Niliyoyashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau

Niliyoyashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Niliyoyashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau.

Kwa mara ya kwanza nilishuhudia barabara za jiji la Dar zikipigwa deki.

Siku Obama anatua jijini ilikuwa kama siku ya kiyama, mji ulisimama, nakumbuka tulikuwa tunaenda kulipa mahari ya rafiki yetu maeneo ya Msasani, tulitumia masaa kama nane kutoka Tabata mpaka Msasani, kufika ukweni saa nne usiku.
B
aba mkwe akasema wajinga ninyi wapare mna dharau rudini hatupokei mahari yenu, tukamuelewesha akatuelewa, mahari ikapokelewa.

Miezi miwili kabla Hotel ya Kilimanjaro ilishafanyiwa booking hakuna mtu aliruhusiwa kuingia, watumishi wote wakifanyiwa vetting upya, wengine walipewa likizo fupi mpaka Obama alivyoondoka.

Ikulu yetu haikubaki salama ikafanyiwa scanning sitazielezea kulinda heshima ya nchi ila kituko kimoja sitakisahau.

Ila kisichokuwa siri ni kuhusu polisi wetukugeuzwa migambo,jiji la Dar lilikuwa chini ya ulinzi wa CIA kwa muda.

Mitandao ya simu haikubaki salama,mawasiliano yalienda ndivyo sivyo.

Hakuna kibaka wala muhuni wala machinga aliyethubutu kuzurura ovyo,wengine walikamatwa na kufungiwa kwa mkapa

Kuna press conference iliandaliwa nje ya viwanja vya Ikulu ambapo Rais Kikwete na mgeni wake wangeongea na waandishi.

Ikulu ikatoa ratiba ya muda wa hiyo press, na ofisa wa Obama wakaichana chana wakisema muda huo si rafiki maana kutakuwa na mvua viunga vya Ikulu wakaomba ratiba isogezwe mbele masaa mawili.

Mzungu ni hatari muda uleule uliokuwa umepangwa na maofisa wa Ikulu lilitanda wingu mvua ikapiga kwa muda wa lisaa limoja na nusu, ilikatika nusu saa kabla ya muda waliopendekeza wasaidizi wa Rais Obama, kumbe mvua walishaiona kitambo kwenye mitambo yao.
 
Hili mie huwa nalikumbuka ki tofauti, kipindi siku Obama anatua kuna askari alinikamata pale ubalozi wa ufaransa (alipofia yule shujaa wa bunduki)

Nilikua naendesha gari, yule askari alivyonistopisha akasema kosa langu ninaendesha gari nikiwa naongea na simu.

Tulibishana sana mwisho ikawa utata, ikabidi aombe kuongezewa nguvu(alikua anataka kuchomoa ufunguo wa gari mie nikakataa nikamwambia huwezi kuja kuzima tu gari ghafla hujui imetoka umbali gani)

Basi ila jamaa kuona namzidi akili ikabidi aombe nguvu, wakaja askari wawili na bunduki kutokea pale kwenye kibanda Chao walipopigiwa risasi wenzao,

Tukaenda mpaka oysterbay polisi, duh!! Masiala masiala meza kuu naambiwa vua mkanda, nikaona masiala masiala hapa naweza kulala ndani, na nikiingia leo ni mpaka Obama aondoke ndio nitatolewa.

Nikaona isiwe tabu mjinga mpe cheo, ikabidi nitumie hela badala ya kudai haki yangu nikatoa 15k wakaniachia
 
Nilikuwa
Niliyo yashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau

Kwa mara ya kwanza nilishuhudia barabara za jiji la Dar zikipigwa deki.

Siku Obama anatua jijini ilikuwa kama siku ya kiyama,mji ulisimama,nakumbuka tulikuwa tunaenda kulipa mahari ya rafiki yetu maendeo ya msasani,tulitumia masaa kama nane kutoka Tabata mpaka msasani,kufika ukweni saa nne usiku,Baba mkwe akasema wajinga ninyi wapare mna dharau rudini hatupokei mahari yenu,tukamuelewesha akatuelewa,mahari ikapokelewa.

Miezi miwili kabla Hotel ya Kilimanjaro ilishafanyiwa booking hakuna mtu aliruhusiwa kuingia,watumishi wote wakifanyiwa vetting upya,wengine walioewa likizo fupi mpaka Obama alivyoondoka.

Ikulu yetu haikubaki salama ifanyiwa scanning sitazielezea kulinda heshima ya nchi ila kituko kimoja sitakisahau.

Kuna press conference iliandaliwa nje ya viwanja vya Ikulu ambapo Rais Kikwete na mgeni wake wangeongea na waandishi.

Ikulu ikatoa ratiba ya muda wa hiyo press,naofisa wa Obama wakaichana chana wakisema muda huo si rafiki maana kutakuwa na mvua viunga vya Ikulu wakaomba ratiba isogezwe mbele masaa mawili.

Mzungu ni hatari muda uleule uliokuwa umepangwa na maofisa wa ikulu lilitanda wingu mvua ikapiga kwa muda wa lisaa limoja na nusu,ilikatika nusu saa kabla ya muda waliopendekeza wasaidizi wa Rais Obama,kumbe mvua wakishaiona kitambo kwenye mitambo yao.
Nilikuwa Tabata Kimanga siku hiyo,kuhusu mvua labda kama ilinyesha karibu na Ikulu,lkn kwa Tabata Kimanga hapakuwepo na mvua. Kama ilinyesha siku ya pili yake sawa.
 
Hili mie huwa nalikumbuka ki tofauti, kipindi siku Obama anatua kuna askari alinikamata pale ubalozi wa ufaransa (alipofia yule shujaa wa bunduki)

Nilikua naendesha gari, yule askari alivyonistopisha akasema kosa langu ninaendesha gari nikiwa naongea na simu.

Tulibishana sana mwisho ikawa utata, ikabidi aombe kuongezewa nguvu(alikua anataka kuchomoa ufunguo wa gari mie nikakataa nikamwambia huwezi kuja kuzima tu gari ghafla hujui imetoka umbali gani)

Basi ila jamaa kuona namzidi akili ikabidi aombe nguvu, wakaja askari wawili na bunduki kutokea pale kwenye kibanda Chao walipopigiwa risasi wenzao,

Tukaenda mpaka oysterbay polisi, duh!! Masiala masiala meza kuu naambiwa vua mkanda, nikaona masiala masiala hapa naweza kulala ndani, na nikiingia leo ni mpaka Obama aondoke ndio nitatolewa.

Nikaona isiwe tabu mjinga mpe cheo, ikabidi nitumie hela badala ya kudai haki yangu nikatoa 15k wakaniachia
Noma sana
 
Back
Top Bottom