AL SHARPTON
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 2,797
- 953
Kazi kweli
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
![]()
😛eep:
Wakuu nimeamua kwa hiyari yangu na pasipo kulazimishwa na mtu yoyote kuitosa club ya Arsenal.Nina sababu nyingi za kuitosa The Gunners.
[1] Kukwepa magonjwa ya moyo.
[2] Imeshindwa kutwaa kikombe chochote kwa muda mrefu sana.
[3] Arsenal imekuwa gulio la kuuza wachezaji wake mahiri kwa Club nyingine
Baada ya kutafakari kwa kinaa na bila kushawishiwa au kulazimishwa na mtu au kikundi chochote nimeamua kujiunga na Club ya Manchester United yenye kutumia uwanja Old Trafold.Zipo sababu kibao lakini nitazitaja chache.
[1] Manchester United inaongozwa na manager mwenye mafanikio makubwa kuliko makocha wote wa UK.
[2] Manchester United imechukua ubingwa wa ligi kuu ya UK mara 19,timu inayoikaribia ni Liverpool pekee yake imechukua ubingwa mar 18 tu.
[3] Manchester United inakaribia kuweka rekodi mpya kwa kuchukua ubingwa mara 20, mpaka leo hii inaongoza ligi kwa tofauti ya point 12.
[4] Ukiishabikia Mancheter United uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari ni mdogo sana.Kila wakati una kuwa ni mtu wa kucheka na kufurahia maisha duniani.
[5] Mwaka 1999 iliweka historia kwa kuchukua vikombe vitatu.Ubingwa wa ulaya.ubingwa wa Uk na Kombe la ligi.
[6] Mashabiki wa Manchester United ni wakarimu, wapole na wenye kujua kuchambua soka. Sifa hizo zinanihakikishia kwamba nitapokelewa vizuri.
Wapenzi wa Arsenal mtanisamehe sana kuhama club ni jambo la kawaida kwa mashabiki kama ilivyo kawaida kwa wachezaji. Siwezi kuendelea kusononeka hapa duniania kisa kupenda Club mbovu.
Nakala: Wacha1 Idimi Belo Steve Dii Mphamvu Dark City gfsonwin The Boss BAK Rejao Viper mfarisayo MwafrikaHalisi Kibunango Maxence Melo EMT Balantanda Mwita Maranya
Hahahahahahaha lol! hujui kupenda wewe Ngongo ungekuwa unajua kupenda usingehama Gunners. Raha ya kupenda ni pale unapofurahia ushindi na kusononeka pale mnapofanya vibaya. Hakuna timu hapa duniani ambayo inashinda kila leo. Vipi sasa ule mpango wako wa kuhamia Chelsea msimu ujao umeishia wapi? Hahahahahah lol! Dongo hiloooo. Karibu tena Gunners tutakupokea kwa mikono miwili weye mwana mpotevu na kukufanyia sherehe kubwa sana.
Mkuu kile kichapo cha goli 8 kama si kutumia umahiri wangu Wacha1 alikuwa anakimbilia sumu nikaona duh isiwe taabu ngoja nihame chama.
Hahahahahahaha lol! ila inakosesha raha Mkuu hata ikiwa goli moja tu kufungwa ni kufungwa tu, ngoja siku mtundikwe goli nane kama hutarudi Gunners weye!
Process ya kwanza lazima uwe karibu na hospital ya magonjwa ya moyo.Jiunge na mfuko wa bima ya afya....
Inategemea unapigwa hizo goli 8 na nani. Tulipigwa goli 6-1 na man city ikauma ila tukasahau na ndio huo mwaka man city wakachukua ubingwa dakika ya 93. Uzuri wa United ni kwamba pamoja na kufungwa ila makombe yanatufanya tusahau maumivu yote.