Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
NIMEAIBIKA; NIMESHINDWA KUFUNGUA SHAMPENI KWENYE SHEREHE YA HARUSU
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Aiseeh! Sijui kwa kweli. Ni stori yenye kufedhehesha. Ushamba flani hivi. Daaah!
Nadra sana kuniona nimevaa suti. Na ukweli ni kuwa nikivaa suti sehemu yoyote watu huniona mimi ndiye mwenye shughuli, ama Mgeni wa heshima, kimsingi nakuwa mtu mwingine kabisa. Yaani hutojua ni yule Mtibeli anayependa kuvaa kawaida.
Nakumbuka matukio makubwa matano ndio watu waliwahi kuniona nikivaa suti. Na wengi wakiniona hufikiri ni AI. Picha zangu wanahisi nimefanya mafekeche. Lakini ndio Mimi bhana!
Jana usiku nilipata mualiko fulani kwa mtu fulani wa heshima hivi. Nikienda na Mke wangu huwaga ndio navaaga suti. Wachunguzi wa maisha yangu walishanijulia kabisa.
Nilivaa Suti ya rangi ya Bluu Navy. Dadeki! Suti ilinisimama kama nini. Juu kama kawaida yangu nywele nyingi kama mwanafalsafa mpole hivi, na Miwani nyeusi.
Tatizo langu nikivaaga nikapendeza ninajikuta navimba hivi, kiburi na jeuri inakuwa juu sana. Hasa mfukoni au simu iwe na kihela fulani hivi. Basi mabega juu kama ngongoti. Uso nimeuweka kijentromen.
Tatizo unavaa suti alafu huna gari hapo ndipo kizaazaa. Anyway nilichukua bolt mpaka maeneo ya Masaki pale kwa huyo mtu wa heshima.
Ilikuwa sherehe ya harusi ya kijana wake. Ni harusi simple ambayo haikuwa na watu wengi kivile lakini pia sio wachache. Takribani watu 100 hivi.
Nilipoingia walijua nimeingia. Ingawaje siku maarufu na hakuna aliyekuwa ananijua zaidi ya mtu wa heshima.
Basi kila mtu aligeuka kututazama mimi na mke wangu. Tulipendeza kama Superstars fulani hivi.
Basi dada mmoja hivi aliyevalia vizuri alitulaki nakutuonyesha sehemu ya kukaa. Shida inakuja kwa ile suti niliyoivaa na jinsi Mimi na mke wangu tulivyopendeza waliona watupe siti za mbele kabisa ungedhani sisi ni ndugu wa karibu wa ile familia.
Kwangu ilikuwa heshima sana. Mtu wa heshima aliponiona alinipa ishara kwa mkono kwamba Amendola. Na mimi nikainamisha kichwa chini kidogo huku nikimtazama kama ishara ya kukubali ukaribisho wake.
Kisha kimakeke nikawa najiweka sawa. Huku mtu w vinywaji akiwa ameshafika. Tukawekewa vinywaji ambavyo alikuwa amevibeba.
Shughuli ikawa inaendelea, wapiga picha na video walikuwa wakija kunichukua mara kwa mara. Hii ilinifanya nijione mtu fulani hivi ambaye naweza kusema jambo watu wakakaa kunisikiliza.
Sherehe inaendelea ujue.
Sasa muda wa kufungua Shampeni ukafika. Mimi sikuwa na wasiwasi kwani nilijua sipo kwenye ratiba yoyote na mimi ni mgeni tuu.
Nashangaa MC anaita, lakini si jina langu. Alikuwa MC wa kike, mrembo fulani hivi sijui nisemeje, akaniita kwa jina la ajabu sana, la Kilatino la mapenzi.
“Señooooor Don Amore! Tafadhali tunaomba uje mbele utusaidie kufungua Champagne!”
Dadeki!
Nikageuka kushoto na kulia kumtafuta huyo Don Amore. Maana kwa namna alivyoliita lile jina nilijua lazima ni bilionea fulani kutoka Argentina.
Kumbe ananiangalia mimi!
Nikajifanya sijamsikia. Akaliita tena huku akinyoosha mkono upande wangu.
Hapo ndipo nilipojua suti yangu imenipeleka kwenye matatizo.
Mke wangu akanigusa kidogo kwenye paja huku akinitazama kwa tabasamu. Nikajua anamaanisha nini. Nisimame.
Mimi nikasimama taratibu. Nikafunga kifungo cha suti yangu. Nikavuta koti kidogo chini, nikanyanyua mabega kama kawaida yangu. Uso nimeuweka kijentromen. Nikatembea kuelekea mbele huku watu wakinipigia makofi.
Aiseeh! Nilitembea kama mtu anayeenda kupokea tuzo ya Nobel.
MC akanipokea kwa tabasamu kubwa. Akanikabidhi chupa ya Champagne.
Sasa ndugu zangu, kuna mambo mawili ambayo sikuwahi kuyafanya katika maisha yangu. La kwanza ni kufungua Champagne. La pili ni siri yangu... maana sitaki aibu mbili za kufungua mwaka.
Nilipoishika ile chupa nikajifanya naichunguza lebo yake. Kama vile ninaangalia mwaka ilipotengenezwa na ubora wa zabibu zilizotumika. Kumbe natafuta pa kuanzia!
Niliona kuna karatasi fulani ya dhahabu pale juu. Nikaanza kuichokonoa kwa kucha. Nikafanikiwa kuitoa. Chini yake nikakutana na vyuma fulani vilivyojizungusha.
Dadeki! Hivi vyuma navifunguaje?
MC akawa ananitazama kwa tabasamu. Watu wakawa wanasubiri. Kamera zote zimeelekezwa kwangu. Nikaanza kuzungusha kile chuma upande mmoja. Hakifunguki. Nikazungusha upande mwingine. Kikalegea kidogo.
Nikajipa moyo.
Tatizo nikawa nimeanza kutokwa na jasho. Na ujue nilikuwa nimevaa suti ya bei ambayo sitaki kuitaja hapa kwa sababu hamtanielewa.
Baada ya kuhangaika kidogo, nikafanikiwa kuondoa kile chuma. Sasa nikabaki na kizibo.
Nikakishika kwa vidole na kuanza kukivuta juu. Hakiji!
Nikakizungusha. Hakiji! Dadeki!
Nikakivuta tena kwa nguvu kidogo. Wapi! Salamaleko.
Hapo nikaanza kuona kama watu wanazidi kuwa wengi kuliko wale mia moja wa mwanzo.
MC akaniambia kwa sauti ya chini, "Just twist it gently, sir."
Nikamtazama kwa tabasamu nikamwambia, "I know, I know."
Uongo mtupu! Leo u-much know wangu nimekamatika.
Nilikuwa sijui chochote.
Nikakumbuka kwenye filamu huwa watu wanatikisa chupa kabla ya kuifungua. Nikasema labda tatizo sijaitikisa.
Nikaanza kuitikisa. Tikitikitiki!
MC akashtuka.
"No, no, no, sir! Don't shake it!"
Nikajifanya nacheka. Nikamwambia, "Relax, young lady."
Kumbe nilikuwa nimeshaishiwa step. Niliabika sana aiseeh!
Nikajaribu tena kukizungusha kile kizibo. Wakati huo kidole gumba kimeanza kuuma. Mkono unateleza kwa jasho. Miwani yangu nyeusi niliyoivaa kichwani imeanza kunisumbua. 😄 🤣
Mtu mmoja kutoka upande wa kulia akasema, "Hold the cork firmly!" Mwingine akasema, "Turn the bottle!" Mwingine, "Use the towel!"
Dadeki! Ghafla ukumbi mzima ukageuka darasa la kufundisha Mtibeli kufungua Champagne. Milunzi mingi na sasa Mtibeli nimegeuka Mbwa wa Njeree.
Nikaanza kukasirika kimoyomoyo.
Hivi watu hawa wanadhani mimi sijui kufungua Champagne?
Tatizo ni kwamba ni kweli sikuwa najua. Sasa nikajikaza. Nikashika kile kizibo kwa nguvu. Nikazungusha chupa huku nikivuta juu kidogo.
Ghafla!
PWAAAAAA!
Kizibo kikaruka kama risasi!
Mimi kwa mshtuko nikarudi nyuma hatua mbili. Chupa ikaniponyoka kidogo mikononi, nikajaribu kuidaka. Champagne ikaanza kumwagika kwa fujo, ikapiga kwenye koti langu, shati, na sehemu ya suruali.
Watu wakapiga kelele!
Wengine wakacheka, wengine wakapiga makofi.
MC akawa anasema, "Wooooow! Congratulations!"
Congratulations za nini wakati mimi nimefedheheka
Nilikuwa nimelowa kama mtu aliyekimbia mvua kutoka Kimara mpaka Masaki.
Nimekoma walahi! Msiniite kwenye sherehe zenu. Mnikome!
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam