Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

Sehemu ya 13 ni episode ya mwisho
MITAPENDEZA kama utanalizia episode ya 14.
Tueleze usiku wa kuamkia sherehe ilikuaje,siku yenyewe ya sherehe uli perform vipi karate, usiku wake furaha ulikuaje, safari ya kurudi home.
Mama alikupokeaje stendi, wadogo zako walifurahí vipi kukuona tena stori zilikuaje mpaka muda wa kwenda kulala.
 
MITAPENDEZA kama utanalizia episode ya 14.
Tueleze usiku wa kuamkia sherehe ilikuaje,siku yenyewe ya sherehe uli perform vipi karate, usiku wake furaha ulikuaje, safari ya kurudi home.
Mama alikupokeaje stendi, wadogo zako walifurahí vipi kukuona tena stori zilikuaje mpaka muda wa kwenda kulala.
Kesho nitakuandikia episode ya kujibu maswali yako.
 
Hii thread ina chai chache ndio maana inavutia kusoma
Hakuna chai mkuu, mengi aliyoyasimulia ni kweli na kwa kiasi flani nimeona kama kambi yao ilikuwa na wepesi. Japo sometimes unaweza pangiwa kambi ngumu ila wakufunzi wanaosimamia kombania uliyopo wakawa fair kwa hiyo mnakula maisha

Mfano hiyo siku yao ya kufungua course ilikuwa nyepesi kiasi, kwetu sisi, group letu ndo lilikuwa la pili kwenye ufunguzi wa course kwa hiyo tulikuwa kama group la maabara, wanatest kitu wakiona impact kubwa, magroup yanayofuata wanalegezewa

Kiukweli kwangu ile siku nilikuwa naona kama naota 😁😁, yaani sikuwa naamini kama naaishi ile hali maana ilifikia stage watu wanazimia yaani hadi tunafika katikati ya safari, group letu lilikuwa na wasichana wawili tu..

Sipendi sana kusimulia hizi experiences ndo maana natoa juu juu tu ila amini kuna watu walipitia experience mbaya zaidi ya unayoisoma
 
Habari!

Nilipomaliza form 6 zikatoka nafasi za kwenda jeshi wanaita "kwa mujibu" basi nikaangaza macho yangu kwenye orodha nikaona "Ephen - Rukwa"

Basi nikafurahi sana, furaha haikua kwasababu naenda jeshi hapana! Hata mpango nayo nilikua sina ila tu niliona ni bahati jina langu kua kwenye list sababu sio wote uchaguliwa.

Nikawasiliana na marafiki zangu kuna baadhi walichaguliwa pia lkn hakuna niliyechaguliwaa nae kambi moja, nikaanza kusikia story plus video za status, instagram watu wanaeka makuruta wanavyogaragara kwenye matope, mazoezi magumu hadi wanalia, nikapata uoga hapo ikawa mzozo nikasema mimi jeshi siendi kwanza kunyoa kipara hapana.

Mzee akaniambia lazima uende, huko Rukwa mkuu wa kambi ni rafiki yangu hivyo wewe mateso hutoyapata nikafikiria nikaona huyu mzee ananipiga fix ili nijae mimi jeshi siendi.

Ila nikawa nataka sitaki na kilichokua kinanitatiza kwenda ni yale mateso tu niliyokua naona kwenye video.

Kuna siku rafiki yangu akanipigia simu kunishawishi twende ila akaniambia "Ephen twende kambi ya mkoa X achana na Rukwa huko wana mazoezi makali sana" nikamwambia kama hivyo fresh acha nijiandae tutaenda next week sababu deadline ilikua bado. Rafiki yangu nampa jina Anna.

Anna ana kaka ake ni mjeda sasa akawa anatupa tips muhimu za kuzingatia mojawapo alisema tranka tutakalobeba tusijaze vitu vingi tuweke vitu vyepesi ikiwezekana vitu tukanunue kambini hukohuko.

Mimi niliona usumbufu yaani nitoke na tranka tupu vitu nikanunulie kambini? nikanunua vitu vyote nikajaza kwenye tranka. Kumbe yule mjeda alikua na maana yake Aisee bora ningemsikiliza.😂

SIKU YA SAFARI
Tukatoka zetu na Anna tukapanda gari tunaenda kambi ya mkoa X japokua tumepangiwa kambi tofauti kila mtu.

Tupo kwenye gari nina furaha naenda kupata experience mpya pia nilifurahi kwenda mkoa mwingine sababu nimezoea dar tu, safari ilichukua almost masaa 7 tukafika huo mkoa X mjini, gari ndo mwisho.

Sasa wote hatujui nini kinafata hapo Anna yeye tranka lake niseme lipo tupu kabeba vitu muhimu tu, mimi nimejaza hadi kubeba linanishinda.

Tukamfata konda kumuuliza, "Sisi tunaenda kambi X tunaomba utupe muongozo" akatuambia pandeni bajaji hadi kituo flani mkifika kuna hiace zinaenda huko jina la kambi ndo jina la kituo cha kushuka.

Tukafanya kama alivyotuambia, tumeingia kwenye hiace asilimia kubwa wana vipara hivyo nikajua wote tunaenda kambini.

Kule tuliposhuka na gari nilipapenda sana ni kuzuri panavutia hamna pilikapilika nyingi nakumbuka nilimpigia simu mama, akaniuliza umepaonaje nikamjibu kwa furaha ni pazuri nimepapenda akaniambia "ukifika kambini nijulishe lkn ukiona huko mateso yamezidi nipe taarifa nikufate urudi nyumbani"

Basi tulivyokua kwenye Hiace tunaenda huko wilaya yenye kambi mwanzoni nasmile na Anna wangu ghafla akili yangu ikavurugika tuliingia barabara ya vumbi sijawahi ona, gari zima hatuonani, kila mtu kwenye gari katapakaa vumbi hadi kope zote nyeupe ndani ya pua nywele vumbi hapo nikapata sign ninapoenda sio pazuri.

Safari ilichukua kama masaa 3 tukaambiwa wale wa kambini mmefika.

Katika maisha yangu bad moment niliyowahi kuexperience ni hii siku, Tumeshuka tu nikaona njia ya vumbi imekata kulia ni ndefu kama 2km nikasikia sauti "Hapohapo wote chuchumaa tranka kichwani ruka kichurachura uelekeo huu hapa kwenda kambini"
Kudadeq ndo nikajua kwanini niliambiwa niende na tranka tupu

Anna yeye chap kachuchumaa tranka kichwani, mimi machozi yashaanza kunitoka nikamwambia Anna mimi nimeghairi siendi narudi nyumbani, hata sijamaliza sentensi nishakula bao la mgongo kutoka kwa mjeda akaanza kufoka wewe bila shaka umetoka Dar naongea tii Amri kwanini umesimama ? Aya tranka kichwani kuruka uelekeo huu.

Akaja mjeda mwingine akanitwika tranka kichwani hapo nishachuchumaa sikuweza kuimili kuruka na tranka.

Anna akaniambia lete nikusaidie chukua langu, yule mjeda aliona tu hata akinipiga ule mzigo siuwezi na Anna pia hauwezi akamwita service man (mjeda anayejitolea) chukua hili tranka wasaidie, basi nikapona hivyo.

Kimbembe kikawa hiyo kichurachura nikiangalia mbele sioni geti, ni mbali almost 2km ndo niruke kichurachura? Hapo machozi yananitoka nalia nkamwambia Anna "mimi namwambia mama anifate siwezi hizi mambo" Anna nae analia Ephen usiondoke ukaniacha mwenyewe bora hivi tupo wote Afadhali.

Nilihisi miguu inawaka moto inataka kupasuka, msafara tupo wengi hadi wanaume wanalia, sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia.

Itaendelea...

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
HiI riwaya ukitoa copy unikumbuke!
 
Hivi kwanini hawaruhusu kukumbatiana/ kukumbatia raia na combat ila wakiwa huko ni ruksa kukatika na combat 😂

Hivi kuna Combatant asiyekuwa na matusi? Hawa watu ni kisima cha matusi.
😂😂😂😂😂😂😂 Acha dharau wewe, kweli kukumbatiana na CBT hairuhusiwi ila ulivyoilinganisha na wale wanaokata viuno umenichekesha sana, kiukweli wapiganaji hawapendi sana bora wavae nguo zingine wale wa band na sanaa.
Sasa matusi si ndo kama sala la bwana we huijui? Ari na Morale
 
Ahaa kama ni hivi sawa kabsaa 😁😁

Kuna vitu kasifia sana kama ni sehemu ipo perfect flani ila kwa experience yangu nasimamia palepale. Mtoto wa kike mzuri sana na ana moyo mwepesi simpeleki

Wa kiume, hadi stendi namsindikiza, akakomae 😁😁
Kambi yetu bakabaka hawakua na hizo mambo jamaniii!!😄
 
Back
Top Bottom