Nimeachana na mpenzi wangu

Nimeachana na mpenzi wangu

FAMILY COMES FIRST

Hii ndio kanuni namba moja kwa mwanaume yeyote anayejielewa ambaye ana mchepuko/michepuko na lazima ahakikishe mchepuko anajua hilo hataki apite hivi

Yeye ni kiburudisho tu, cum dustibin

Wife wa ndoa (mama watoto) ndio kipaumbele cha kwanza
Na hiyo ndio 'principle' ukipata majanga, atakayepambana ni mke wa ndoa
 
Huyu rafiki yangu (mchepuko) ana ujauzito wa miezi miwili; baada ya kumuona jana jioni hana mishe, nikaamua kumpigia simu ili nimtoe 'out' angalau tukapige kitimoto na maji ya dhahabu.

Tukakubaliana tukutane kiwanja fulani; baada ya kufika tukapiga kilo mbili za kitimoto pamoja na vinywaji, bahati nzuri sisi wote ni wanywaji.

Baada ya kupiga maji sana, tukawa tunajiandaa tuondoke, ile nataka kusimama tu, bi mkubwa (wife) akanipigia simu, tukabadilishana abc na kumuambia kesho nitakutumia kiasi fulani cha salio.

Ile mchepuko kusikia naongea na bi mkubwa kuhusu mikakati, akajawa na wivu na kuanza kulalamika na kusema, ''anayependwa hapa ni mtu mmoja tu''. Nikamuuliza kwa nini unasema hivyo, hakunijibu,matokeo yake akawa ananipa pochi yake nibebe. Nikamwambia mimi ni mwanaume siwezi kubeba pochi/mkoba wako.

Alikuwa ameshikilia chupa ya maji akatupa kule, tukavutana mpaka tukafika nyumbani; ile tumelala kitandani hataki kuguswa, akaamka kwa hasira usiku huo na kusema hatonitafuta tena na anaenda kwake; ikabidi nimwambie sawa hakuna shida.

Baada ya kuondoka usiku huo, nikamtumia ujumbe na kumwambia; mimi niko huru sasa kuwa na mtu mwingine,nawe pia kuwa huru kuwa na mwanaume mwingine.

Mpaka sasa hajajibu huo ujumbe; na sitegemei kumbembeleza arudi kwenye mahusiano.​
Umeenda kunywa pombe na mtu mwenye ujauzito wa miezi miwili?
 
Kwa wivu huo mkali juu yako,amini kashakuendea sana kwa Waganga huyu akuteke mazima.
Siku akikutana na Fundi wa kweli,unavunja Nyumba yako Mkuu.
Inawezekana mkuu, kwa sababu nimekuwa mwepesi sana wa kuchangia shughuli zake
 
Huyu rafiki yangu (mchepuko) ana ujauzito wa miezi miwili; baada ya kumuona jana jioni hana mishe, nikaamua kumpigia simu ili nimtoe 'out' angalau tukapige kitimoto na maji ya dhahabu.

Tukakubaliana tukutane kiwanja fulani; baada ya kufika tukapiga kilo mbili za kitimoto pamoja na vinywaji, bahati nzuri sisi wote ni wanywaji.

Baada ya kupiga maji sana, tukawa tunajiandaa tuondoke, ile nataka kusimama tu, bi mkubwa (wife) akanipigia simu, tukabadilishana abc na kumuambia kesho nitakutumia kiasi fulani cha salio.

Ile mchepuko kusikia naongea na bi mkubwa kuhusu mikakati, akajawa na wivu na kuanza kulalamika na kusema, ''anayependwa hapa ni mtu mmoja tu''. Nikamuuliza kwa nini unasema hivyo, hakunijibu,matokeo yake akawa ananipa pochi yake nibebe. Nikamwambia mimi ni mwanaume siwezi kubeba pochi/mkoba wako.

Alikuwa ameshikilia chupa ya maji akatupa kule, tukavutana mpaka tukafika nyumbani; ile tumelala kitandani hataki kuguswa, akaamka kwa hasira usiku huo na kusema hatonitafuta tena na anaenda kwake; ikabidi nimwambie sawa hakuna shida.

Baada ya kuondoka usiku huo, nikamtumia ujumbe na kumwambia; mimi niko huru sasa kuwa na mtu mwingine,nawe pia kuwa huru kuwa na mwanaume mwingine.

Mpaka sasa hajajibu huo ujumbe; na sitegemei kumbembeleza arudi kwenye mahusiano.​
Ila inavoonekana umeumia Sana alivokunyamazia mpaka ukalileta huku
 
Back
Top Bottom