Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

332d39909d10c02b661637063654fb2d.jpg
 
Haya ni maelezo ya upande mmoja. Ni ngumu kutoa hukumu katika huu muktadha.

Kabla sijaenda mbali, hiyo wewe unaiita kumjaribu, kumbuka hakujua kama una mjaribu au unamaanisha, ulitaka Binti wa watu apokee namna Gani hizo taarifa?

Kumbuka uliahirisha kwenda kupeleka mahari, haujasema sababu ipi ilitokea na hiyo taarifa uliiwasilishaje upande wa wakwe.

Kama kweli unamhiraji na una maanisha, naamini unaweza kurekebisha makosa Yako mkayajenga.

Utatoa melezo Gani kwamba ulikua unamjaribu? Kwa sababu zipi na malengo Gani?
Uko sahihi hapo uliposema kwamba haya ni maelezo yangu, hamjajua maelezo yake.

Lakini trust me, niliahirisha kupeleka posa kwasababu ambayo ilikuwa justifiable, na wakwe walinielewa.

Nilimjaribu ili kujua anawaza nini, mwanamke ambaye ananipenda na ana lengo la kutengeneza familia na mimi asingekubali tuachane kirahisi vile mkuu.
 
Pole mkuu nadhani huyo rafike yake anajua stories zako za huko nyuma maana umekiri wewe mwenyewe kwamba ulikuwa kiwembe hawa wenzetu wakishapata stories zako mbili tatu hata kama umeshabadilika huwa hawanaga kupembua chuya na mchele.
Kabla sijaanza nae mahusiano nilishamuelezea historia ya maisha yangu na akakubali kunipokea hivyohivyo, akasema tusahau yaliyopita tugange yajayo kwasababu hata yeye alikuwa na past life yake ingawa haikuwa mbaya kama yangu.
 
Back
Top Bottom