Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu nimeamua kwa hiyari yangu na pasipo kulazimishwa na mtu yoyote kuitosa club ya Arsenal.Nina sababu nyingi za kuitosa The Gunners.
[1] Kukwepa magonjwa ya moyo.
[2] Imeshindwa kutwaa kikombe chochote kwa muda mrefu sana.
[3] Arsenal imekuwa gulio la kuuza wachezaji wake mahiri kwa Club nyingine
Baada ya kutafakari kwa kinaa na bila kushawishiwa au kulazimishwa na mtu au kikundi chochote nimeamua kujiunga na Club ya Manchester United yenye kutumia uwanja Old Trafold.Zipo sababu kibao lakini nitazitaja chache.
[1] Manchester United inaongozwa na manager mwenye mafanikio makubwa kuliko makocha wote wa UK.
[2] Manchester United imechukua ubingwa wa ligi kuu ya UK mara 19,timu inayoikaribia ni Liverpool pekee yake imechukua ubingwa mar 18 tu.
[3] Manchester United inakaribia kuweka rekodi mpya kwa kuchukua ubingwa mara 20, mpaka leo hii inaongoza ligi kwa tofauti ya point 12.
[4] Ukiishabikia Mancheter United uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari ni mdogo sana.Kila wakati una kuwa ni mtu wa kucheka na kufurahia maisha duniani.
[5] Mwaka 1999 iliweka historia kwa kuchukua vikombe vitatu.Ubingwa wa ulaya.ubingwa wa Uk na Kombe la ligi.
[6] Mashabiki wa Manchester United ni wakarimu, wapole na wenye kujua kuchambua soka. Sifa hizo zinanihakikishia kwamba nitapokelewa vizuri.
Wapenzi wa Arsenal mtanisamehe sana kuhama club ni jambo la kawaida kwa mashabiki kama ilivyo kawaida kwa wachezaji. Siwezi kuendelea kusononeka hapa duniania kisa kupenda Club mbovu.
Nakala: Wacha1 Idimi Belo Steve Dii Mphamvu Dark City gfsonwin The Boss BAK Rejao Viper mfarisayo MwafrikaHalisi Kibunango Maxence Melo EMT Balantanda Mwita Maranya
Hauna tofauti na wale wanawake wanao amua kuwa ma-blender kwa sababu wameumizwa na wanaume zao..
He he mbona unahamaki hivyo kijana we jana umeangalia mechi Man v/s Norwich,kama ungeliona hiyo machi hata wewe ungejiunga na mashetani wekundu.
Haukuwa na mapenzi yoyote kwa Arsenal.....Na hauna mapenzi yoyote kwa Man Utd...........Nina uhakika Utd wakiteleza utahamia Spurs.....Kama sio City au Chelsea.....Na mwisho utajikuta umerudi Arsenal.....Heshima sana wapenzi wa ligi kuu ya UK.
Jana majira ya saa 4 usiku Manchester United waliitandika bila huruma Aston Villa bao 3 bila majibu.Mabao yote ya Man Utd
yalifungwa kipindi cha kwanza na mshambuliaji mahiri mtakatifu RvP.Kila goli lilikuwa na sababu zake hapa nahainisha kwa kifupi sana.
Goli la kwanza lilikuwa kwaajili ya kuchukua ubingwa mara 20.
Goli la pili lilikuwa goli bora la msimu mzima (Goli la mwaka).
Goli la tatu kuhakikisha RvP anakuwa mfungaji bora wa msimu huu.
Wale waliodhani Ngongo alikurupuka kukimbia chama la Wenger sasa wanatahayari na kujutia uamuzi wa kuendelea kushabikia timu inayopigania nafasi ya nne.
Karibuni Man Utd tufurahie makombe na mpira mzuri,karibuni Man Utd tufurahie mabao ya RvP.
Machester United Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.Raha dunia.
Nakala: Wacha1 Idimi Belo Steve Dii Dark City EMT Balantanda Maxence Melo mfarisayo Kibunango Mphamvu gfsonwin MwafikaHalisi Mwita Maranya @BelindaJacob Peasant Godlisten Masawe ACCOUNT FULL BAK Nzi Pianist.
Haukuwa na mapenzi yoyote kwa Arsenal.....Na hauna mapenzi yoyote kwa Man Utd...........Nina uhakika Utd wakiteleza utahamia Spurs.....Kama sio City au Chelsea.....Na mwisho utajikuta umerudi Arsenal.....
GLORY HUNTER.................
teh teh tehhhhh, hata mimi nahamia airtel, lol!Mkuu Ngongo hukuwa na mapenzi ya kweli kwa Arsenal. Wewe ni wale washabiki wanaopenda timu ambazo zinakuwa mabingwa tu, timu ikianza kusuasua unasepa haraka sana. Kila la heri na MANU ila msimu ujao ukiona wanasuasua sitashangaa ukitutaarifu kwamba umeamua kuhamia MANC lol!!! Hongera kwa ubingwa
Good day 🙂