Niliyoyashuhudia kutokana na mwingiliano wa Kenya na Tanzania mkoani Mara wilaya ya Tarime

Niliyoyashuhudia kutokana na mwingiliano wa Kenya na Tanzania mkoani Mara wilaya ya Tarime

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,304
Habari wanaJamii Forums.

Leo katika nimekumbuka visa kadhaa na matukio ambayo niliwahi kuyashuhudia miaka kadhaa iliyopita huko mkoani Mara wilaya ya Tarime.

Terminator nimezaliwa miaka 37 iliyopita huko mkoani mara Wilaya ya Tarime kabila ni Mkurya.. Wa Tarime katika kijiji cha Kubiterere.. Kwa wenyeji wa mkoa wa mara ndio watakuwa wanakitambua hiki kijiji ila kwa wasio wenyeji huwa tunatumia kijiji cha sirari kutokana kwamba ndio sehem maarufu ambayo ukitaja ukiwa katika mikoa ya watu inakuwa rahisi kueleweka.
Ila ukweli sisi wazawa ndio tunaojua tofauti hizo.

Kwa uchache tu mkoa wa mara unakaliwa na Makabila mengi sana ila kabila maarufu ni wakurya..
Ila ndani ya hilo kabila linalotambulika kama wakurya ndani yake kuna koo au jamii za watu tofauti wanaotofautiana utamaduni.. Tabia na hata historia na jiografia.
Nitaorodhesha hapa baadhi ya jamii za wakurya au koo za wakurya ambazo zinakaa mkoa wa Mara japo siwezi kuziorodhesha zote kutokana kwamba ni nyingi zaidi ya 50.
1. BARENCHOKA.
2.BAKIRA.
3.BAANCHARI.
4.BASWETA
5.BAMERA.
6.BAHUNYAGA
7.BATIMBARU.
8.BAKENYE
9.BAIKOMA
10. BASIMBETE ...ETC

Koo hizo zote kwa ujumla ni Wakurya na wote wanazungumza kikurya japo kuna baadhi ya maneno hawasikilizani kutokana na tofauti za ki'lahaja,

Na hizo koo huwa hazichangamani kila watu huwa wanajiografia yao.. hapa naaanisha koo hizi hawachangamani ila kila koo inakiwa na sehem yake mara nyingi koo hizi zinatenganishwa na mito, milima na mabonde...
Na kila koo inapokaa huwa imejitegemea kiutamaduni na kila kitu yaani mifumo yao ya ulinzi na kila kitu imejitegemea na koo nyingine.

Na hapa mkiskia wakurya wanapigana ugomvi wa koo kwa koo mara nyingi ni pale ambapo koo moja ikijaribu kuingilia mipaka ya koo nyingine au kujaribu, Kuiba au kuchukua kitu, mali kutoka koo nyingine pasipo ridhaa ya wahusika. Hapo ndio kelele zinapigwa na wahusika kisha vijana wa koo zote zilizokosa maelewano kukutana mipakani na kuanza kugombana kwa kutumia siraha za jadi na wanaoelemewa mali zao huchukuliwa na hata kuharibiwa.

Na fikiri hapa nitakuwa nimewafumbua macho wale wasiojua kwanini Wakurya wanakatana mapanga au wanauwana ila sababu kuu ni kwamba koo hizo zinavyojaribu kutanua teritories zao ndio matokeo ya vita huanza

Koo za Warenchoka na Wakira ndio koo pekee ambazo ziko mpakani mwa Kenya na Tanzania.. na koo hizi zina watu pande zote hapa namaanisha kenya na Tanzania..

Mwaka 2007 nilishuhudia vita kati ya Warenchoka na Wanchari.. Kitu ambacho kimesababisha kuandika huu uzi nilishuhudia muingiliano wa koo hizi ukisababisha makosa makubwa ya uvunjifu wa Aman na makosa ya ki Intelijensia kati ya Kenya na Tanzania.
Kwa maana Raia wa Kenya ambao ni wakurya wa koo ya Barenchoka ndio walikuwa wapiganaji wakuu katika koo hiyo.

Vijana wa na Raia wa Kenya walikuwa wakivuka mipaka na siraha zao za Jadi kuja kushambulia na Kuuwa Raia wa Tanzania nchini kwao kwa sababu ya ukabila...

Na suala hili halikuwahi kuongelewa popote wala kuonekana kama ni jambo la kushangaza na kupingwa na kila Mtanzania ambae analipenda taifa lake.

Na hadi sasa Maisha ya kule Wakenya kuja kujiandikisha Tanzania kwa ajili ya kupiga kura kwao sio kitu cha ajabu wala hawachukulii kama ni kosa.

Pia watanzania kwenda kujiandikisha kenya na kushiriki kupiga kura Kenya hawaoni kama ni Tatzo wala kosa.

Nakumbuka mwaka X mbuge X wa Kenya jimbo la Kurya West aliwahi kununua mifuko ya cement katika shule X ya Tanzania kama moja ya Rushwa za kikampeni akihimiza watu wavuke mpaka na kwenda kumpigia kura Kenya na ilikuwa hivyo hadi akashinda kwa kura za watanzania..

Je kuna namna serikali ya Tanzania wanatambua huu mwingiliano wa haya Mataifa?
 
Hapo kunashda gan? wache wale fursa adimu hyo.au una mpango unagombea jimbo
 
Nakurekebisha kwa baadhi ya maeneo.
Wakiira
Nyabasi
Wairege
Warenchoka.
Hizo ndizo koo zilizogawanywa na mpaka I mean mpaka umewakata kwa Tanzania na Kenya na Wana mwingiliano WA moja kwa moja katika kila shughuli za kijamii,kisiasa na kiusalama.

Miaka ya nyuma....wabunge wa kuria east(shadrack manga) na kuria west( Dr gisuka machage) wote walitoka tarime na ni watanzania kwa asilimia Mia.
Ushirika wetu upo kwenye mambo yafuatayo
1. Ndoa
2. Wizi wa ng'ombe
3. Kuibua na kupambana na migogoro.
4. Kuchagua viongozi
NB
Mbunge wa kuria west kwa sasa hon Mathias robi ana ndugu wengi na machawa wengi tz kuliko huko Kenya na no wonder huwa anashinda uchaguzi kwa kura za watanzania
 
Sirari (Tanzania) na Isbania (Kenya) pia mwingiliano ni mkubwa sana.
 
Wenye nchi wenyewe wanasemaje? Anyway naendelea kupata maoni ya wapita njia kwanza!
 
Nakurekebisha kwa baadhi ya maeneo.
Wakiira
Nyabasi
Wairege
Warenchoka.
Hizo ndizo koo zilizogawanywa na mpaka I mean mpaka umewakata kwa Tanzania na Kenya na Wana mwingiliano WA moja kwa moja katika kila shughuli za kijamii,kisiasa na kiusalama.

Miaka ya nyuma....wabunge wa kuria east(shadrack manga) na kuria west( Dr gisuka machage) wote walitoka tarime na ni watanzania kwa asilimia Mia.
Ushirika wetu upo kwenye mambo yafuatayo
1. Ndoa
2. Wizi wa ng'ombe
3. Kuibua na kupambana na migogoro.
4. Kuchagua viongozi
NB
Mbunge wa kuria west kwa sasa hon Mathias robi ana ndugu wengi na machawa wengi tz kuliko huko Kenya na no wonder huwa anashinda uchaguzi kwa kura za watanzania
Uko sahihi ila hatuna neno "wakira wala warenchoka " kwa usahihi ni bhakira na bharechoka. (ba) hiyo "Wa" inatokana na matokeo ya direct translation ya kurya to swahili ila umeeleza vyema sana
 
kuna tukio moja nalikumbuka kuhusu wakurya lilitokea miaka ya 2000+ japo.nilikuwa si mkubwa sana ila nakumbuka.kuna nyumba walikuwa wanakaa wakurya wawili mtu na ndugu yake.sasa siku moja waligombana.basi walifunga milango kwa ndani na kuanza kupigana na kukatana mapanga kavu kavu.mpaka wakafa.mpaka leo uwa najiuliza wale jamaa waliwaza nini.
 
kuna tukio moja nalikumbuka kuhusu wakurya lilitokea miaka ya 2000+ japo.nilikuwa si mkubwa sana ila nakumbuka.kuna nyumba walikuwa wanakaa wakurya wawili mtu na ndugu yake.sasa siku moja waligombana.basi walifunga milango kwa ndani na kuanza kupigana na kukatana mapanga kavu kavu.mpaka wakafa.mpaka leo uwa najiuliza wale jamaa waliwaza nini.
wanafaa kuwa jeshini wana morari ya vita
 
Nisalimieni kina manka tarimo na shayo hapo isbania,

Nataka nikija Mara nifike mok border niende maragoli
 
Back
Top Bottom