Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Kwanza niseme hakuna ulichokosea katika maandishi yako kwakuwa umetoa mtazamo wako juu ya swala hili,na hata kama ningekosea bado ungekuwa sahihi kunisahihisha hakuna mkamilifu isipokuwa Allah

Kuna aya naitafuta kwa kauli yake Allah anasema kuhusiana na wasaidizi malaika ambao waadilifu,bado naitafuta sikumbuki nimesoma katika sura ipi

Lkn kama ulivyosema huenda ikawa lugha gongana vile vile mathalani unapozungumzia kazi za malaika waandishi,je wanafanya kazi ya nani,vp kuhusu malaika watoa roho,na hao walinzi wa motoni na chungu ya malaika na kazo zao mbali mbali

Lakini tunaposema wasaidizi wa Allah haimaniishi bila hao mambo hayaendi,kwani Allah akitaka jambo huliambia kuwa nalo huwa,kwahiyo tunaposema Allah anawasaidizi hii haiondoi utukufu wa Allah hata kidogo

Anway bado naitafuta ile aya nikiipata inshallah ntaileta
 
Kumbe ninapoteza muda na mtu aliyeishia kidato cha nne.

Ndio maana basi..
 
Kumbe ninapoteza muda na mtu aliyeishia kidato cha nne.

Ndio maana basi..
Kuishia Form IV haimaanishi kwamba hana kitu ambacho labda mwenye Degree hawezi jifunza kutoka kwake.
 
Ok. Nakumbuka Arsis kuna siku alisema neno kuhusu safari mtume kwenda mbinguni....... (Nimejaribu kutafuta huko nyuma nimekosa sabb uzi kwasasa ni mkubwa Sana!!

Nikumbusheni hii kitu aliizungumziaje, ile safari ni really!?
Au imekaaje.... Kuna kitu chanitatiza hapa
FaizaFoxy
Arsis
 
Kuna aya naitafuta kwa kauli yake Allah anasema kuhusiana na wasaidizi malaika ambao waadilifu,bado naitafuta sikumbuki nimesoma katika sura ipi
Nitafurahi kama utaipata,

Lkn kama ulivyosema huenda ikawa lugha gongana vile vile mathalani unapozungumzia kazi za malaika waandishi,je wanafanya kazi ya nani,vp kuhusu malaika watoa roho,na hao walinzi wa motoni na chungu ya malaika na kazo zao mbali mbali
Teh yes, ila hapa haitakua lugha bali maana mgongano 🀣. Kwani mtumwa ni nani na msaidizi ni nani kwa ufaham wako? Kingine kwa hizo kazi walizopewa malaika mie nafaham haziwapi daraja za kua wasaidizi bali wataendelea kua watumwa au niseme watumishi wa Mwenyezi Mungu mtukufu kama hilo neno utumwa linakupa ukakasi ha ha.

Nikuulize swali labda, kwani sisi binadam tulivyopewa ukhalifa hapa duniani. Vipi ndio kigezo cha kua wasaidizi wa Mwenyezi Mungu katika utawala wake? Natumai jibu litakua ni hapana. Kwani sisi viumbe vyote mbele yake ni "Watumwa"... (Servants) na si vinginevyo.

Lakini tunaposema wasaidizi wa Allah haimaniishi bila hao mambo hayaendi,kwani Allah akitaka jambo huliambia kuwa nalo huwa,kwahiyo tunaposema Allah anawasaidizi hii haiondoi utukufu wa Allah hata kidogo
Mmmh sidhani kama upo sahihi na utakua unaipinga Ayah kwenye Quran. Navyofaham mie sie kwake ni watumwa "Servants" sio wasaidizi "Helpers". Viumbe wote wa Allah mtukufu sie mbele yake ni watumwa. Ikikupendeza kaisome Al-Isra 17:111 hapa chini. Sasa kama unayo wewe unayoijua inasema kua Malaika ni wasaidizi ni sawa na kutaka kuniambia kua Quran inajipinga, huku inasema hivi kule inasema vile.

 
Nimesoma maelezo yako,ngoja niitafute ile aya,nikiipata ntaileta inshallah
 
Habari Simba. Nadhani hilo eneo lenye vyakula vingi mlolitembelea mlipoenda Chakechake Pemba panaitwa Machomane (sio Machomanne), nilikulaga chipsi tamu hapo sijapata kula huku kwetu Bara.

Kama sijakosea hilo ndo eneo lenye pirika nyingi Pemba mpaka usiku mkubwa. Watu wengi toka Bara hukaa hapo Machomane kwa sababu ya uwepo wa kambi ya jeshi maeneo hayo (Kama tunavyojua Jeshi ni la Muungano). Nashkuru sana Simba kwa kurudisha memory zangu nyingi kupitia uzi huu.
Umenikumbusha pia Barafaa, miaka mingi nyuma huyo alikuwa maarufu sana kwa kuku watamu, nilisoma hapo Shule ya Amana (Habib Punja), nikakaa sana Ilala kwa muda, Mtaa Dodoma, Mtaa Arusha, Mtaa Tanga.

Umenikumbusha pia familia ya kina Kibao coz ni jamaa wa karibu, kuna mengi walinihadithia wenyewe miaka ya nyuma kwa sasa ndo naanza kuelewa kupitia uzi huu. Thanx a lot for the memory.

Salamu kwa Arsis
 
Umeeleza vizuri sana na ukipata muda dondosha nondo usisahau kuni tag ili nione(ombi), kati ya watu nawakubali ni wale wenye fikra huru wanaoongozwa na kiasi katika kila jambo, inaonesha ni mmoja wao.

Mimi kitabu nilichokisoma nikakielewa vizuri ni Biblia, haimaanishi vitabu vingine sijavielewa au lah! Ila ni neema tu ambayo naweza sema nimekutana nayo. Huwa siisomi kwa mazoea najitahidi kuisoma kwa kutafakari na kuihoji hadi nipate majibu. Mimi sio mtu wa dini, habari nilizosisoma kupitia biblia za maisha ya Yesu Kristo namna aliishi duniani na kupitia mafundisho yake ndio umekuwa muongozo wangu.

Nakubaliana na wewe kuwa neno linapotafsiriwa kwenda lugha nyingine kuna uwezekano wa kupoteza maana hiyo ni kweli kabisaaa, ila tukumbuke kuwa hizi lugha zote ni za wanadamu, lugha ya Mungu ni mitetemo na inatembea katika wave, hivyo kuelewa mambo magumu ya imani na yaliyofichwa inakulazimu uwe connected na frequency sawa na hiyo wave, kwa neema yake unaweza kupata mwanga wa nini kinamaanisha.

Niliposema Mungu hatujui katika label ya dini, sikumaanisha kwamba hana ufahamu kuhusu dini zetu HAPANA, Mungu ni mjuzi wa yote hata tunayoyawaza anayafahamu, nilichomaanisha ni kuwa hazingatii haya matabaka tuliyojiwekea, yeye anatuchukulia sote kama kitu kimoja na atakuhesabia haki kulingana na matendo yetu.

Kwa uelewa wako ningependa kujua lugha ya Mungu ni ipi?

Paragraph ya mwisho kuna kitu unataka kusema ila unaficha ficha funguka mkuu.
 
Sikuhz humu ni mabishano tu,,,,, elim imeanza kuadimika kweny huu uzi watu ni kubishania vitabu ambayo hata hawajui kilichoandikwa humo kina uharisia kiasi gani🚢🚢


Anyway bado nipo kwenye swali langu hapo juu.....
Labda niweke kidogo sababu za kuuliza maana napuuzwa wakati swali lina mada nzito nyuma yake (naweka kwa uchache ili nijibiwe niunganishe doti)

Majuzi jumapili kuamkia jumatatu mbingu zilikuwa wazi..... Kwanzia usiku mpaka mida kama ya saa 5 hivi (wakati wa swala ya dhuha)

Kuna somo lilipitika kuhusu mtume, kwenye hiyo safari ya kwenda mbinguni.... (Alikaa huko kwa muda wa lisaa na dk 50 pekee akifundishwa siri za mbinguni)
Kuhusu ni siri gani hapo sijui.... Na kuhusu nimeyajuaje yote hayo

(Ni maono.... Tuishie hapa 🀝
Nilitaka kujua Arsis alizungumza vipi kuhusu safari ya mtume
 
Nimeona nikate baadhi a maandiko nipate kujibu kila moja kivyake, ili majibu yasiwe marefu sana.

Hilo la kupuuzwa wala usilifikirie kabisa. Waislam tunatakiwa tuwe chanya sio hasi.

Hilo jambo nilikua nalitafuta, ii nijibu kitu cha uhakika. Uzi umekua mrefu. Natumai ulikua unaongelea suala hili; Tafadhali gonga hapa.
 
Umeeleza vizuri sana na ukipata muda dondosha nondo usisahau kuni tag ili nione(ombi), kati ya watu nawakubali ni wale wenye fikra huru wanaoongozwa na kiasi katika kila jambo, inaonesha ni mmoja wao.
Nimefurahi kama the way ninavyo andika ninaeleweka. Shukran kwalo!

Mimi sio mtu wa dini, habari nilizosisoma kupitia biblia za maisha ya Yesu Kristo namna aliishi duniani na kupitia mafundisho yake ndio umekuwa muongozo wangu.
Hili ni jambo jema hakika, kama unayafata vizuri aliyoteremshiwa Iysah A.S kama anavyoitwa upande wetu, kwa mujibu wa Iman yangu nakuona upo katika njia sahihi. Na Quran inathibitisha hilo....



Labda angalizo tu kuhusu hilo, uwe unafata yale ya "Yesu Kristo" yaliyo ya kweli na si yale ambayo kazushiwa nayo. πŸ‘ˆ Hii sentensi ya angalizo langu kwako rafiki uisome mara mbili mbili eeh kuna kitu utanielewa ndani yake.

Zaidi niseme lingine iwe kama faida, na niliseme kwasababu ya hiyo screenshot hapo juu, kwani ndani yake kuna neno "Injili/Gospel". Kwa ufaham nilionao, as usual kila elim ina marejeo.

Kwa ufaham wangu hakuna kitabu kitakatifu kilichoshushwa kwa mitume chenye jina la "Biblia (Bible)" hata ukiamua kulitafuta ndani ya Biblia yenyewe.

Mwana wa Maryam naemjua mimi aliteremshiwa Injili, kama ilivyo Torat kwa Mussa A.S na Quran kwa Muhammad P.B.U.H

Hapa usipokua na jazba, ukawa na fikra huru utanielewa vizuri. Na kunielewa vizuri kwenyewe itapasa kuanza kwa kujua maana ya neno Bible(Biblia) kisha mengine baadae.

Either kwa mujibu wa dini ya Kikristo au kilugha utakuta ina maana ya "A collections of religious texts or scriptures". Ndio maana ndani yake unaipata Agano la kale (Old testament) na Agano jipya (New Testament).

I do hope unaelewa kua Agano la kale imebase kwenye Torah (Torat) na kiasi chake agano jipya ndio imebase kwenye injili. Na ukumbuke wanaoifata Torah hawajiiti wakristo bali wayahudi. Hapo kama una fikra huru utajiuliza, Kama Torah ilishushwa kwa Mussa A.S na Injili imeshuka kwa Yesu/Iysah mwana wa Maryam.

Je mjumuisho wa vyote, I mean kama mapokezi yote yapo ndani ya kitabu kimoja, Je hicho kitabu kinakua ni cha nani kati yao? Wote kwa pamoja au mmoja wapo na kwanini? Jiulize tu, Je Bible ni ya Mussa? kama sio kwanini wakati kuna Torah iliyoshushwa kwake ndani yake? Je Bible ni ya Mwana wa Maryam? Kama ndio kwanini kuna Torah ndani yake ambayo haikushushwa kwake? Je ile Injili iliyoshushwa kwa Mwana wa Maryam yeye kama yeye iko wapi na kwanini iunganishwe na Torah ipewe jina la Bible kwani jina la Injili lina mapungufu gani? Lengo haswa ni nini?

Teh au basi, hilo niliache, kama una fikra huru namna navyokudhania naamini nitakua nimekupa fikra mpya au wazo jipya la kufatilia ambako huenda ukapata kipya chenye manufaa nawe pamoja na wanao kuzunguka kwani elim haina mwisho.

Sehem hii nimekusoma vizuri tu. Kuhusu lugha hizi tulizonazo kwa ufaham wangu mimi ni moja katika Ishara za uwepo wake Mwenyezi Mungu. Marejeo ya ufaham huu nitaunganisha sehem katika Quran kama nilivyosema hapo awali kua hakuna ufaham usio na marejeo.



Sasa ingekua vizuri na we ungenifahamisha marejeo ya ufaham wako kuhusu lugha ya Muumba kua ni mtetemo umeutoa wapi. Kwani as far as I know, hapo naona umetoa definition ya neno "Sound" na sio kuilezea lugha ya Mwenyezi Mungu.

Sijajua hoja yako kuhusu lugha ya Muumba ulitaka kusema nini ila kama ulikua na maana ya elim katika lugha asili basi acha niseme au niongezee kwa kusema hivi, Mfano leo ukaamua kujifunza kuhusu Quran, irejee kwenye lugha yake ya asili ambayo ni kiarabu. Ukitaka lel say kuileta katika kiswahili ni vyema ukawa na mfasiri zaidi ya mmoja kwa ajili ya kufanya ulinganisho wa tafsiri zao kwani kila mmoja wao atakua anatafsiri kulingana na uelewa wake. Vinginevyo unaeza kujikuta huielewi Quran bali uelewa wa yule alie kupa tafsiri kuhusu Qur'an.

Vivyo hivyo katika injili, irejee katika lugha ya asili waliyofundishwa kwao watu wa mwanzo, lugha aliyoongea Mwana wa Maryam kwa watu wake ambayo ni Aramaic, kisha ufanye kama nilivyosema hapo juu. Uwe na mfasiri zaidi ya mmoja ili ufaham wako usijijenge katika uelewa wa mfasiri bali ile halisi ya maarifa kama yalivyo.

Sio ile ooh mie namfata Sheikh flan 🀣, yule Sheikh sio Quran banaa... au mara ooh mie namfata Askof flan. Hapana sio sawa kwani yule pia sio Injili na haitakiwi kwa mtu mwenye utashi wa kujifunza kitu kwa uhuru awe namna hiyo. Tena kibaya zaidi walim wa sasa kwa mambo yahusuyo Iman na Dini wanachokifundisha ni Misimamo yao walio nayo sio ile asili ya vitabu kama ilivyo.

Too bad 😒

Na kuhusu hii sehem naona kama unakosea kiduchu kulingana na ufaham wangu mimi kuhusu Dini, kuhusu Imani. Kwanza nikukumbushe, kila unapotamka neno dini kinachonijia akilini ni mfumo au mwongozo wa Maisha. Mwongozo ya namna gani tuishi na namna gani tuabudu kaiweka yeye kupitia mitume wake ndio maana leo hii una dini ya kikristo kupitia kwa Mwana wa Maryam, Una dini ya Kiislam kupitia kwa Muhammad P.B.U.H, Una uyahudi na Torah kupitia kwa Mussa A.S.

Miongozo ama njia nikiwa na maana ya dini inaeza kua tofauti kulingana na Zama husika, watu husika ila Imani ni moja na inafanana kwani chanzo chake ni Mola mmoja aliye na nguvu na mwenye hekima.

TUnaweza kutofautiana katika uvaaji, chakula gani tule kipi tusile lakini sio Imani juu ya Muumba. Na ukiona kuna utofauti basi ujue moja wapo sio sahihi. Mfano, katika nguzo za Imani ya Kiislam (Kujisalimiha kwa muumba) ni hizi. 1. Kumuamini Mwenyezi Mungu, 2. Kuamini Malaika wake, 3. Kuamini vitabu vyake (eg Torah, Zaburi, Injili, Quran), 4. Kuamini mitume wake (eg Mussa A.S, Dawd A.S, Iysah A.S, Muhammad P.B.U.H), 5. Kuamini siku ya mwisho, 6. Kuamini Qadar zake Mwenyezi Mungu.

NImeamua kuzitaja nikiwa na sababu zangu, Kwanza unielewe kua hizo ni Nguzo za Imani na zipo pia nguzo za dini ya Kiislam. Ambazo zenyewe hasa zinaelezea namna gani tuishi, issue kama salah na zakah na mengineyo.

Nimezitaja hizo nguzo pia ili uone ufanano wa kitu. Ninaamini katika hizo nguzo za Imani, Ya kwanza, Ya pili, ya 5 uko nazo hizo zingine sitaki kukusemea. Ufanano huo ndio nachokimaanisha katika kusema Imani sahihi inayotoka kwa Muumba mmoja haipingani bali inafanana.

Bali katika dini/mwongozo ndio unaeza kupishana zama na zama. Mfano zama hii tulizo nazo upande wetu waislam tumeamrishwa sala 5. Zama zilzopita hawakusali sala 5 kama zetu but walisali. Kuna mengine yanafanana mfano issue ya kufunga. Waliamrishwa kufungaa pia waliokuepo kabla yetu. Ila kwenye Imani sahihi wote tunafanana kwetu sisi na wale walio tangulia. Tunamuamini Mungu Mmoja, Tunaamini Malaika zake, Mitume wake vitabu vyake na siku ya mwisho.

So hapa najaribu kukwambia kua kuna miongozo/dini ambayo katupatia yeye mola wetu mlezi kupitia mitume wake kuanzia zama za Adam A.S hadi zama hizi tulizopo sasa. Pia kuna miongozo/dini tulizo zibumba sisi kulingana na tamaa zetu na upumbafu wetu kwenye kuzihadaa nafs zetu.

So kila aliepokea mwongozo/dini sahihi katika zama zote zilizo tangulia (hapa napo uninukuu vizuri) basi atakua chini ya Rehema zake. Na miongozo sahihi hiyo ni ile itokayo kwake pekee. Hivyo dini sahihi ama lugha mwongozo sahihi sio jambo la kuzua (Matabaka unayosena tumejiwekea) bali dini ambazo si sahihi hizo ndio matokeo ya matamanio ya nafsi zetu wenyewe.

As usual, ufaham huo juu marejeo yake ni hapa.



Nakumbuka kauli kama hii uliisema kule juu, ila hukunambia umeirejea wapi. But binafs Quran ndio kitabu changu na main source ya ufaham wangu juu ya haya nayokuelezea so sioni haya kujiachia nayo kama hivi.

Kukazia zaidi katika mada yetu ya dini ni nini, Imani ni nini. Dini ni muongozo wa kua na Imani iliyo sahihi. Kama mtu anao muongozo mbaya hawezi kua na Imani iliyo sahihi. (Unishike vizuri hapa, sijataja aina za dini bali nimesema dini na imani kwa ujumla wake). Vile vile mtu anaweza kua na muongozo/dini sahihi ila akakosa Imani iliyo sahihi. Upande wangu huku ndio kuna kitu tunasema... Kila Muumini ni Muislam ila sio kila Muislam ni Muumini. Niirudie kauli hiyo kwa kutoa maneno yenye asili ya kiarab itasomeka hivi. "KILA MUUMINI KAJISALIMISHA KWA MOLA WAKE ILA SIO KILA ALIE JISALIMISHA KAAMINI".

Kwa uelewa wako ningependa kujua lugha ya Mungu ni ipi?
Kuhusu hili sina elim hiyo, na sina hakika kama kuna kiumbe mwenye elim hii.

Miongozo yote aliyoteremsha kwa mitume na manabii imeshuka kwa lugha ambazo walikua wanazungumza wao katika zama hizo. So itoshe mimi kusema yeye Muumba anazijua lugha za viunbe vyake vyote sio sisi binadam tu, bali wanyama na viumbe wengine tunao wajua na tusio wajua. Lakini sisi hatuijui lugha yake.

Mwisho rafiki yangu, kiumbe mwenzangu 😊. Niombe tuufunge huu mjadala na upande wangu basi liwe gazeti la mwisho kuandika.

Nahisi post itakua ndefu balaa 🀣🀣🀣 ila yote kheri.
 
Sikua na uoga wala haikunijia kuogopa kabisa.

Sababu ni nyingi, ukiusoma uzi vizuri utakuta mimi ni wa ukoo wa Simba. Hayo ya Usimba ni mambi ya kimizimu, nimkekua nayo tangu mdogo. Ingawa siku hizi sifati mila wala desturi z Kisimba. Lakini wa ukoo wetu wa Kisimba tunachanjiwa mitishamba na mizizi mingi tokea wadogo. mambo ya mizimu na majini hayatupi shida.

Kingine ni kua hilo pango ndio ni michezo yetu humo kuanzia wadogo tukija shamba kwa babu yetu, wala hapakua pageni kwangu.
Simba.
 
Basi acha kuwaongopea watu kwa kujinasibu kitu ambacho hukijui.
Sawa kabisa, vipi nisichokijua kukuuliza wewe ni makosa?

Nimekuuliza nini maana ya "mtanashati" na liemeanzia wapi hilo neno, nikakulizia unaijua elimu ya antropolojia?
Simba.
 
Nimeona mnamwaga elimu, wewe na Battor. Mnatufaidisha sana.

Nawafahamisha tu, mkipitia series ya kisa cha Adam nilioianza lakini ilikua inasuasua kwa kumalizia kisa cha Kojani, naomba muipitie na muifatilie ikianza tena, mtapata elimu tofauti, kwa mtazamo tofauti kabisa ambao mbinu (method) yake ya kuifahamu Qur'an unaelekezwa humo.

natamani sana na mtaalamu mwenye ujuzi mpana, asieweza kujibu maswali mepesi kabisa, anaeitwa Hance Mtanashati nae aufatilie.
Simba.
 
Teh yah, hicho nitakifatilia. Japo kwenye huu uzi bado niko nyuma kiasi... Page Number 149 ila nitakifikia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…