sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Simba SC iliingia Unguja siku ya tarehe 20 mwezi huu, na mpaka leo wametimiza siku 8. Yafuatayo ndiyo niliyoyaona katika kambi ya mabingwa watarajiwa wa VPL msimu wa 2015/2016.. Simba SC.
1. Muda wa Mazoezi
Simba SC imekua ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, ambapo hutumia si chini ya masaa 5. Mda mwingi hufanyika katika Kiwanja cha Amaan, na Mara chache huingia kujichimbia katika fukwe zilizopo kisiwani humo.
2. Nini Kinafanyika Unguja?
Simba SC ilitumia week 2, mjini Lushoto kwa ajili ya mazoezi ya utimamu wa mwili, ambayo yaliongozwa na Kocha mtalaamu kabisa wa viungo toka nchini Serbia, Momoclovic. Mazoezi hayo yalikua ni mithili ya kikosi maalumu SWAT cha nchini China. Kisiwani Unguja, kocha mwenye Grade A ya leseni ya ukocha toka UEFA, Mtalamu Kerr anawafundisha vijana mbinu za uwanjani.
3. Mfumo tutakaoutumia Msimu ujao.
Lile soka la pasi fupi fupi zenye kasi ya ajabu huku zikiwa na macho (kwa mashabiki wa Arsenal na Barcelona nadhani mnanielewa) kwa mara ya kwanza limetua Tanzania.. Defence imetengeneza ukuta usiopitika, na kwa ukuta huo hata Hans Pope tunaweza tukampanga golini na akaondoka na clean sheet maana mipira haifiki golini kabisa.. Kuhusu ushambuliaji inabidi Ndugu Jamal Malinzi aongeze mipira mingi sana uwanjani maana kuna uwezekano mkubwa Mavugo, Kiiza na "mzee wa mahatrick" Ajibu wakawa wanaondoka na mipira yao katika kila mechi.
4. Muitikio wa Mashabiki.
Mashabiki wa mpira wamekua wakijazana sana uwanjani kushuhudia vijana wa Msimbazi wakijifua. Huwezi amini nimekutana na Bibi wa miaka 90, ambaye alifunga safari toka sehemu inaitwa Madungu, iliyopo Chake Chake kisiwani Pemba, kuja kuwashuhudia vijana.. Ama kweli Simba SC ni ya watu wote.
5. Simba SC vs Kombaini ya Zanzibar.
Jana kulikua na mechi kati ya Simba SC na Kombaini ya Zanzibar (wachezaji bora kabisa a.k.a fahari ya visiwa vya Unguja na Pemba).. ambapo Simba SC ilishinda 2-1. Hamis Kiiza Aguero na Fundi Mgosi ndo walitupia kambani. Kwa soka lililooneshwa jana na Simba SC nadhani ni muda muafaka wa Ndugu Jamal Malinzi kuandaa Kombaini ya Tanzania Bara icheze na Simba SC, mechi hata 3, then mwenye point nyingi atakua Bingwa (naimani Simba SC itashinda zote) wa Vodacom Premier League.
6. Benchi La Ufundi.
Benchi la ufundi limekua likifanya kazi 24/7 kuhakikisha vijana wanaiva ipasavyo. Mtalamu Kerr amekua akiwapa maelezo kwa vitendo vijana wa Simba SC, huku akienda nao sambamba.. Specialist wa Viungo, Momoclovic nae amekua akionesha ni kwa jinsi gani nchini Serbia anaheshimika sana.. Kocha wa Makipa, amekua kivutio kikubwa visiwani humu, kwani amekuja na vifaa ambavyo kwa mara ya kwanza barani Africa vimetua Msimbazi.. Ama kweli Benchi la ufundi limejipanga.
"Na Simba Day Ifike Mapema"
Nikiripoti toka Kisiwani Unguja, ni Mimi Sembo wa SimbaTV.