Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Wala hujakosea, natafuta kutoa na kupokea elimu.

Kua na lugha ya ulimi (lisan) nyepesi kidogo, uzi wa kielimu huu.
Simba.
Ndugu yangu, naona ulikurupuka kaanze upya.
Uzi wako nmeufatila mwanzo mwisho siku taka comment chochote mpaka nione hitimisho lako kwa sasa huna jipya.

Umesema Mtume Muhammad(S.A.W) Haja tafsiri Qur-an zaidi ya Aya20 huu ni uwongo wa dhahiri kabisa mtume (s.a.w) ame wafundisha maswahaba zake qur an na kuwa tafsiria ni shie hapo hakuna Arsis ulitaka kuuchafuwa uislam na umeshindwa,
Hii dini Allah ndie anaeilinda.
 
Ndugu, Naona bwana simba ameuliza maana ya Qareen hapo, Japo sio swali langu mimi nitajaribu kujibu kwa ninavyoelewa kama ilivyotajwa katika quran na hadith Arsis atafafanua vizuri natumai.
KILUGHA: Neno "qareen" (قرين) ni masdar ya neno "qarana" (قرن), ambalo lina maana ya "kuunganishwa" au "kushirikishwa."
Hivyo katika lugha ya Kiarabu "qareen" inamaanisha "mwandamizi" au "mshirika."
Mpaka hapa utapata swali je ni mshirika wa nini?
Sasa tuje katika Qur an ukisoma katika surat Zukhruf sura ya 43 aya ya 36 utaona ametajwa qareen inasema:-
وَمَن يَعۡشُ عَن ذِكۡرِ ٱلرَّحۡمَٰنِ نُقَيِّضۡ لَهُۥ شَيۡطَٰنٗا فَهُوَ لَهُۥ قَرِينٞ
If anyone withdraws himself from remembrance of (Allah) Most Gracious, We appoint for him an evil one, to be an intimate companion to him.
Katika aya hii utaona sheikh Yusuph Ali ametarjama kwa tutumia neno companion kumaanisha qareen lakini pia Sahihi International nao wametumia neno hilohilo companion, mpaka hapa utaona neno qareen linasimama kama mshirika au mwenza.
Katika aya hiyo Allah anasema ambaye ataacha kumkumbuka yaani kukumbuka rehma zake atateuliwa shetani ambaye atakuwa ni qareen(mshirika) kwake.
Katika hadithi pia qareen katajwa katika hadithi hii:-
عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّـهِ صَلَّى اللَّـهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "كُلُّ إِنْسَانٍ مُعَلَّقٌ بِقَرِينِهِ". قَالُوا: وَأَنتَ يَا رَسُولَ اللَّـهِ؟ قَالَ: "نَعَمْ، وَلَكِنَّ اللَّـهَ أَعَانَنِي عَلَيْهِ فَأَسْلَمَ."
Imepokewa kutoka kwa ibn masood amesema , Mtume amesema"Kila mtu ameunganishwa na qareen wake." Wakauliza: "Na wewe, Ewe Mtume wa Allah?" Akasema: "Ndio, lakini Allah amenisaidia dhidi yake, wa kwangu amesilimu.

Hivyo kulingana na maelezo hayo naweza sema kuwa :-
Qareen ni mshirika wa mtu kiroho ambaye anaweza kuwa sababu ya mtu kufanya madhambi wengi katika wanazuoni wanasema mshirika huyo ni katika majini hivyo,mwanadamu anatakiwa kumtegemea Allah ili amkinge na ushawishi wa jini huyu.
 
Umeeleza vyama kabisa, mimi nitaongezea kidogo sana. Hususan hapo ulipotaja "shetani". Qur'an inatueleza mashetani ni katika majini na watu. Au sivyo?

Naamini Qareen ni jini kwa maana ya kutokuonekana, kama zilivyo nafs zote.

Tunapoendelea na kisa cha Adam na In shaa Allah visa vinginevyo tutaliona na kulifanyia tafsil neno Qareen.
Wa bi Llahi Tawfiq.

Ma Shaa Allah, #suhendra, umeona maana ya elimu? Si lazima itokee kwa fukani tu. Ndio maaana nikakwambia na wewe tupe uyajuayo. Usijidunishe kwa kutumia "lisan" isio na maana.
Simba.
 
Umeniuliza kuhusu qareen kama sijakosea nimekwambia Sijui.. hebu nielekeze lakini kwa misingi sahihi ya quran na sunna .. mengine nimekujibu .. ibada na ufugaji wa majini ni ushirikina... Kuagua kwa kutumia majini Mtume wetu hakuwahi kufanya na yeye kama kiigizo chetu kama hakuwahi kufanya na wewe unafanya Bidaa inaingia hapo na bidaa mwisho inageuka na kuwa shirki
 
Kama unasubiri "hitimisho" basi umewahi sana, ndio kwanza tupo utangulizi wa kisa cha adam, bado hata hatujakimaliza kisa hicho, fikiria , kiishe, kianze cha Issa kiishe, na vya mitume wengine viishie, halafu in between kuna vionjo vya kina Arsis.

ElIMU haitaki haraka, unachotakiwa kufanya ni mimi nakupa "skeleton" , wewe ulijazilie nyama kwa tafiti zako za kielimu.

Unapoona tuna hitilafiana, unakuja na elimu yako tunajadili, inaweza kua mmoja wetu yupo sahihi zaidi ya mwengine. Lakini unapokuja na maneno yako matupu tu, nakuona hujaelewa unachhokisoma, unachotakiwa kama hujaelewa uulize. Mbona mimi nauliza maswali?
Simba.
 

Q 17:81. Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke! 81
Na bila shaka hii ni screenshot toka kwa app ya tarjama ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani, shukrani sana Simba kwa hili darsa, hata kama bado hatujalikubali hili la Adam ila wallahi tumestafidi pakubwa mno mpaka hivi sasa. Asante
 
Soma post #3909 na #3910 kuna jibu la qareen.
 

Ahsante kwa jibu lako nimeelewa na nimekubali sababu umeongea kwa dalili mimi ni nani nipinge ... Na umemaliza vizuri sana ( Mwanadamu anatakiwa kumtegemea Allah ili amkinge na huyu jinni ambaye ni shetani )
Iweje kuna watu kama hawa kina Dr Sule , mtoa mada na mfano wa watu hao wanayafuga haya majini na wanategemea katika tiba zao .. nikauliza swali Mtume au mmoja kati ya wanafunzi wake au wanafunzi wa wanafunzi wake katika zile karne tatu Bora walishafanya haya?!
 
Mbona unajihami sana Sheikh? Misingi wangu ni Qur'an, vingine vyote ni sekondari.

Naona Sheikh Lidafo kakujibu hilo na mimi nimetia nyama kidooogo.

Kama hujaridhika na majibu yake tuendelee na elimu.

Vipi na hayo maswali yangu mengine kwako?
Simba.
 
Mtoa mada ni mimi, wapi umeona nafuga majini Sheikh? Nukuu. Au hunisomi vizuri?

Kwanza hujamalizia kujibu maswali yangu, unakurupuka na maswali mengne na unachomekea wasiopo kwa kuwahukumu kwa swali lako. Maana naona ushahukumu kua tunafuga majini. Hio ni dhanna na dhanna si nzuri katika mafundisho ya Uislam.
Simba.
 
وَقَالَ قَرِينُهُۥ هَـٰذَا مَا لَدَىَّ عَتِيدٌ (Surat Qaaf, 23), Hapa pia imetajwa Qareen, ila watafsiri wengine wanasema hii Qareen hapa ni malaika na wakataja malaika kabisa kwa neno kwny tafsiri zao, na hapo ndipo ilipo hoja kubwa ya Arsis....acha tu tusome Qur-an na elimu zake ili tuielewe vyema zaidi
 

Bado sijafika hadhi ya sheikh bado ni mwanafunzi ,,,Rudia swali ambalo sijakujibu.. umeniuliza bidaa nimeona wapi nishakujibu .. la pili nikasema sijui .. ! Bahati nzuri nikaeleweshwa ...
Kwa elimu yangu ndogo niliyonayo unless wewe uniongezee ..Kumuita jini na kuomba akisaidie jambo fulani tayari mnamafungamano na ndio ufugaji wenyewe huo ..
Nami nimekuuliza hayo unayoyafanya Mtume au maswahaba zake washayafanya
 
Ndugu yangu umemsoma Sheikh Lidafo kuhusu Qareen? Umemuelewa? Umeiona na nyama nilioongezea mimi kidooogo?Je, na hapo utasema kua Bwana Mtume Muhamaad (SAW) alikua anafuga jini? Au hujamuelewa alichojibu?

Ukiyajibu na yale maswali yangu mengine utapata jibu kamili ndani ya nafsi yako.
Simba.
 
Mimi nitamuelezea Qareen kwa tafsil, itapofika wakati wake.

Hio ya "malaika" au jini" kama ulivyoandika kwanza, zote ni jitihada za watafsiri, muhadeethin na Maulamaa.
Simba.
 

Nimeelewa na au kuna uelewa fulani unataka wewe niwe nao . Nimesema mimi ni mwanafunzi seems like hakuna jipya unaoweza kunifunza wacha nipite mbali

Mtume Mohamad Rehema na Amani ziwe juu yake hakuwahi kuwatumia majini na huo ndio msimamo ila yeye kama mtume aliwahi na alikuwa na uwezo wa kuongea nao pale wanapojitokeza kwake kumbuka sio kuwaita... Majini yaliwahi kumjia Mtume wasilimishwe .. baada ya kumsikia akisoma Quran ..

Note📌 RasoolAllah Hajawahi kuwaita majini ili awatume, ile awaague watu au kuwa na Urafiki na jini yeyote.

Nitoe onyo wa waislam watakao pita kwenye hili thread kuna wachawi wanaojifunika na kujipa jina la usheikh.. sijui Sharifa majini , de Sule na wengine mfano wa hao ... na kuunasibisha uislamu na kuwatumia hawa viumbe (majini) ilahli wao ni wachawi na ni madai waliosimama katika milango ya jahanam watawatumbukiza katika jehanam . Uislamu sahihi ni kufuata mwenendo wa mtume pamoja na tabeen katika zile karne tatu bora . UFuGAJi, KUTUMIA MAJINI KUFANIKISHA JAMBO FLANI HiYo SI DINI BALI NI UCHAWI ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…