Niliyoyashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau

Niliyoyashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau

Tukumbuke kwamba Tanzania wana historia nayo mbaya katika masuala ya ugaidi. Ubalozi wao ulishawahi kukumbwa na tukio.

Kituko zaidi walikiona watumishi wa airport kule, kwani wao waligeuzwa kuwa kama abiria tu, shughuli zote walihodhi USA, hadi uwanja wa jeshi ulikuwa chini yao. Chochote walichokiona ni tishio kiliondolewa hata kama kilikuwa kwenye eneo la jeshi, Ile miti ilipunguzwa matawi yaani wakazi wa eneo lile hakuna rangi walikosa kuiona.
Yaani unaweza kusema walituvua nguo kabisa
 
kuna wanafunzi wa azania walikuepo kwenye kumpokea obama

alikuwepo uncle wangu hapo.. aliniambia hivi

uncle alipokuwa akitusogelea obama kutupungia mkono wanafunzi wote tulihisi kama mazonge hivi,

kama wamekula madawa kiasi kwamba huwezi fanya chochote kupiga kelele wala sijui kama unataka kuleta fujo

aliniambia alizani ni yeye tu sasa kwenye kushare na wanae wakamwambia sisi pia tulijisikia hivyo hivyo

mpaka leo nashindwa kuelewa ilikuwa ni issue gani hapo
Labda jamaa walipuliza hewa ya kufubaza ubongo
 
Niliyoyashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau.

Kwa mara ya kwanza nilishuhudia barabara za jiji la Dar zikipigwa deki.

Siku Obama anatua jijini ilikuwa kama siku ya kiyama, mji ulisimama, nakumbuka tulikuwa tunaenda kulipa mahari ya rafiki yetu maeneo ya Msasani, tulitumia masaa kama nane kutoka Tabata mpaka Msasani, kufika ukweni saa nne usiku.
B
aba mkwe akasema wajinga ninyi wapare mna dharau rudini hatupokei mahari yenu, tukamuelewesha akatuelewa, mahari ikapokelewa.

Miezi miwili kabla Hotel ya Kilimanjaro ilishafanyiwa booking hakuna mtu aliruhusiwa kuingia, watumishi wote wakifanyiwa vetting upya, wengine walipewa likizo fupi mpaka Obama alivyoondoka.

Ikulu yetu haikubaki salama ikafanyiwa scanning sitazielezea kulinda heshima ya nchi ila kituko kimoja sitakisahau.

Kuna press conference iliandaliwa nje ya viwanja vya Ikulu ambapo Rais Kikwete na mgeni wake wangeongea na waandishi.

Ikulu ikatoa ratiba ya muda wa hiyo press, na ofisa wa Obama wakaichana chana wakisema muda huo si rafiki maana kutakuwa na mvua viunga vya Ikulu wakaomba ratiba isogezwe mbele masaa mawili.

Mzungu ni hatari muda uleule uliokuwa umepangwa na maofisa wa Ikulu lilitanda wingu mvua ikapiga kwa muda wa lisaa limoja na nusu, ilikatika nusu saa kabla ya muda waliopendekeza wasaidizi wa Rais Obama, kumbe mvua walishaiona kitambo kwenye mitambo yao.
Ile mvua, shikamoo …(…..)
 
Yaani unaweza kusema walituvua nguo kabisa
Pamoja na yote hayo kufanyika, hakuna kiongozi aliyehoji hali hiyo kutokea, kisababishi pamoja na impact yake.

Waafrika saazingine tuna akili kama za ngiri.

Ngiri akifukuzwa na simba, akapiga chenga na kusevu, huwa hana muda wa kutafakari, ama hata angalao tu dakika moja ya kusimama kusikilizia hofu inavyodundisha moyo, hakuna.

Akisimama ni muda huo huo kuanza kuchakurachakura udongo kutafuta minyoo chakula chake pendwa, keshasahau.
 
Mzungu ni hatari muda uleule uliokuwa umepangwa na maofisa wa Ikulu lilitanda wingu mvua ikapiga kwa muda wa lisaa limoja na nusu, ilikatika nusu saa kabla ya muda waliopendekeza wasaidizi wa Rais Obama, kumbe mvua walishaiona kitambo kwenye mitambo yao.
Hii kali aisee
 
nakumbuka kuna mtu fulani mchizi alikuwa analala chini ya daraja la reli karibu pale majani ya Chai, kuingia barabara ilipokuwa zamani Tigo makao makuu.. Sasa kumbe FBI washamfuatilia yule msela zaidi ya mwezi, anaenda kariokoo anachukua mabox matupu anakuja anatandika hapo analala chini ya kidaraja fulani kilikuwa pale...Jamaa wanazoom kama mwezi hivi, wakajua hana issue.. Basi ilivyokaribia ujio wa Obama, FBI wakawambia polisi wetu, kuna mtu analala pale kwenye daraja.. Tumemchunguza hana madhara, ila kamtoeni pale ... Polisi, unavyojua walimshukia kama mwewe, hinginja hingija, tupa kule, mtama , tanganyika jeshi.... Wale FBI wanawashangaa hawa polisi, wakawambia huyo hana madhara ...

Yaani hiyo kitu ilikuwa hatari tupu..
Teh teh 😃 😃 😃 dah!...maisha haya..
 
Aisee mi nakumbuka nilikuwa nakaa migomigo wapangaji wenzangu wote wakatoka kwenda barabarani kwenda kuuona msafara wa obama mi nikasema upuuzi huo siufanyi nikawasha feni nikalala usingizi wa maana nimekuja kuamka bado wako barazani wanasimuliana kuhusu msafara wa obama
 
Back
Top Bottom