Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

Habari!

Nilipomaliza form 6 zikatoka nafasi za kwenda jeshi wanaita "kwa mujibu" basi nikaangaza macho yangu kwenye orodha nikaona "Ephen - Rukwa"

Basi nikafurahi sana, furaha haikua kwasababu naenda jeshi hapana! Hata mpango nayo nilikua sina ila tu niliona ni bahati jina langu kua kwenye list sababu sio wote uchaguliwa.

Nikawasiliana na marafiki zangu kuna baadhi walichaguliwa pia lkn hakuna niliyechaguliwaa nae kambi moja, nikaanza kusikia story plus video za status, instagram watu wanaeka makuruta wanavyogaragara kwenye matope, mazoezi magumu hadi wanalia, nikapata uoga hapo ikawa mzozo nikasema mimi jeshi siendi kwanza kunyoa kipara hapana.

Mzee akaniambia lazima uende, huko Rukwa mkuu wa kambi ni rafiki yangu hivyo wewe mateso hutoyapata nikafikiria nikaona huyu mzee ananipiga fix ili nijae mimi jeshi siendi.

Ila nikawa nataka sitaki na kilichokua kinanitatiza kwenda ni yale mateso tu niliyokua naona kwenye video.

Kuna siku rafiki yangu akanipigia simu kunishawishi twende ila akaniambia "Ephen twende kambi ya mkoa X achana na Rukwa huko wana mazoezi makali sana" nikamwambia kama hivyo fresh acha nijiandae tutaenda next week sababu deadline ilikua bado. Rafiki yangu nampa jina Anna.

Anna ana kaka ake ni mjeda sasa akawa anatupa tips muhimu za kuzingatia mojawapo alisema tranka tutakalobeba tusijaze vitu vingi tuweke vitu vyepesi ikiwezekana vitu tukanunue kambini hukohuko.

Mimi niliona usumbufu yaani nitoke na tranka tupu vitu nikanunulie kambini? nikanunua vitu vyote nikajaza kwenye tranka. Kumbe yule mjeda alikua na maana yake Aisee bora ningemsikiliza.😂

SIKU YA SAFARI
Tukatoka zetu na Anna tukapanda gari tunaenda kambi ya mkoa X japokua tumepangiwa kambi tofauti kila mtu.

Tupo kwenye gari nina furaha naenda kupata experience mpya pia nilifurahi kwenda mkoa mwingine sababu nimezoea dar tu, safari ilichukua almost masaa 7 tukafika huo mkoa X mjini, gari ndo mwisho.

Sasa wote hatujui nini kinafata hapo Anna yeye tranka lake niseme lipo tupu kabeba vitu muhimu tu, mimi nimejaza hadi kubeba linanishinda.

Tukamfata konda kumuuliza, "Sisi tunaenda kambi X tunaomba utupe muongozo" akatuambia pandeni bajaji hadi kituo flani mkifika kuna hiance zinaenda huko jina la kambi ndo jina la kituo cha kushuka.

Tukafanya kama alivyotuambia, tumeingia kwenye hiance asilimia kubwa wana vipara hivyo nikajua wote tunaenda kambini.

Kule tuliposhuka na gari nilipapenda sana ni kuzuri panavutia hamna pilikapilika nyingi nakumbuka nilimpigia simu mama, akaniuliza umepaonaje nikamjibu kwa furaha ni pazuri nimepapenda akaniambia "ukifika kambini nijulishe lkn ukiona huko mateso yamezidi nipe taarifa nikufate urudi nyumbani"

Basi tulivyokua kwenye Hiance tunaenda huko wilaya yenye kambi mwanzoni nasmile na Anna wangu ghafla akili yangu ikavurugika tuliingia barabara ya vumbi sijawahi ona, gari zima hatuonani, kila mtu kwenye gari katapakaa vumbi hadi kope zote nyeupe ndani ya pua nywele vumbi hapo nikapata sign ninapoenda sio pazuri.

Safari ilichukua kama masaa 3 tukaambiwa wale wa kambini mmefika.

Katika maisha yangu bad moment niliyowahi kuexperience ni hii siku, Tumeshuka tu nikaona njia ya vumbi imekata kulia ni ndefu kama 2km nikasikia sauti "Hapohapo wote chuchumaa tranka kichwani ruka kichurachura uelekeo huu hapa kwenda kambini"
Kudadeq ndo nikajua kwanini niliambiwa niende na tranka tupu

Anna yeye chap kachuchumaa tranka kichwani, mimi machozi yashaanza kunitoka nikamwambia Anna mimi nimeghairi siendi narudi nyumbani, hata sijamaliza sentensi nishakula bao la mgongo kutoka kwa mjeda akaanza kufoka wewe bila shaka umetoka Dar naongea tii Amri kwanini umesimama ? Aya tranka kichwani kuruka uelekeo huu.

Akaja mjeda mwingine akanitwika tranka kichwani hapo nishachuchumaa sikuweza kuimili kuruka na tranka.

Anna akaniambia lete nikusaidie chukua langu, yule mjeda aliona tu hata akinipiga ule mzigo siuwezi na Anna pia hauwezi akamwita mjeda anayejitolea chukua hili tranka wasaidie, basi nikapona hivyo.

Kimbembe kikawa hiyo kichurachura nikiangalia mbele sioni geti, ni mbali almost 2km ndo niruke kichurachura? Hapo machozi yananitoka nalia nkamwambia Anna "mimi namwambia mama anifate siwezi hizi mambo" Anna nae analia Ephen usiondoke ukaniacha mwenyewe bora hivi tupo wote Afadhali.

Nilihisi miguu inawaka moto inataka kupasuka, msafara tupo wengi hadi wanaume wanalia, sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia.

Itaendelea......
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Umechekesha sana kuanzia hapo ulivyoshuka kwenye gari
 
Interview huanzia kuanzia siku ya kwanza unaripoti hapo getini ripoti wanaandika huyu tumepokea ni selule yaani mtoto wa mama huyu Jeshi hamna kitu wanaweka na marks zinahifadhiwa.Baadaye kwenye Kila eneo la mafunzo unatizamwa na wafunzi tofauti marks zinahiadhiwa Kwa Siri baadaye Kuna lile zoezi la kulenga shabaha unatizamwa unaangaliwa uwezo wako Kuna hizo ajira wengine huondoka nazo siku ya kufunga mafunzo tu anaambiwa Kwa Siri wewe ukitoka hapa karipoti Jeshi Fulani Nenda na barua hii au ukifika pale jitambulishe wewe Fulani usimwambie mambo mengi faili lako litakuwa limemfikia
Sio kuwa tu kuwa umekanyaga JKT ajira ipo.Perfomance ilikuwaje huko .
Yah uko sahihi nakumbuka kuna mwanangu week moja kabla ya kumaliza alifatwa na VX. Walikompeleka hatukujua nikaja kumuona baada ya takribani miaka 6 mbeleni akiwa front kwenye msafara wa magu.

Kwa jinsi tulivyoingia nae mpka anaondoka kambini na jinsi alivyokuwa anapiga kaz na mazoez na shabaha aliyonayo mpka maafande wakawa wanahis huyu atakuwa usalama kaja kuchunguza huku.

Mwez mmoja kabla ya kumaliza mafunzo kuna wanafunzi wakaongezwa kama watatu tukawa nao jambo la ajabu, ila jamaa alipoondoka tu na wenyewe wakapotea kwenye mazngira ambayo mpaka leo hatukuyaelewa jambo ambalo baadae sana baaada ya kuunga dot's nikaelewa

Asikwambie mtu jeshini ni raha sana
 
Form six gani Hiace anaita Hiance? Halafu wewe huu uandishi wako ushaharibiwa. Hakuna kitu umebaki nacho. Ndo maana mzee wako alitaka uende jeshini ukakaze misuli ya matako. Umeshalegea sana. Mwanaume hawezi omba saidiwa na mwanamke na hawezi lia eti anamwita mama yake. Wewe ni takataka. Ondoka hapa na uzi wako.
Kwani huyu ni ME mkuu!
 
Hiyo ilikuwa interview ya kufa mtu swali la mwisho kupima kama una uwezo wa kikomandoo na IQ Iko juu sana na kupima muda umekaa kambini je mazingira ya nje wayajua vizuri au ukipewa ile ruksa siku mnaambiwa Leo mko huru uliitumiaje muda wote wa mafunzo? Kama hujui hata internet cafe Iko wapi na hujui Wana msàada wowote kwako?
Kusoma mazingira ni jambo la kwanza kufanyika mkuu, within few days wale watundu tulishajua mpaka vilabu vya pombe na njia za magendo. Kifupi nilikuwa doja with benefits 😂 najua chimbo na chocho nyingi ndani ya muda mfupi.
 
SEHEMU YA 2
Ilipoishia..........
Sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia......

Endelea
Mpaka tumefanikiwa kulifikia geti kuna kuruta waliozimia njiani, wengine kilio kikubwa mimi mmojawapo Aisee wanajeshi waheshimiwe sio kwa mazoezi yale.

Getini tukaambiwa aya kila mtu alale chini mnaingia ndani kwa kubimbilika tranka liache hapohapo, Niliona Afadhali kubimbilika kuliko kuruka kichurachura fasta wazee tukaanza kuingia ndani kwa kubimbilika wengi hapa tuliumia sababu chini kuna vikokoto .

Tumeingia tumekuta kuruta wengi sana tukaungana nao hapo mimi wazo langu ni moja tu KURUDI NYUMBANI.

Tukaanza kupangwa unaitwa jina unaenda upande mwingine zoezi lilienda hadi saa 4 usiku.
Sasa mjeda mmoja akasema tumeita wote nyie majina yenu hayapo vipi? Tulikua wengi kiasi, mimi nilitoa sababu kua nimepangiwa Rukwa lkn kule baridi kali siwezi nina matatizo ya mbavu.
Walituelewa wote tukaruhusiwa.

Sasa majina yakaanzwa kuandikishwa, mimi narudi nyuma mjeda akaniona akanita alikua mmama.
Wewe vipi mbona unarudi nyuma? Nikaanza kulia! Kumbe ndo naharibu akashout "Maafande njooni muone kuruta analia" wote wakaja "Kuruta unalia?" Ebu chuchumaa nikachuchumaa fasta maswali yakaanza unaitwa nani nikataja jina umetokea wapi nikasema, unalia nini nikasema Nataka kurudi nyumbani.... Wewe nilikoma!!! Aya simama twende squat 100 nikaanza kupiga squat huku machozi kama yote basi wanacheka

Sikuzimaliza nikaambiwa ungana na wenzako hapa kuna kuingia hamna kutoka.

MAMBO RASMI
Tukakusanywa uwanja wa damu (uwanja wa damu - uwanja wa mazoezi, paredi) hapo kumbuka hatujapumzika tokea tumefika tukaanza kupewa risala huku tumesimama ole wako usinzie, tupo wengi na wajeda wengi pia ukigeuka huyu hapa

Tukafunguliwa stoo, ipo pembeni ya uwanja tunaingizwa kwa mafungu "ingia toka na godoro ole wako uchelewe kutoka"
Wanajeshi wakali kitu kidogo ushakula tusi tena la mzazi huna cha kumfanya na ole wako unune😂
Mimi nilivyoingia chap nimetoka na godoro bahati nzuri yote ni mazuri yamejaa.

Mpaka tunaruhusiwa kwenda Angani (Angani - Hall la kulala) muda umeenda karibia alfajiri.
Nimeingia na marafiki zangu, hapo nimekutana na wale tuliosoma nao advance, sekondari tulikua kama 7 Anna akiwepo.
Tukashauriana tukaoge tulionyeshwa sehemu zote za muhimu mabomba, vyoo.
Sasa tunachota maji akaja mjeda anayejitolea akasema eee kuruta mnaenda kuoga sasa hivi? Sasa sisi tunabaki tunashangaa sababu tulikua kuruta wengi kumbuka hapo ni saa 9 alfajiri
"Bora mkalale dakika chache zilizobaki, muda si mrefu filimbi inalia"
Kudadeq " Anna mimi siwezi hapa kesho namwambia maza anifate" hapo nalia, wengi wanajuta kwenda jeshi muda huo.

Tukapiga moyo konde tukaenda kuoga, tunarudi lisaa hata haijafika tunasikia filimbi wajeda wakike kama wote wamekuja na virungu kutuamsha
Sasa hata hatujalala halafu tunaamshwa hii ni hatari.

Wengine waliolala bila kuoga wanaamka fasta wanachukua miswaki na ndoo eti wakaoge! 😂
Wajeda walitembeza virunguu! "Mnaenda kuoga kwani hamjasikia filimbi, hapa hamna kupiga mswaki wote uwanja wa damu fastaa" kiaina nilishukuru Mungu nimeoga sababu sio kwa vumbi lile plus kugaragara chini.

Tukakusanyika uwanja wa damu saa 10 alfajiri, Kuna wale wanaojitolea wanoko sana! Tukapewa watusimamie uelekeo mchakamchaka basi tukawekwa ki kombania, Mimi nikafight nikawa kombania B pamoja na Anna.
Uelekeo ukaanza jogging tumekimbia huku tunaimba plus wajeda nyuma na gari, hilo gari kumbe ni kwaajili ya kubeba wale watakaozidiwa njiani au kuzimia.

Sasa tunakimbia nikicheki tunapita ile road tuliyokuja nayo jana kutoka mjini. Nikafikiria kwahiyo tunaenda hadi mjini au? Basi sina jinsi tulikimbia sana wengine wanazimia njiani wanapakiwa kwenye gari umbali ulikua kama kutoka Gongo la mboto hadi Airport kwa wanaojua hizo sehemu wataelewa.

Wakati tunarudi huku tunakimbia kushakucha ndo tunaonana vizuri😄ilikua vichekesho tumeloa vumbi hadi kope ndani ya pua kote vumbi masikioni usipime ukimuangalia mwenzako unacheka huna mbavu.
Tumerudi kambini tunakutana na majembe, ndoo za michanga. Mimi nilijua tukirudi tunapumzika kumbe kazi inaendelea nilijihisi kukonda kwa siku moja.
Tukapangiwa kazi nikaangukia kwenda shamba, tena huko shamba ni kule tulipotoka kukimbia njia ile ya vumbi ya kutoka mjini katikati barabara pembeni kulia kushoto mashamba ya wajeda sina jinsi.

Tukapiga mguu huku nalia mbaya zaidi sikua na rafiki yangu niliyepangiwa nae kusema tungefarijiana, msidhani mimi mzembe wakuu hapana! Tuliolia tulikua wengi hadi wanaume, tena sikia hivihivi kwa ninavyohadithia kuliko ikutokee.

Njiani kuna mjeda akaniona ni wale wanaojitokea ni binti mzuri mweupe sijui alifata nini kule Wallah!
Akaniambia usilie utazoea mwaya, unaitwa nani nikamwambia Ephen, kumbe ni namesake wangu bhana akafurahi akaanza kunitambulisha kwa wale wajeda wengine huyu ni mdogo wangu. Kumbuka hawa wajeda tuliopewa twende nao shamba ni wale wanaojitolea sio waajiriwa.
Basi ikawa nafuu kwangu, "sasa huku tunaenda ni shamba kung'oa visiki, ningekujua mapema ningekupeleka kule shamba la kuvuna machungwa kule bata, ila usijali kesho utaenda huko" akaniambia

Tulifika shamba kama saa 2 hivi kazi ikaanza kung'oa visiki hawajali mwanaume wala mwanamke wote kazi kazi!
Kisiki kimoja watu watatu tena vile visiki vinene, nilipiga panga na jembe hadi marengerenge yananitoka nayaona
Nilisikitika sana nikajuta kwenda jeshi, nikakumbuka nyumbani nilijihisi nipo dunia ya peke yangu watu wote wameniacha.

Itaendelea......
Pole mwaya....
 
SEHEMU YA 3
Watu tunang'oa visiki huku tunasinzia, yule mjeda namesake akanifata "njoo huku" nikaenda sasa kuna vichaka vingi akanipeleka kichaka flani hivi majani yamekaa kimduara katikati uwazi upepo unapita. Akaniambia "lala hapo muda wa kuondoka ukifika nitakufata" nikapiga zangu mbonji.

Nakuja kushtuliwa na mateke, nimekurupuka namuona bakabaka ananitizama tena ana nyota mbili (bakabaka - mwanajeshi aliyeajiriwa) "toka huko chuchumaa hapa haraka" nikatii amri mzee.
Umefikaje huku? Swali nimepigwa...

Nikafikiria nikaona siwezi kumchoma mjeda namesake ni vyema nipambane na hali yangu.
Nikaanza kujitetea pale, "Mimi naumwa vidonda vya tumbo nimezidiwa nikaona nipumzike hapa" akamwita mjeda hana cheo akamwambia naomba umshughulikie huyu.
Yule mjeda akaniambia "adhabu yako utabeba kisiki kikubwa peke yako kupeleka kambini". Nikaona nishaanza kupata msala mapema muhimu nikurudi nyumbani.

Nimekaa kihuzuni mjeda namesake akaja "nimekutafuta kule sijakuona" nikamwambia nilifumwa nikampa mkasa wote akaniambia nisijali atanisaidia. Kweli saa 4 ikafika filimbi ikalia kisiki kimoja mnabeba watu wawili kwenda kambini. Yule bakabaka akasema yule mwenye adhabu yangu yuko wapi? Nikaenda akanipa kisiki kikubwa machozi yakaanza kunilenga.

Akaniambia unatoka mkoa gani nikamwambia Dar! Akacheka sana "mbona watu wa dar wajanja? Wewe kitu kidogo unalia ebu acha usen....."

Nikapewa kisiki kikubwa peke yangu yeye akaondoka, namesake akawapasia kile kisiki kuruta wengine, akawaita wakaka wawili akawaambia kisiki chao wanipe mimi changu wabebe. Hawakupinga fasta wakabeba.
Kama kawaida uelekeo kambini, umbali kutoka pale shamba hadi huko ni kama 2km, kutembea ni mchakamchaka.

Tumefika tukaenda dining, tukakuta bakabaka kama wote
"Aya kila mtu ana kikombe chake! chukua ndoo nenda kituoni kajaze mchanga ulete hapa ndo uchukue chai"
Kituoni ni kule siku ya kwanza tuliposhuka na gari
Njaa inauma, muda huo nikawa sisikii tena kulia ila hasira kama zote nikajuta kwenda jeshi.

Kufika huko kituoni michanga yenyewe ina maji, nikatiliwa mchanga nikamuomba yule mjeda aniwekee ndoo nusu sababu kipara plus ndoo ya mchanga nzito, akaniwekea.
Niliporudi jikoni kumbe bakabaka wanakagua kama ndoo imejaa au ipo nusu........

Tupo kwenye foleni ya kukaguliwa machozi yananilenga najua kabisa narudishwa nikajaze ndoo, akaja mjeda namesake akaniuliza "ndoo yako imejaa? Nikamwambia hapana
Basi kuna kuruta alikua anapita amerudishwa akajaze ndoo mjeda namesake akamwambia chukua mchanga wako muongezee huyu wewe ukajaze tena!

Yule akupinga akanijaziwa ndoo nikakaguliwa imejaa nikachukua chai na mkate.
Uzuri chai imekolea sukari na mkate mzuri mkubwa nikala nikashiba ila majonzi yakawa palepale ninayo moyoni.
Yaani siwezi kupewa msosi mpaka jasho linitoke???
Nikipata upenyo lazima nimpigie mama aje kunifata.
Unawaza mama tu😅😅
 
Back
Top Bottom