Nimeachwa kisa siko romantic

Yaani kwanza mi mtu akishaanza izo mambo sijui umekula nini, unafanya nini mara sijui njoo nikulishe bla bla za ivo nachefukwa chap kwa haraka

Muhimu upate mwanamume anaekupenda, mwema, alietulia, alie karibu na Mungu wake, huyo ndie mwanaume haswaa. Hayo ya romantic sijui nini huwa mnayaokotea wapi lakini, mbona hayaendani na waafrika!! Wanawake wa sasa mnavituko mjuwe, na mnapenda kuiga iga tamaduni za nje! Mabinti wa sasa sio kama wa zamani walikua wakiishi kwa upendo na amani, na walidumu kweni ndoa zao. Na ukiangalia asilimia kubwa ya wasichana wa siku hizi huachwa sababu ya midomo, ujuaji n.k. Munatabu kweli kweli ninyi wakina dada.



Wakina dada, Ombeni sana mupate wanamume wema, waliotulia na walio karibu na Mungu.

kwa wakina kaka, Ombeni sana mupate wanawake wema, waliotulia na walio karibu na Mungu.
 

Kipengele ni

Anaekupenda
Alietulia [emoji3526]
 

Unajua ya kwamba unaweza pata mwanaume/mwanamke mwema, katulia lakini hakupendi? What if akawa mwema huko nje kwako akawa mwiba?

By the way kila mtu ana mahitaji yake ni vema unapoomba kwa imani yako mueleze Mungu mwanamke/mwanaume unayemtaka bila kupindisha
 


Mwanaume mwema na aliekaribu na Mungu hawezi acha kukupenda, kwa maana ingine mwanaume huyo hatembei nje ya ndoa/Mahusiano. Huyu ndie mwanaume haswaa. Na mwingine ndio huyoo unaemkusudia, aweza akawa ametulia na akajifanya mwema kwako kumbe ni balaaaa 😄
 
Kuna wanaojua kuwa romantic ni ile mvua ya mameseji, uko wapi, umekula nini, unafanya,nini umevaa nini....maneenah kabisa!

Sijavaa kitu, nimejigeuza firigisi ngozi ndani nyama nje.
Wewe mwanamke huwa unanifurahisha sana.

Yaani upo ki-gangstar zaidi, hebu sogea kwa wakala unipe namba ya wakala ukapoze koo kwanza
 
hahahhhahahaha

Kabisaaa, fanya hivyo sasa kabla sijapotea hewani. Bad girl gone good!

Nilipokuwa o'level tulikuwa na bad girl darasani tukimuita Beka. E.Bakari mwenyewe akijiita Beka
Waiterrr lete kama nilivyooo, Heineken 3 zinazovuja jasho tahadhali... bill kwa kaka angu Relief!!!
 
Tafuta Mapene.... Acha Kelele.
For the record Jeff Bezos aliachana na mkewe, Elon Musk aliachana na mpenzi wake wa mwanzo, Two richest men in the world right now. Boss Roman Abramovich na visima vyake alitaka kuachwa na mkewe ila akabembeleza sana baada ya kusikia wanagawana mali. Njoo Bongo Reginald Mengi aliachana na mkewe. Zari aliachana na Ivan. Mifano ni mingi mno hao ni watu maarufu 2. Kwahyo allow me to say kusema mapenzi pesa ni ulimbukeni unless umaanishe mapenzi biashara. Infact I have got money to afford many women in Tanzania that's why nlichangia vile.
 
Jaman mambo yakuwa romantic tuwachie wahindi huko sisi wabongo hebu tuvumiliane jaman maisha yenyewe magumu bado tena uwe romantic aaaaaahhhh
 
Mi nilishajaribu kuwa romantic nikashindwa kwanza naona ni umama

Demu akiniambia I love you mi namjibu "barid mamb yanaendaje"
Akiniambia I miss you mi namjibu "sawa poa"
Akiniambia naskia baridi namjibu "jifunike mashuka"
na akijidai ananipenda sana naona ananiigizia tu sipend kila saa aniletee mambo ya kuniambia ana nimiss au ananipenda akiyazidisha tu napunguza kumpenda naona ananiigizia

Kuna mmoja nilimuacha kwasababu ya maswali ya kipuuzi eti baby umekula? Umelala? Nikaona huyu ananiletea utoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…