Nimeacha kusikiliza Wasafi Fm kwa sababu ya Zembwela

Nimeacha kusikiliza Wasafi Fm kwa sababu ya Zembwela

Chumvi na ndimu, wananifurahisha Sana kwenye magazeti, huwezi penda Kila kitu na huwezi pendwa na Kila Mtu, Mimi huwa naongeza na sauti kipindi cha chumvi na ndimu na michezo, Sasa walivyoanza kuhama hama sijui nisikilize ipi
Kitenge nasikia hayuko wasafi tena.
 
Kichekesho ni kua mtoa uzi unasikiliza wasafi kwA ajili ya serious issues
Wasafi imeji-dubb kama stesheni ya entertainment
Mtu kalipia tangazo la biashara yake sio serious issue hiyo? We veepe. Watu wenye hela za kununua hizo bidhaa sio hao anaowalenga zembwela kwenye komedi zake. Watu wenye uwezo wa kufanya manunuzi wanaanzia 40+, hawa hawapendi mahoka yaliyopitiliza, they have so many fish to fry
 
Duh bongo uchawi mwingi wanatamani ushuke chat kubabeki hii nchi sio..wananchi wake maneno mengi kazi kidogo
 
labda anataka wadau wapande dau na yeye atimuke zake.
 
Zimbwela bwana.

Amenifanya nimeacha kusikiliza Redio ya Wasafi asubuhi.

Huyu jamaa anafanya comedy hata kwenye serious issues, anatengeneza kelele masikioni na kupoteza muda wa wasikilizaji wake akidhani kuwa wasikilizaji wako tayari kusikiliza kila kitu anachosema na kufanya kwenye studio, ananiboa.

Hata bidhaa anazozitangaza ninaziona kama zisizo na ubora kwa namna anavyopitiliza kuzinadi. Anasahau kuwa "kizuri kinajiuza na kibaya kinajitembeza na kupambwa mno".

Anachohitaji mtu kwenye bidhaa ni kujua jina la bidhaa, aina na ubora wake dhidi ya bidhaa nyingine zilizoko kwenye soko ova!

Sijui kama hii inanipata mimi tu.
ww auto humuelw
 
Back
Top Bottom