mkubwa wa habari
Member
- Jun 8, 2023
- 24
- 37
Wakuu hope salama, polenii na majukumu ya kulijenga taifa na familia kwa ujumla.
Dhumuni la kuandika huu uzi ni namna now navyojiskia, ilikuwa mwaka 2018 baada ya kumaliza chuo nikiwa kitaa sina mchongo nikapata taarifa kuwa kuna kampuni ipo Abu Dhabi inahitaji wafanyakazi wa kwenye meli yani tuite ubaharia sasa nikafanyiwa mpango kweli nikapata ile kazi maeneo ya Mussafa, Adnoc, kwa wanaofahamu haya maeneo watathibitisha kuwa jua lake ni la kuchemsha yai likaiva, sasa na mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye boti kama msaidizi kwa hiyo tunakuwa nje kuanzia asubuhi mpaka jioni
Hii hali ilinitesa sana nikaamua kuachalia mbali ile kazi na kurudi bongo kusoma CPA, kwaajili ya kuendeleza professional yangu. Sasa imekuwa lawama kwa ndugu kila mahali wananinyooshea mikono kuwa nimekosea kwa uamuzi nilioufanya sasa inanipa shida na sometimes mwenyewe nimeshaanza ingiza hofu mpaka hata elimu ya CPA inashindwa kupanda kutokana na maneno ya ndugu.
Kwa hiyo wakuu nimekuja kwenu kwa ushauri wenu kuhusu ili kuwa uamuzi nilioufanya ni sawa ua nimekosa sana manake kazi haikuwa ngumu ila mnakesha juani sasa nikapoteza raha kabisa.