenzenu akanywe chai muda wa kombania haya wote kichurachura mnaenda na kurudi hadi kukuche, Wazii kuruta?
Kuruta wenzangu wakaanza kulia "Afande sisi hatujamtuma! Tunaomba tukalale"
Nauliza tena "Wazii kuruta?"
Tukaitikia waziii Afande!
Huku wenzangu wananitukana nimewaponza hawaendi kula utawala (kula utawala- kupumzika)
Bakabaka sasa "Kila mtu akachukue ndoo ya maji mje kumwaga hapa na poda ya kutosha mje mumpake usoni" 😄 (Poda-Vumbi)
Nililia sana basi wakaenda kuchukua poda wakanipaka, maji yakamwagwa kwenye vumbi kukawa na tope nikaambiwa,
"Wewe siumekuja hapa kula! Aya twende kama kambare"
Nikaanza kuroll kwenye tope.
Yule afande alikua na roho ngumu sanaaa
"Aya kuruta simama hapo uanze kupiga makofi wao wanafatisha"
Nikaanza nikipiga kofi wanasimama nikipiga wanalala chini! Ngoma ilienda hadi afande akasema nasimama pale nyie endeleeni!
Kumbe aliondoka sisi tukaendelea tukidhani anatuangalia, tumeshtuliwa na filimbi ya alfajiri
Tulikesha tena na wenzangu!!
Walinichukia! siku hio nikawa na kazi ya kuwaomba msamaha. Niliwafanya wasilale tena kwa usiku mwingine ukijumlisha na siku 7 za mwanzo.
Itaendelea.......
Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
Najitahidi mkuu ila nashindwa kuoanisha kabisa hizo faida!!Mkuu fikiria vizuri kama ulichosema ni sahihi.
Ufisadi ni utamaduniNajitahidi mkuu ila nashindwa kuoanisha kabisa hizo faida!!
Uzalendo kama Faida na lengo namba moja Graduates wengi ndio majizi haswaa huku kazini!! Viongozi wetu wengi ambao wao walikaa JKT mwaka mmoja hawa ndio kabisa kila siku tunasikiliza report zao kwa CAG!!
Yaan ukiangalia Inputs ni kubwa ila Outputs ndogo
May be jaribu basi kunishawishi nikuamiamini jaribu mkuu!!
naisoma mara nyingi kana kwamba sijawahi kuisoma .nataka kuiwekea lamination akilini mwangu yaani stori yote na nzima pamoja na wewe mwenyewe ephen. Kama hili ni kosa na jinai basi acha tu nifungwe kwa ajili yako na story yako.Asante sana
Ulikua hujaisoma au unairudia?
Aya isomenaisoma mara nyingi kana kwamba sijawahi kuisoma .nataka kuiwekea lamination akilini mwangu yaani stori yote na nzima pamoja na wewe mwenyewe ephen. Kama hili ni kosa na jinai basi acha tu nifungwe kwa ajili yako na story yako.
Unaniogopa?Pm nimekufungia wewe kaa ukijua😂
Kwa nini?Kama ukoma
haiko hivyo unavyofikiria, nina katatizo ka 'explicit content'Mimi napenda Apples wewe unapenda kula maparachichi
hapanaBut you spoke your heart
Hajaelewa. Nadhan jkt ni kitu ambacho hatujakitumia ipasavyo, nataman nchi nzima wangehusika kwenda jkt, jkt inazalisha, watz sote tungehusika kuzalisha, nashangaa sana vijana kukaa mtaani vijiweni kuna vijana wana vipaji wamekaa navy, kumbuka usemi punda haendi bila bakora, ndio maana hamkuwapenda waliokuwa wanajitolea, kwa sabab wangesaidia sana nchi hii kwenda mbele.Mkuu fikiria vizuri kama ulichosema ni sahihi.