Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Habari Kaka, mimi ni Binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba wangu. Huyu Kaka nilikaa naye kwenye mahusiano kwa miaka mittano. Lakini alianza kubadilika ghafla mpaka akampa mwanamke mwingine ujauzito wakawa wanaishi naye. Alishanitambulisha mpaka kwao lakini baada ya kumpa huyo dada ujauzito aliniambia kuwa wazazi wake hawanitaki kwakua hawana uhakika kama nina kizazi au la hivyo wamemuambia kuwa amuoe huyo mwanamke mwingine.

Nilimuambia nimbebe mimba yake akagoma na kuniambia tuendelee kuwa marafiki tu lakini suala la ndoa haliwezekanai. Niliumia sana akawa anakuja kwangu ila anaishi kwa ule mwanamke mpaka alipojifungua. Baada ya kuanza kukusoma niliona kama ananipotezea muda hivyo niliamua kuchana naye. kuna Kaka alikua ananitongoza nikaamua kumkubalia na tukaanza mahusiano, huyo Kaka alikua siriasi kwani baada ya miezi minne tu alikuja kujitambulisha kwetu, akatoa mahari na mipango ya ndoa ilianza.

Baada ya kuona kuwa naolewa X wangu alinitafuta, aliomba tuonane na mimi kwakukua nilikua na mtu wangu basi nilikubali. Huko alianza kunielezea matatizo na mwanamke wake, aliniambia kwanza ni mchafu, mchotyo, hapendi ndugu zake na anafikiria kumuacha kwani Mama yake hamtaki tena anatamania angenioa mimi. Tuliongea mengi sana lakini sikumsikiliza, ila alianza kuomba msamaha, akawa anatuma mpaka na rafiki zake.

Kwakua ni mtu ambaye nilikua nampenda nilijikuta kuwa narudi wkake, nikajikuta sina hamu tena na mchumba wangu na mwisho nikaamua kumuambia mchumba wangu mpya kuwa tuliharakisha lakini mimi simpendi hivyo nataka tuachane. Alilia sana akaumia kw2ani alidai nimemuaibisha kwao kwakua kila kitu kilishaandaliwa ila sikua na namna, niliona hakuna haja ya kuingia kwenye ndoa na mwanaume ambaye simpendi wakati mtu ninayempenda amerudi.

Ndugu zangu walinisihi sana nisimuache lakini nilishafanya maamuzi. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, baada ya kuchana na mchumba wangu huyu mwanaume alinishawishi kubeba mimba yake ili iwe rtahisi yeye kunitambulisha kwa wazazi wake kwani hawawezi kunikubali kama hawajui kuwa nazaa. Nilibeba mimba yake kweli na sasa hivi nina ujauzito wa miezi nane ila kuna mambo yamebadilika Kaka naomba unisaidie kwani nimechanganyikiwa.

Kwanza bado anaishi na X wake, mwanzo aliniambia kuwa wanaishi pamoja kwasababu ya mtoto ila yeye hana mapenzi naye kwani hata tendo la ndoa hawafanyi. Lakini Kaka mimi mimba yangu ina miezi nane nimechunguza nimegundua kuwa kumbe hata huyo mwanamke naye ana mimba ya mtoto wa pili. Kumbuka aliniambia wanalea tu mtoto, sasa Kaka namuuliza kwanini amempa ujauzito ananiambia ilikua ni bahati mbaya.

Anadai kuna siku alirudi nyumbani kalewa ndiyo mwanamke akammbaka na kumlazimisha kufanya naye mapenzi lakini yeye hamtaki. Tuligombana sana nikamuambia kuwa amuache huyo mwanamke, basi siku iliyofuata alichukua vitu vyake kwa huyo mwanamke na kuhamia kwangu. Aliniambia kuwa kaamua kumuacha mwanamke wake, lakini Kaka sio hivyo nimechunguza nimegundua kuwa kule kwa yule mwanamke kamuaga kuwa anasafiri kikazi na wala hajamuambia kuhusu mimi.

Nimemuambia si nina mimba basi anipeleke kwao kunitambulisha ananizungusha ananiambia kuwa Mama yake sasa hivi ana presha kwahiyo tutamchanganya tusubiri mpaka apone ndiyo anipeleke. Kaka naomba nisaidie, mwanuame kaja anaishi kwangu, ana kazi nzuri lakini hatoi chochote, kila kitu nahudumia mimi, yaani hata umeme ukikatika hawezi kununua. Kifurushi cha Azam kikiisha basi kama kuna mpira atanunua cha wiki nisiponunua ila ndiyo basi, naomba nisaidie kuna mapenzi kweli hapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona unakopi kwa idd makengo??[emoji849][emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuvaa suti kidume mtoto ndani ya shela kuna raha yake.
Hapa unapata baraka zote za wazazi na pia ndoa yenu inakuwa ina nguvu fulani,
Ila pia unawaheshimisha wazazi wako
na kujivunia kuwa na wewe.

Ila hii sogea tukae haijakaa sawa kabsa.
Inashusha thamani ya ndoa na wanandoa pia.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mnafunga ndoa baada ya miezi 7 mnatengana,ndio raha unayoisemea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja amchakaze akili ikae Sawa.
Huyo bwana na familia yake kuna jambo ambalo wanalificha. Wanataka bidada ajipeleke kwao ili hata siri ikija kufichuka: tayari bidada amezama +mimba au watoto; so asiwe na option ya kutoka.

In short kwa bwana huyo ndoa hakuna; bidada akiamua kujipeleka ajipeleke tu; ila asije akaishia kupata kichaa cha ndoa kwa kumuuliza bwana ni lini wataenda kujitambulisha. Hapo soon atapewa na sharti la kubeba mimba ili ndo wakajitambulishe vizuri; akija kushtuka tayari watoto wawili/watatu; bwana hana mpango wa kujitambulisha; kutoka hawezi, kukaa anaona hapaeleweki. Kichaa cha ndoa hiki hapa
 
Wakuu kuna jambo linanitatiza.
Nimekuwa na mahusiano kwa miaka miwili sasa huyu mwenzangu anataka tuchukuane kimya kimya (sogea tuishi) pasipo ndoa rasmi. Anaeleza kuwa baada ya mimi kwenda kwake wazazi wake waende nyumbani kwetu kutoa taarifa kuwa nimeolewa!

Kwa upande wangu nimejaribu kumueleza kuwa siyo jambo la busara mimi kufanya hivyo nahofia wazazi wangu kusononeka (nitakosa baraka za wazazi)

Nimejaribu kumweleza tutambulishane rasmi tufunge ndoa simple tu isiyokuwa na shamrashamra ila amekuwa mgumu kuelewa.

Ameamua kuniacha kisa nimekataa kuolewa kimyakimya pasipo kuwaeleza wazazi kuwa nimepata mchumba.

Bado nampenda sana nifanyeje ili tuweze kufikia suluhu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda mkaishi mwambie akatoe kishika uchumba kinatosha sana,
 
Au ana wasiwasi wazazi wake hawatakukubali?[emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana. Ndugu wa mwanaume wapo pamoja na kijana wao; amchukue tu mdada kimya kimya kwanza. Mabwaku....
Hili ni kweli ndugu zake wanashauri nikubali kuolewa bila kufuata utaratibu hata kama wazazi wangu watasononeka sitarudi tena kwetu kwa sababu nitakuwa tayari nimeshaolewa
Hili jambo halikuniingia akilini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom