Wadau,
Mimi ni msomaji sana wa historia za Sheikh wangu,
Mohamed Said na nimekuwa na bahati ya kukutana naye pia nyumbani kwake Magomeni Mapipa, miaka miwili iliyopita. Kama kawaida yake, ukimchokoza na kifurushi cha jero, yeye anakuletea kifurushi cha 50k.
Hebu leo kwa faida ya wasomaji, tupate historia ya Denis Phombeah, kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika. Nimemsoma kwenye kitabu cha The Life and Times of Abdulwahid Sykes; Untold Stories of Muslims Struggle in Tanganyika. Huwa sichoki kukisoma.
Sasa, sijui tutaanzia wapi, ila niko interested sana na safari ya Denis Phombeah na safari yake Salisbury akiwa na Ali Sykes.
Karibu
Mohamed Said