Nimeacha Kushabikia Taifa Stars rasmi

Nimeacha Kushabikia Taifa Stars rasmi

Nikiwa na akili zangu timamu kabisa wala sijashawishiwa na mtu yoyote yule, kwa aibu hii tuliyoipata leo toka kwa Algeria, naacha kushabikia timu ya taifa, kutiana presha sipendi tena, japo nitaonekana sio Mzalendo ila potelea mbali.

we acha upuuzi ww, unaacha kuishabkia stars et kisa imefungwa 7-0.
mbna brazil alpgwa gol hzo na ujerumani tena kwenye ardhi yake!!
Ulimbukeni wa mawazo Yako
 
msiwage mnajipa matumaini sana na timu zetu...mtakuja kufa na presha shauri zenu...
 
Poleni sana wadau wenzangu. Issue ni kwamba magoli Taifa Stars waliyoyakosa hapa Dar ndiyo magoli waliyopata Algeria kule kwao. Kwa hiyo tungeyapata magoli yale tungekuwa tunacheka. Kingine ni tabia ya waTz kukata tamaa mapema.

Niliangalia magoli aliyofungwa yule kipa wa kwanza yalikuwa mepesi na kufungwa goli la mapema kukawapa hofu wachezaji wa Stars. Nilipredict mapema kabisa lazima kutakuwa na red card kwani back ilikosa umakini na wakawa wepesi wa kucheza rafu kwa hasira. Sasa Waarabu wanajua fitina sana ya mpira ukicheza rafu lazima kadi utaipata.

Hii ni tabia ya waTz kwamba hatuko aggressive, tunakata tamaa mapema na mara nyingi hatuna plan B always. Ndivyo tulivyo hata kwenye maisha yetu. Tunakuwa na fear of unknown ndiyo maana hatusongi mbele kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni nk.

Tabia hizi za watanzania hata kupigania haki yetu twaogopa, tukionewa tunakaa kimya. Wakenya na waganda wanatushangaa sana. Ili tufanikiwe lazima tuondokane na utumwa wa akili zetu na hii ni kujiamini, kufanya kazi hata kwenye mazingira magumu na tusipende vitu vya chee.
 
we acha upuuzi ww, unaacha kuishabkia stars et kisa imefungwa 7-0.
mbna brazil alpgwa gol hzo na ujerumani tena kwenye ardhi yake!!
Ulimbukeni wa mawazo Yako
Brazilamechukua ubingwa wa dunia mara 5, Taifa stars wana kombe gani?
 
Mimi nilishaacha kitambo sana,niliona mpira tunaucheza mdomoni kwa maneno,kuliko uwanjani kwa miguu.
 
Nikiwa na akili zangu timamu kabisa wala sijashawishiwa na mtu yoyote yule, kwa aibu hii tuliyoipata leo toka kwa Algeria, naacha kushabikia timu ya taifa, kutiana presha sipendi tena, japo nitaonekana sio Mzalendo ila potelea mbali.
Una akili sana !
 
Back
Top Bottom