Niliyo yashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau
Kwa mara ya kwanza nilishuhudia barabara za jiji la Dar zikipigwa deki.
Siku Obama anatua jijini ilikuwa kama siku ya kiyama,mji ulisimama,nakumbuka tulikuwa tunaenda kulipa mahari ya rafiki yetu maendeo ya msasani,tulitumia masaa kama nane kutoka Tabata mpaka msasani,kufika ukweni saa nne usiku,Baba mkwe akasema wajinga ninyi wapare mna dharau rudini hatupokei mahari yenu,tukamuelewesha akatuelewa,mahari ikapokelewa.
Miezi miwili kabla Hotel ya Kilimanjaro ilishafanyiwa booking hakuna mtu aliruhusiwa kuingia,watumishi wote wakifanyiwa vetting upya,wengine walioewa likizo fupi mpaka Obama alivyoondoka.
Ikulu yetu haikubaki salama ifanyiwa scanning sitazielezea kulinda heshima ya nchi ila kituko kimoja sitakisahau.
Kuna press conference iliandaliwa nje ya viwanja vya Ikulu ambapo Rais Kikwete na mgeni wake wangeongea na waandishi.
Ikulu ikatoa ratiba ya muda wa hiyo press,naofisa wa Obama wakaichana chana wakisema muda huo si rafiki maana kutakuwa na mvua viunga vya Ikulu wakaomba ratiba isogezwe mbele masaa mawili.
Mzungu ni hatari muda uleule uliokuwa umepangwa na maofisa wa ikulu lilitanda wingu mvua ikapiga kwa muda wa lisaa limoja na nusu,ilikatika nusu saa kabla ya muda waliopendekeza wasaidizi wa Rais Obama,kumbe mvua wakishaiona kitambo kwenye mitambo yao.