SEHEMU YA 2
Ilipoishia..........
Sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia......
Endelea
Mpaka tumefanikiwa kulifikia geti kuna kuruta waliozimia njiani, wengine kilio kikubwa mimi mmojawapo Aisee wanajeshi waheshimiwe sio kwa mazoezi yale.
Getini tukaambiwa aya kila mtu alale chini mnaingia ndani kwa kubimbilika tranka liache hapohapo, Niliona Afadhali kubimbilika kuliko kuruka kichurachura fasta wazee tukaanza kuingia ndani kwa kubimbilika wengi hapa tuliumia sababu chini kuna vikokoto .
Tumeingia tumekuta kuruta wengi sana tukaungana nao hapo mimi wazo langu ni moja tu KURUDI NYUMBANI.
Tukaanza kupangwa unaitwa jina unaenda upande mwingine zoezi lilienda hadi saa 4 usiku.
Sasa mjeda mmoja akasema tumeita wote nyie majina yenu hayapo vipi? Tulikua wengi kiasi, mimi nilitoa sababu kua nimepangiwa Rukwa lkn kule baridi kali siwezi nina matatizo ya mbavu.
Walituelewa wote tukaruhusiwa.
Sasa majina yakaanzwa kuandikishwa, mimi narudi nyuma mjeda akaniona akanita alikua mmama.
Wewe vipi mbona unarudi nyuma? Nikaanza kulia! Kumbe ndo naharibu akashout "Maafande njooni muone kuruta analia" wote wakaja "Kuruta unalia?" Ebu chuchumaa nikachuchumaa fasta maswali yakaanza unaitwa nani nikataja jina umetokea wapi nikasema, unalia nini nikasema Nataka kurudi nyumbani.... Wewe nilikoma!!! Aya simama twende squat 100 nikaanza kupiga squat huku machozi kama yote basi wanacheka
Sikuzimaliza nikaambiwa ungana na wenzako hapa kuna kuingia hamna kutoka.
MAMBO RASMI
Tukakusanywa uwanja wa damu (uwanja wa damu - uwanja wa mazoezi, paredi) hapo kumbuka hatujapumzika tokea tumefika tukaanza kupewa risala huku tumesimama ole wako usinzie, tupo wengi na wajeda wengi pia ukigeuka huyu hapa
Tukafunguliwa stoo, ipo pembeni ya uwanja tunaingizwa kwa mafungu "ingia toka na godoro ole wako uchelewe kutoka"
Wanajeshi wakali kitu kidogo ushakula tusi tena la mzazi huna cha kumfanya na ole wako unune!
Mimi nilivyoingia chap nimetoka na godoro bahati nzuri yote ni mazuri yamejaa.
Mpaka tunaruhusiwa kwenda Angani (Angani - Hall la kulala) muda umeenda karibia alfajiri.
Nimeingia na marafiki zangu, hapo nimekutana na wale tuliosoma nao advance, sekondari tulikua kama 7 Anna akiwepo.
Tukashauriana tukaoge tulionyeshwa sehemu zote za muhimu mabomba, vyoo.
Sasa tunachota maji akaja mjeda anayejitolea akasema eee kuruta mnaenda kuoga sasa hivi? Sasa sisi tunabaki tunashangaa sababu tulikua kuruta wengi kumbuka hapo ni saa 9 alfajiri
"Bora mkalale dakika chache zilizobaki, muda si mrefu filimbi inalia"
Kudadeq " Anna mimi siwezi hapa kesho namwambia maza anifate" hapo nalia, wengi wanajuta kwenda jeshi muda huo.
Tukapiga moyo konde tukaenda kuoga, tunarudi lisaa hata haijafika tunasikia filimbi wajeda wakike kama wote wamekuja na virungu kutuamsha
Sasa hata hatujalala halafu tunaamshwa hii ni hatari.
Wengine waliolala bila kuoga wanaamka fasta wanachukua miswaki na ndoo eti wakaoge!
Wajeda walitembeza virunguu! "Mnaenda kuoga kwani hamjasikia filimbi, hapa hamna kupiga mswaki wote uwanja wa damu fastaa" kiaina nilishukuru Mungu nimeoga sababu sio kwa vumbi lile plus kugaragara chini.
Tukakusanyika uwanja wa damu saa 10 alfajiri, Kuna wale wanaojitolea wanoko sana! Tukapewa watusimamie uelekeo mchakamchaka basi tukawekwa ki kombania, Mimi nikafight nikawa kombania B pamoja na Anna.
Uelekeo ukaanza jogging tumekimbia huku tunaimba plus wajeda nyuma na gari, hilo gari kumbe ni kwaajili ya kubeba wale watakaozidiwa njiani au kuzimia.
Sasa tunakimbia nikicheki tunapita ile road tuliyokuja nayo jana kutoka mjini. Nikafikiria kwahiyo tunaenda hadi mjini au? Basi sina jinsi tulikimbia sana wengine wanazimia njiani wanapakiwa kwenye gari umbali ulikua kama kutoka Gongo la mboto hadi Airport kwa wanaojua hizo sehemu wataelewa.
Wakati tunarudi huku tunakimbia kushakucha ndo tunaonana vizuri, ilikua vichekesho tumeloa vumbi hadi kope ndani ya pua kote vumbi masikioni usipime ukimuangalia mwenzako unacheka huna mbavu.
Tumerudi kambini tunakutana na majembe, ndoo za michanga. Mimi nilijua tukirudi tunapumzika kumbe kazi inaendelea nilijihisi kukonda kwa siku moja.
Tukapangiwa kazi nikaangukia kwenda shamba, tena huko shamba ni kule tulipotoka kukimbia njia ile ya vumbi ya kutoka mjini katikati barabara pembeni kulia kushoto mashamba ya wajeda sina jinsi.
Tukapiga mguu huku nalia mbaya zaidi sikua na rafiki yangu niliyepangiwa nae kusema tungefarijiana, msidhani mimi mzembe wakuu hapana! Tuliolia tulikua wengi hadi wanaume, tena sikia hivihivi kwa ninavyohadithia kuliko ikutokee.
Njiani kuna mjeda akaniona ni wale wanaojitokea ni binti mzuri mweupe sijui alifata nini kule Wallah!
Akaniambia usilie utazoea mwaya, unaitwa nani nikamwambia Ephen, kumbe ni namesake wangu bhana akafurahi akaanza kunitambulisha kwa wale wajeda wengine huyu ni mdogo wangu. Kumbuka hawa wajeda tuliopewa twende nao shamba ni wale wanaojitolea sio waajiriwa.
Basi ikawa nafuu kwangu, "sasa huku tunaenda ni shamba kung'oa visiki, ningekujua mapema ningekupeleka kule shamba la kuvuna machungwa kule bata, ila usijali kesho utaenda huko" akaniambia
Tulifika shamba kama saa 2 hivi kazi ikaanza kung'oa visiki hawajali mwanaume wala mwanamke wote kazi kazi!
Kisiki kimoja watu watatu tena vile visiki vinene, nilipiga panga na jembe hadi marengerenge yananitoka nayaona
Nilisikitika sana nikajuta kwenda jeshi, nikakumbuka nyumbani nilijihisi nipo dunia ya peke yangu watu wote wameniacha.
Itaendelea...
Muendelezo soma
Niliyoyashuhudia Jeshini