Niliyoyashuhudia katika Kambi ya Simba SC kisiwani Unguja

Niliyoyashuhudia katika Kambi ya Simba SC kisiwani Unguja

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
attachment.php


Yule mnyama mkali mwituni, asiye na masihara anapokutana na kitoweo mbele yake, Simba SC anazidi kunoga kisiwa cha Unguja.

Simba SC iliingia Unguja siku ya tarehe 20 mwezi huu, na mpaka leo wametimiza siku 8. Yafuatayo ndiyo niliyoyaona katika kambi ya mabingwa watarajiwa wa VPL msimu wa 2015/2016.. Simba SC.

1. Muda wa Mazoezi


Simba SC imekua ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, ambapo hutumia si chini ya masaa 5. Mda mwingi hufanyika katika Kiwanja cha Amaan, na Mara chache huingia kujichimbia katika fukwe zilizopo kisiwani humo.

2. Nini Kinafanyika Unguja?


Simba SC ilitumia week 2, mjini Lushoto kwa ajili ya mazoezi ya utimamu wa mwili, ambayo yaliongozwa na Kocha mtalaamu kabisa wa viungo toka nchini Serbia, Momoclovic. Mazoezi hayo yalikua ni mithili ya kikosi maalumu SWAT cha nchini China. Kisiwani Unguja, kocha mwenye Grade A ya leseni ya ukocha toka UEFA, Mtalamu Kerr anawafundisha vijana mbinu za uwanjani.

3. Mfumo tutakaoutumia Msimu ujao.


Lile soka la pasi fupi fupi zenye kasi ya ajabu huku zikiwa na macho (kwa mashabiki wa Arsenal na Barcelona nadhani mnanielewa) kwa mara ya kwanza limetua Tanzania.. Defence imetengeneza ukuta usiopitika, na kwa ukuta huo hata Hans Pope tunaweza tukampanga golini na akaondoka na clean sheet maana mipira haifiki golini kabisa.. Kuhusu ushambuliaji inabidi Ndugu Jamal Malinzi aongeze mipira mingi sana uwanjani maana kuna uwezekano mkubwa Mavugo, Kiiza na "mzee wa mahatrick" Ajibu wakawa wanaondoka na mipira yao katika kila mechi.

4. Muitikio wa Mashabiki.

Mashabiki wa mpira wamekua wakijazana sana uwanjani kushuhudia vijana wa Msimbazi wakijifua. Huwezi amini nimekutana na Bibi wa miaka 90, ambaye alifunga safari toka sehemu inaitwa Madungu, iliyopo Chake Chake kisiwani Pemba, kuja kuwashuhudia vijana.. Ama kweli Simba SC ni ya watu wote.

5. Simba SC vs Kombaini ya Zanzibar.

Jana kulikua na mechi kati ya Simba SC na Kombaini ya Zanzibar (wachezaji bora kabisa a.k.a fahari ya visiwa vya Unguja na Pemba).. ambapo Simba SC ilishinda 2-1. Hamis Kiiza Aguero na Fundi Mgosi ndo walitupia kambani. Kwa soka lililooneshwa jana na Simba SC nadhani ni muda muafaka wa Ndugu Jamal Malinzi kuandaa Kombaini ya Tanzania Bara icheze na Simba SC, mechi hata 3, then mwenye point nyingi atakua Bingwa (naimani Simba SC itashinda zote) wa Vodacom Premier League.

6. Benchi La Ufundi.


Benchi la ufundi limekua likifanya kazi 24/7 kuhakikisha vijana wanaiva ipasavyo. Mtalamu Kerr amekua akiwapa maelezo kwa vitendo vijana wa Simba SC, huku akienda nao sambamba.. Specialist wa Viungo, Momoclovic nae amekua akionesha ni kwa jinsi gani nchini Serbia anaheshimika sana.. Kocha wa Makipa, amekua kivutio kikubwa visiwani humu, kwani amekuja na vifaa ambavyo kwa mara ya kwanza barani Africa vimetua Msimbazi.. Ama kweli Benchi la ufundi limejipanga.

"Na Simba Day Ifike Mapema"

Nikiripoti toka Kisiwani Unguja, ni Mimi Sembo wa SimbaTV.
 

Attachments

  • 1438063130187.jpg
    1438063130187.jpg
    34.8 KB · Views: 1,132
mmh naona kama unatoa haja kubwa tu.
haya bhana Bingwa wa kujitarajisha 2015/2016.
 
Kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya yanga hiyo
 
Kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya yanga hiyo

Mkuu niliyoshudia Unguja, sikuamini macho yangu.. 08/08/2015 karibu Taifa Stadium, uthibitishe nilichoandika.
 
mkuu niliyoshudia unguja, sikuamini macho yangu.. 08/08/2015 karibu taifa stadium, uthibitishe nilichoandika.

mkuu sembo , kwa heshima na taadhima, naomba majina ya vijana wetu waliocheza jana
 
Mkuu niliyoshudia Unguja, sikuamini macho yangu.. 08/08/2015 karibu Taifa Stadium, uthibitishe nilichoandika.

Mkuu mbona unajihakikishia hivyo,ni kwa hayo mazoezi ya jim na kukimbia beach ,au kwa kushinda hako kamchezo kamoja zanzibar?!
 
Always yanga is....
 

Attachments

  • 1438074929067.jpg
    1438074929067.jpg
    23.9 KB · Views: 328
Eti ajibu ni mvivu?

Mkuu hizo ni story za kwenye Magazeti.. Dylan Kerr hana mzaha kabisa na mazoezi, kama Ajibu angezingua mazoezini angekua kashawekwa pembeni. Kuonesha ni kwa jinsi gani ana mrate highly, juzi kati kipindi anataja combination zake za washambuliaji.. Ajibu kaingia katika combination 2, Moja ni yeye na kiiza, nyingine yuko na maguli.. Pia alimsifia kua ni kijana mwenye kipaji cha ajabu sana.
 
mkuu sembo , kwa heshima na taadhima, naomba majina ya vijana wetu waliocheza jana

Mkuu jana Mtalamu Kerr aliwatumia vijana wote, I mean timu iliyocheza 1st half na 2nd half ni tofauti.
 
Mkuu Sembo, mpira siku zote kupata balance ya defence na forward ni kazi kubwa sana. Option inakuwa ama defence iwe nzuri lakini wafanye counter attacks (Chelsea) au Forward na midfielders wawe wazuri iwe ni timu ya kushambulia zaidi (Barcelona). Kocha wenu itabidi aamue wapi ataweka kipaumbele.

Mfano mzuri ni Real Madrid ya sasa. Sioni Rafa benitez akimaliza mwaka kama ataweka kipaumbele kwenye defence kama ilivyo kawaida yake. Timu haitafungwa lakini pia haitafunga sana.
 
Mkuu hiyo ilikua msimu uliopita.. Msimu huu tunarudi kwenye nafasi yetu.

...lakini Simba.....mbona kauli ya "kurudi kwenye nafasi yetu" kila mwanzoni mwa msimu huwa mnaitoa hivi lakini ligi ikianza mnakuwa doro ghafla na kufukuza makocha?

halafu mbona mmeanza kusajili vijeba sasa (Mgosi, Kazimoto) kinyume cha mnachoita sera yenu???
 
Mkuu Sembo, mpira siku zote kupata balance ya defence na forward ni kazi kubwa sana. Option inakuwa ama defence iwe nzuri lakini wafanye counter attacks (Chelsea) au Forward na midfielders wawe wazuri iwe ni timu ya kushambulia zaidi (Barcelona). Kocha wenu itabidi aamue wapi ataweka kipaumbele.

Mfano mzuri ni Real Madrid ya sasa. Sioni Rafa benitez akimaliza mwaka kama ataweka kipaumbele kwenye defence kama ilivyo kawaida yake. Timu haitafungwa lakini pia haitafunga sana.

Mkuu Sibonike, falsala ya Kerr ni kushambulia mwanzo mwisho.. Naheshimu kauli yako.. ila nachoamini mimi ataweza kubalance timu.
 

...lakini Simba.....mbona kauli ya "kurudi kwenye nafasi yetu" kila mwanzoni mwa msimu huwa mnaitoa hivi lakini ligi ikianza mnakuwa doro ghafla na kufukuza makocha?

halafu mbona mmeanza kusajili vijeba sasa (Mgosi, Kazimoto) kinyume cha mnachoita sera yenu???

Mkuu M-mbabe,

1. Kwa sasa Simba SC inamhitaji sana Mgosi kuliko wakati wowote ule kwani,
-mvinyo wa kale ni bora.. na hii kadhihirisha msimu uliopita kwa kuzitungua timu zote za Dar.
- Ni kiongozi bora ndani na nje ya uwanja.. na hii ni kutokana na kua na nidhamu ya hali ya juu.. na sasa ndo Kaptain wa timu.

2. Ukiangalia katika safu ya kiungo ya timu, kiungo mzoefu ambaye chipukizi wenye vipaji vya ajabu kama Mkude, Ndemla n.k watajifunza toka kwake.. mtu huyo si mwingine bali ni "pass master" Mwinyi Kazimoto.

3. Kwa benchi la ufundi lililopo sasa na usajili wa nguvu uliofanywa.. lazima turudi katika nafasi yetu.. Mkuu mark my words.
 
nilitarajia mtakuja na faraja za aina hii ili angalau muwe nacho cha kuongea.
 
Mikia kwa kujifariji mupo aiseeee.,

Mwisho wa msimu mtaishia nafasi ya 4.
 
Back
Top Bottom