Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

Hahaha nalipenda ila zile 6 week ziishe kwanza, napenda maisha yale tu unakuwa hauna stress zingine unajua utaenda mabio, mpango kazi, usiku doso, chenja hapo sasa mavibe kama yote. Ila sirudi sio kwa madoso yale mwanzoni mpk kuna mda unashindwa kukaa
MtU anakaa wiki 6 bila kuoga sanasana Ngorongoro
 
Wiki mwanamke hajaoga huko chini kuna hali gani? Ukiingia siku zako inakuwaje?
SEHEMU YA 7
Nashangaa muda unaenda mbona haturuhusiwi kwenda kulala?
Yule bakabaka akastopisha kwata akasema hivi sasa ni saa 2 usiku muda bado kabisaa!
Kuruta tunaulizana muda bado kivipi akati tumetumia muda mwingi kombania.
kuruta wakisinzia wanapewa kazi ya kushindana kukimbia
Mimi sikua nasinzia nilikua najipa moyo muda simrefu tunaenda kulala ila wapiiiii.... kila muda bakabaka anasema ndo kwanza saa 2 kamili usiku.

Tunaimba chenja, mazoezi ya viungo kwenye mazoezi nilikua napenda viroba (squats) hata 100 nashuka tu nasihisi kuchoka. then bakabaka anasema hapohapo ulipo jilaze ulale! Basi watu fasta tunajilaza kwenye vumbi
Dakika 5 nyingi anasema inuka rukaruka kichura
Kuruta tulipata hasira hadi wengine wakaanza kusonya.

Hapa nilishangaa kitu! Kuruta anamsonya bakabaka halafu hafanywi kitu zaidi tu anasmile halafu anasema "kuruta fungua moyo huo"
Ila walikua wanaudhi fikiria mtu anakuambia lala ghafla ruka kichura anarudia mara nyingi zile hasira plus usingizi watoto wengine hawana adabu wanamsonya na yeye anablush tu.

Hamuwezi amini alfajiri ilifika tukishuhudia kwa macho! Sasa tunaulizana "mbona leo hatujaenda kulala?" Tutafanya nini ndo ishapita hiyoo

Tukapanga foleni mabio yakaanza, kama nilivyosema muda wa mabio niliupenda sana zile chenja ndo ugonjwa wangu nikawa nakimbia bila kutegea nafurahia kukimbia.

Tumerudi jogging uelekeo shambani, tukitoka shambani chai kuipata hadi ukimbie 2km, tukitoka chai uelekeo kwata
Sikupenda kwata nilikua nanga nimekula mabao mengi tu mpaka bakabaka akanichoka! Akaniambia labda utaweza vitu vingine kama ngoma coy, karate au kazi mchanganyiko.

Ratiba iliendelea mpaka wiki ikakata hatukurudi angani hatukulala wiki nzima!

Baada ya wiki sasa bila kulala! vituko vilianza mtu anachuma machungwa huku kafumba macho anaota kabisa
Mimi ile mabio nikawa nakimbia huku nasinzia, chenja naitikia miguu inaenda mbele lakini nimelala ila naota nakimbia.
Unaweza usiamini lakini hali ndio hiyo.

Bakabaka wakawa wanasema hawa itabidi leo wakalale wasije kutufia bure hapa!
Kitengo cha kuvuna machungwa tulikua tunapiga story sana na bakabaka.
Wiki ilipita bila kuoga.


Usiku ukafika mimi najua kabisa leo tunaenda kulala, nikawa na furaha , sasa muda unaenda ila haturuhusiwi, njaa ikawa inaniuma nikasema subiri nitoroke niende kunywa chai jikoni halafu nirudi fasta kombania nilihisi tulidanganywa leo tena tunakesha.

Lahaula nilijuta kwanini nilitoroka........

Itaendelea.

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
 
Very interesting story, kwa sisi ambao hatukuwahi kwenda inafurahisha kusoma.

Kuna jamaa alileta yake, eti siku hiyo akajikuta na mdada kwenye shimo au nini, wakapata nafasi ya kupunguziana, najiuliza hali hiyo mwili si umekufa ganzi kabisa.!
After six weeks unaweza kujarbu
Mimi kuna service girl alikua ananpiga sana mchinjo kwa mzabuni
Siku moja ziwani akanipa BABY KURUTI nijipimie
HASIRA ZA GADI NO 1
HASIRA ZA KUJILA KISA SERENGETI
nkazimwaga palee
 
Wiki mwanamke hajaoga huko chini kuna hali gani? Ukiingia siku zako inakuwaje?
Kama mtu ana asili ya usafi atafanya juu chini akaoge, unaomba hata kwenda chooni then unaoga chap ila usichelewe
 
After six weeks unaweza kujarbu
Mimi kuna service girl alikua ananpiga sana mchinjo kwa mzabuni
Siku moja ziwani akanipa BABY KURUTI nijipimie
HASIRA ZA GADI NO 1
HASIRA ZA KUJILA KISA SERENGETI
nkazimwaga palee
Kweli ugwadu hauchagui mazingira
 
Kama mtu ana asili ya usafi atafanya juu chini akaoge, unaomba hata kwenda chooni then unaoga chap ila usichelewe
Nataka kujua zike siku mwanamke anazoingia kwenye siku zake, yale maumivu ya tumbo, mgongo kuuma wengine wanaharisha ,wengine wanatapika, hizo siku za periodi unaruhusiwa kulala? Inakuwaje? Pad mnakuwa nazo? Unaweza kwenda kubadilisha atleast kila baada ya masaa mawili?
 
Nataka kujua zike siku mwanamke anazoingia kwenye siku zake, yale maumivu ya tumbo, mgongo kuuma wengine wanaharisha ,wengine wanatapika, hizo siku za periodi unaruhusiwa kulala? Inakuwaje? Pad mnakuwa nazo? Unaweza kwenda kubadilisha atleast kila baada ya masaa mawili?
Kwa upande wangu huwa sipati maumivu hivyo kwenye kazi nilikua naenda nafanya kama kawaida,
Kama nilivyoelezea nilikutana na service girl mwenye jina kama langu tukapendana akawa ananisaidia hivyo nilikua namwambia, yeye alinisaidia nipangwe kazi za around kambi muda ukifika naenda kubadili chap.

Kwa wengine sijui walikua wanafanyaje sikuwahi kuona watu angani zaidi ya wawili wanaolinda, anga zilikua 4 hivyo kuruta 8 wanabaki kulinda, nahisi serengeti waliokua kwenye mwezi wao walikua wanaomba wabaki walinde anga.

Naamini kuna wengine walikua wanaomba ruhusa kwa bakabaka wa kike waende kubadilisha naamini walikua wanaruhusiwa japo sikuwahi kufatilia hilo

Kuhusu kuumwa halafu ulale angani hairuhusiwi, walikua wanasema beba jembe utaenda kulala shambani lakini ukifika huko shambani kazi ni mtindo mmoja

Kwa ufupi wanajeshi hawana roho mbaya kihiivyo kusema uombe ruhusa kwa sababu kama hiyo halafu akukazie
 
Back
Top Bottom