Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda hilo la kwanza mkuu, la pili hapana.Labda ulipenda sana kuliko yeye alivokupenda.
Au kapata mwanaume zaidi yako.
ndivyo ilivyo alikuwa mguu mmoja nje mwingine ndaniInavyoonekana huyu kashafanya uamuzi mkuu.
Dah!! Ila JF kuna mambo!!!Karbu kubet kijana hakik utasahau maumivu yakipuuzi haya mpe Chelsea goli mbili tukutane jion
🤠🤠🤠🤠🤠🤠🤠🤠🤠!Walimu nasi tumekengeuka,sa itakuwaje?🤔
Itakua kampata anayempelekea moto zaidi yakeSijasahau bhana ulileta Uzi jinsi unavyomgegeda mwanamke wako mpaka anafurahi, sasa naona umeandikwa umeachwa, aisee wanawake....
Sijui wanataka nini?
Nashukuru sana mkuu.Thats life mkuu piga moyo konde na maisha lazima yaendeleee!!
Pole sana.
una haki ya kujua sababuHatujawahi, hali ilikuwa ni shwari kabisa, upepo ukabadilika ghafla.
Nitafute mkuuThats life mkuu piga moyo konde na maisha lazima yaendeleee!!
Pole sana.
Nitazingatia ushauri wako mkuu.Sawa kam unampenda sana jaribu kumtumia mshenga kwaajili ya maridhiano akikataa achana nae unasafari ndefu atakusunbua
Sure. Time is the best answer!Nashukuru sana mkuu.
Najitahidi mno kumsahau, ni swala la muda tu.
Ukiachilia mbali ualimu wake wa Shule ya Msingi, ana sifa zote za mama wa familia kwa upande wangu.Mwalimu wa shule ya msingi and you're crying! Anyways, kumbuka kufanya maintenance ya gari mara Kwa mara. Siku njema mkuu!
Najua mkuu, Pole sana muda ni daktari mzuri. Kupitie Nondo za Dizasta utakua sawa.We acha tu mkuu..inauma.
Needy is an attraction killer.Maisha ni lazima yaendelee.
Nakiri kwamba nilikuwa malaya sana zamani lakini nikaamua kubadilika baada ya kugundua kwamba mahusiano mengi kwa wakati mmoja yanapoteza muda, rasilimali fedha, yanadhoofisha mwili, akili n.k.
Nimekuwa kwenye mahusiano serious kwa takribani mwaka na nusu na Mwl mmoja wa Shule ya msingi. Mpole, msikivu, mcha Mungu, mnyenyekevu, sio mbinafsi, mshauri mzuri na zaidi ya yote amekuwa mfano bora wa mama wa familia. Nikaamua kumpenda kwa dhati. Nikawaambia hadi ma-x wangu. Nikawa najiachia nae, nikamtambulisha kwa baadhi ya wana.
Nikakaa kitako na Baba nipeleke barua ya posa, binti akaridhia. Barua ikaandikwa, mwanangu mmoja ambaye ameshaoa akakubali kuwa mshenga. Barua ilikuwa ipelekwe tangu j5 ya wiki iliyopita ila nikapata dharura tukaahirisha. Ilikuwa baada ya kupeleka posa ndio nikamtambulishe home.
J'mosi ya juzi akaanza kubadilika kuanzia kwenye mawasiliano na kila kitu. Jana nampigia simu aniambie barua tupeleke lini, akashtuka kama hajui kinachoendelea! Akajibu nisubiri kwanza, mara anaomba tupeane muda kuna mambo ajiridhishe!
Nikajiongeza, nikamwambia muda siwezi kumpa kwasababu tulishalizungumza hili. Aseme tu kama anadhani hatuwezi kuwa pamoja tena nitamuelewa. Akasisitiza nimpe muda! Nikamjaribu kwa kumwambia tuachane ili tusipotezeane muda (kumbuka hapa nilikuwa namjaribu); ili nione anawaza nini.
Lahaulaa, akasema 'SAWA'. Nikaishiwa nguvu. Nilikuwa barabarani nikasimama kwanza kwasababu nilipatwa na wenge nikahisi naweza kusababisha ajali.
Ina maana ile kupenana muda ilikuwa ni gia tu, alishaamua tuachane. Sikumtafuta tena tangu jana na yeye kakaa kimya mpaka muda huu!
Huyu ni msichana aliyeniaminisha kwamba hawezi kuniacha. Kwamba hata nikijaribu kumuacha atafanya jambo baya (ni kama alikuwa anatishia kujiua).
LAWAMA ZANGU ZOTE NAZIELEKEZA KWA RAFIKI YAKE MWENYE JINA LINALOANZA NA HERUFI 'J', ANAYEISHI MKOA UNAOANZA NA HERUFI 'M'. Mpenzi wangu alikuwa anamsikiliza sana, na mara nyingi wamekuwa wakiniongelea, nina kila sababu ya kuamini kwamba ushauri wake umechangia kumfanya mwanamke wangu afikie uamuzi huu. Huyu dada yeye kaolewa, leo kaamua kumfanyia figisu rafiki yake! We dada wewee....
Biblia imesema tushukuru kwa kila jambo. Pengine kuna jambo Mungu ameniepusha nalo. Naumia ila najikaza.