Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Pole Mkuu Amicus Curiae huwa naelewa sana falsafa zifuatazo katika mahusiano.

1. Ni makosa makubwa mwanamke kufahamu kuwa bila yeye mambo yako yatakwqma, hakika mwanamke akilijua hilo lazima akusumbue tu.

2. Hii inabebana na iyo ya kwanza, kamwe mwanaume haupaswi kujishusha mbele ya mwanamke hasa mwanamke uliye naye kwenye mahusiano. Huna sababu ya kujieleza kwa jambo lolote kwake. Ila muhimu wewe muheshimu tu na mipaka izingatiwe.

3. Usimuombe mwanamke kumuoa wewe fanya mambo yako hadi siku yeye atakapoomba wewe umuoe na kamwe usikubali akuendeshe au kukulazimisha kumuoa

Sasa Mkuu huyu mwanamke alijua bila yeye mambo yako hayataenda, huyo usihangaike naye kabisa funga ukurasa focus kwenye mambo mengine.

Pole sana Mkuu Amicus Curiae
 
Dada kapindua meza, pole mwamba. Hapo kashapata option nyingine anayoamini ndio sahihi.

Vuta subira kidogo, muda huwa hausemi uongo, utajua kila kitu kwa undani wake.
 
Pole sana...

IT’S DIFFICULT”.
Hii ni layer ambayo kama si mvumilivu, safari yako inaweza kuishia hapa, lakini kwa wanaokomaa hujiambia, “ni ngumu lakini nitajaribu”. Ctrl + C
 
Mkuu, nakushukuru sana kwa busara hizi.

Hakika umeuponya moyo wangu kwa sehemu. Nimeamini watu wema bado mpo, wengine wananifanyia mizaha tu humu.

Nimeamua kumuacha aende, najitahidi kutomnung'unikia pia. Mungu anajua dhamira yangu kwake, kwamba ilikuwa ni njema sana.
 
Bora Huyo alokwambia live unajua na kushika 50 zako .. kuna miamba inaacha kimya kimya no calls no sms no o anything mwisho wa siku ujiongeze mwenyewe tu kuwa nishaachwa. !
Mapenzi ni Hekaheka mkuu Mungu akuponye majeraha yako haraka!
Asante sana mkuu. Nakushukuru mno. Sasa naamini kwamba watu wema bado mpo JF, wengine wanaishia kunifanyia mizaha tu humu.
 
Pole sana,tunda limeponyoka kimasihara🤩🤩🤩
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…