Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

Tokea mwanzo nilijua wewe wa kiume. Nimekuja kujua sehemu ya 5. Sasa sijui nianze upya?. Maana kule mwanzo kote nimekuweka wa kiume. Kwa hiyo hata mawazo ya usomaji namsoma kiume. Sasa huku kuibadiri tena uwe wa kike,bila kuanza mwanzo. Daah..! Ngoja nisonge nayo kigumu
Sijajua ukiume umeonekana wapi mimi ni Miss!
 
SEHEMU YA 2
Ilipoishia..........
Sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia......

Endelea
Mpaka tumefanikiwa kulifikia geti kuna kuruta waliozimia njiani, wengine kilio kikubwa mimi mmojawapo Aisee wanajeshi waheshimiwe sio kwa mazoezi yale.

Getini tukaambiwa aya kila mtu alale chini mnaingia ndani kwa kubimbilika tranka liache hapohapo, Niliona Afadhali kubimbilika kuliko kuruka kichurachura fasta wazee tukaanza kuingia ndani kwa kubimbilika wengi hapa tuliumia sababu chini kuna vikokoto .

Tumeingia tumekuta kuruta wengi sana tukaungana nao hapo mimi wazo langu ni moja tu KURUDI NYUMBANI.

Tukaanza kupangwa unaitwa jina unaenda upande mwingine zoezi lilienda hadi saa 4 usiku.
Sasa mjeda mmoja akasema tumeita wote nyie majina yenu hayapo vipi? Tulikua wengi kiasi, mimi nilitoa sababu kua nimepangiwa Rukwa lkn kule baridi kali siwezi nina matatizo ya mbavu.
Walituelewa wote tukaruhusiwa.

Sasa majina yakaanzwa kuandikishwa, mimi narudi nyuma mjeda akaniona akanita alikua mmama.
Wewe vipi mbona unarudi nyuma? Nikaanza kulia! Kumbe ndo naharibu akashout "Maafande njooni muone kuruta analia" wote wakaja "Kuruta unalia?" Ebu chuchumaa nikachuchumaa fasta maswali yakaanza unaitwa nani nikataja jina umetokea wapi nikasema, unalia nini nikasema Nataka kurudi nyumbani.... Wewe nilikoma!!! Aya simama twende squat 100 nikaanza kupiga squat huku machozi kama yote basi wanacheka

Sikuzimaliza nikaambiwa ungana na wenzako hapa kuna kuingia hamna kutoka.

MAMBO RASMI
Tukakusanywa uwanja wa damu (uwanja wa damu - uwanja wa mazoezi, paredi) hapo kumbuka hatujapumzika tokea tumefika tukaanza kupewa risala huku tumesimama ole wako usinzie, tupo wengi na wajeda wengi pia ukigeuka huyu hapa

Tukafunguliwa stoo, ipo pembeni ya uwanja tunaingizwa kwa mafungu "ingia toka na godoro ole wako uchelewe kutoka"
Wanajeshi wakali kitu kidogo ushakula tusi tena la mzazi huna cha kumfanya na ole wako unune!
Mimi nilivyoingia chap nimetoka na godoro bahati nzuri yote ni mazuri yamejaa.

Mpaka tunaruhusiwa kwenda Angani (Angani - Hall la kulala) muda umeenda karibia alfajiri.
Nimeingia na marafiki zangu, hapo nimekutana na wale tuliosoma nao advance, sekondari tulikua kama 7 Anna akiwepo.
Tukashauriana tukaoge tulionyeshwa sehemu zote za muhimu mabomba, vyoo.
Sasa tunachota maji akaja mjeda anayejitolea akasema eee kuruta mnaenda kuoga sasa hivi? Sasa sisi tunabaki tunashangaa sababu tulikua kuruta wengi kumbuka hapo ni saa 9 alfajiri
"Bora mkalale dakika chache zilizobaki, muda si mrefu filimbi inalia"
Kudadeq " Anna mimi siwezi hapa kesho namwambia maza anifate" hapo nalia, wengi wanajuta kwenda jeshi muda huo.

Tukapiga moyo konde tukaenda kuoga, tunarudi lisaa hata haijafika tunasikia filimbi wajeda wakike kama wote wamekuja na virungu kutuamsha
Sasa hata hatujalala halafu tunaamshwa hii ni hatari.

Wengine waliolala bila kuoga wanaamka fasta wanachukua miswaki na ndoo eti wakaoge!
Wajeda walitembeza virunguu! "Mnaenda kuoga kwani hamjasikia filimbi, hapa hamna kupiga mswaki wote uwanja wa damu fastaa" kiaina nilishukuru Mungu nimeoga sababu sio kwa vumbi lile plus kugaragara chini.

Tukakusanyika uwanja wa damu saa 10 alfajiri, Kuna wale wanaojitolea wanoko sana! Tukapewa watusimamie uelekeo mchakamchaka basi tukawekwa ki kombania, Mimi nikafight nikawa kombania B pamoja na Anna.
Uelekeo ukaanza jogging tumekimbia huku tunaimba plus wajeda nyuma na gari, hilo gari kumbe ni kwaajili ya kubeba wale watakaozidiwa njiani au kuzimia.

Sasa tunakimbia nikicheki tunapita ile road tuliyokuja nayo jana kutoka mjini. Nikafikiria kwahiyo tunaenda hadi mjini au? Basi sina jinsi tulikimbia sana wengine wanazimia njiani wanapakiwa kwenye gari umbali ulikua kama kutoka Gongo la mboto hadi Airport kwa wanaojua hizo sehemu wataelewa.

Wakati tunarudi huku tunakimbia kushakucha ndo tunaonana vizuri, ilikua vichekesho tumeloa vumbi hadi kope ndani ya pua kote vumbi masikioni usipime ukimuangalia mwenzako unacheka huna mbavu.
Tumerudi kambini tunakutana na majembe, ndoo za michanga. Mimi nilijua tukirudi tunapumzika kumbe kazi inaendelea nilijihisi kukonda kwa siku moja.
Tukapangiwa kazi nikaangukia kwenda shamba, tena huko shamba ni kule tulipotoka kukimbia njia ile ya vumbi ya kutoka mjini katikati barabara pembeni kulia kushoto mashamba ya wajeda sina jinsi.

Tukapiga mguu huku nalia mbaya zaidi sikua na rafiki yangu niliyepangiwa nae kusema tungefarijiana, msidhani mimi mzembe wakuu hapana! Tuliolia tulikua wengi hadi wanaume, tena sikia hivihivi kwa ninavyohadithia kuliko ikutokee.

Njiani kuna mjeda akaniona ni wale wanaojitokea ni binti mzuri mweupe sijui alifata nini kule Wallah!
Akaniambia usilie utazoea mwaya, unaitwa nani nikamwambia Ephen, kumbe ni namesake wangu bhana akafurahi akaanza kunitambulisha kwa wale wajeda wengine huyu ni mdogo wangu. Kumbuka hawa wajeda tuliopewa twende nao shamba ni wale wanaojitolea sio waajiriwa.
Basi ikawa nafuu kwangu, "sasa huku tunaenda ni shamba kung'oa visiki, ningekujua mapema ningekupeleka kule shamba la kuvuna machungwa kule bata, ila usijali kesho utaenda huko" akaniambia

Tulifika shamba kama saa 2 hivi kazi ikaanza kung'oa visiki hawajali mwanaume wala mwanamke wote kazi kazi!
Kisiki kimoja watu watatu tena vile visiki vinene, nilipiga panga na jembe hadi marengerenge yananitoka nayaona
Nilisikitika sana nikajuta kwenda jeshi, nikakumbuka nyumbani nilijihisi nipo dunia ya peke yangu watu wote wameniacha.

Itaendelea...

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
😁😁😁😁
 
images - 2024-03-31T235702.122.jpg
 
99% alichoandika mleta mada ni kweli

nilipita Mtabila Jkt 825 kj kama kundi fulani maalumu lilipelekwa huku kupika kozi hio miezi 4 hivi

aisee siku za mwanzo sawa sawa kama mleta mda alivyosema bila kufungua moyo hutoweza

na kwa misosi aise jeshini wanakula vizuri sana kuliko hata baaadhi watu huko majumbani.

sema mimi nilikuwa naharisha daily sijawahi pata choo kigumu kwa miezi 4 sababu kwanza mikono ilikuwa michafu muda wote kutokana na kazi na kukaa chini yaani ilikuwa mekunda haitakati hata unawe vipi na sabuni.

pili, maji ya bomba ndio ya kunywa nimeumwa sana tumbo, amiba, na muda wa kujiuguza haukwepo.

unaenda kwenye mishe zao unajua kabisa hapa naumwa
Mimi pia nimepita hapo Op Magu
 
SEHEMU YA 5
Basi bhana simu ikapigwa wakaeka loudspeaker
Mama akaanza, "Ephen?"
Abee mama
"Eee niambie vizuri kuna shida gani huko au chakula cha shida?"
Hapana mama.. sasa naongea kwa kwikwi huku bakabaka ananikata jicho
Nikajikaza pale nikaongea nae akaniambia "nimeongea na mwanangu hapo, kaniambia ana jina kama lako atakuangalia vizuri jikaze sawa mwanangu?"
Nikaitikia ndiyo mama

Basi tukaagana rasmi na mama huku nikijua kumbe pale ndo nimefika mpaka miezi mitatu ipite.
Duh!! Sina jinsi zaidi ya kupambana na hali halisi.

CHAKULA CHA JESHI
Kwenye msosi jeshini nawapa hongera! nilijaribu kuulizia kambi zingine baada ya mafunzo jinsi walivyokua wanakula nao pia hawalalamiki.

Pale kambini asubuhi ni chai na mkate, mkate ni mkubwa mtamu mlaini wanapika wajeda kila siku.
Tena hawabanii kuongeza kama hujashiba.

Mchana ni ugali maharagwe na nyama, tena nyama ni moja ila kubwa kinyumbani ile ukiikata inatoka vipande vitatu. Na chungwa tumekula karibia kila siku
Kambi yetu ilikua ina shamba la machungwa.

Jioni saa 12 wali, maharage na chai siku mojamoja na mboga za majani. msosi umepikwa vizuri kama wa nyumbani
Huwa stress zangu zinaisha muda wa kula.

Kwenye msosi jeshini chukueni maua yenu.

MAVAZI YA JESHI
Hapa kwanza nicheke zile pitshorts kwa watoto wa kike sijazielewa kabisa, muda wa kukimbia , mazoezi zinapanda usawa wa mapaja inakua kama boxer.

Tukiwa kombania mapaja yoye nje tunaona kawaida sababu mtu una mastress ya kazi hujali kuhusu mwili tena.

Kwanini jeshi wasiweke wanawake wavae suruali ndefu za kitambaa zinazobana chini?
Kuepuka hii shida? Au kwao sio tatizo?

Nikiangaliaga picha zangu za jeshini na marafiki zangu, wote mapaja nje hakuna anayejali walaa nini!

MALAZI NA MAZINGIRA
Malazi ni mazuri, magodoro yanaridhisha, maji yalikuepo ya kumwaga kambini kwetu ila kambi zingine walilalamiKa hamna maji.

Maji yapo Ila muda wa kuoga hamna, kupiga week nzima bila kuoga ni kawaida na harufu husikiii. Sanasana watoto wa kiume.

Mazingira masafi sababu usafi tunafanya wenyewe tunasimamiwa, vyoo vinaridhisha ksbisa.

TUKUTANE KESHO KWENYE WEEK 6 ZA MATESO, KUMBE TUNAWEZA KUKAA ZAIDI YA WEEK BILA KULALA!

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
Du hapa ndio nimejua kumbe wewe ni wa kike kabla sijagundua hilo nilikuwa nashangaa unaposema mpaka wanaume wanalia
 
Back
Top Bottom