Nimeagiza mzigo wangu wa kwanza China kodi niliyokadiliwa na TRA ni kubwa mno je nawezaje kuomba kupunguziwa wakuu nishaurini nimechanganyikiwa

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Habari zenu wakuu..

Wakuu nisaidieni namna ya kupunguza kodi tra huko maana kwa kodi hii niliyoletea mawiwili either nipate hasara au niususe mzigo bandarini hapo hapo.

Nafahamu huku JF kuna wataalamu wa haya manbo naombeni msaada wenu

Ombi langu kama kuna njia kusaidia kodi ipungue nitashukuru kwa michango na ushauri wenu.
 
Wakuu nisaidieni namna ya kupunguza kodi tra huko maana kwa kodi hii niliyoletea mawiwili either nipate hasara au niususe mzigo bandarini hapo hapo.

Ombi langu kama kuna njia kusaidia kodi ipungue nitashukuru kwa michango na ushauri wenu.
Sasa ndugu yngu uliagizaje mzigo bila kuzingatia hivyo vitu?

Humu kuna mtu anaitwa Mwl.RCT (hope sijakosea.) naamin ukimpata atakusaidia , huyu jamaa ni mtaalamu sana wa masuala hayo , tena ana uzi wake wa biashara hiyo. Ngoja nicheki link niweke.

----------
Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu umeagiza peni china moja inauzwa shilingi kumi ikifika Bongo kodi shilingi mia hapo ndio utajua Bongo nyoso

CC Zero IQ
 
Lazima ijulikane base iliyotumika kufanya hiyo Tax assessment ili ku I challenge

Pengine Wewe ndio umeshusha bei uliyonunulia huko ili upate unafuu wa kodi
 
Ndiyo kuna namna unayoweza fanikisha kupunguziwa kodi kama unahisi kodi unayochajiwa si sahihi.

Kwanza unatakiwa uandike malalamiko yako na kuyatuma ndani ya siku 30(kwanzia siku uliyofanyiwa makadirio ya kodi).
Ila hakikisha ile kodi unayohisi ulitakiwa kulipa umeilipa (siyo ile waliyokukadiria)

Wasipo kusikiliza utakata rufaa kupinga kodi unayochajiwa. Wasipokusikiliza utasonga mbele hadi mwisho wa siku Mtaenda hadi mahakamani.

Na court of appeal ndiyo maamuzi ya mwisho yatatolewa.
Ukitaka namna na mahali pakuanzia niambie.

Ila kama unahisi ni kodi sahihi wewe lipa tuu . Hata kama ni kubwa.

USHAURI.
Kabla haujaagiza kitu nje ya nchi, fanya research ujue kabisa utaki import kwa gharama gani. Tena hususani kwa bidhaa ambazo zina patikana Tanzania (zinazalishwa Tanzania pia). Maana ukiziingiza kwa bei ndogo viwanda vyetu vitakufa.


The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
 
Yes unaweza kupatiwa punguzo la kodi ya mzigo wako.

Juzi nimenunua iPhone 7 toka Atlanta USA custom wakanibambikia kodi almost laki na ishirini.

Nilifanikiwa kufanya bargain wakanipunguzia kidogo

Hizi kodi si rafiki kabisa jitahidi kuongea nao vizuri
 
Aaante sana.
 
Mkuu funguka umeagiza nini na ulitarajia kodi iweje na uchachajiwaje ili watu wenye field ya ulichoagiza wakwambie abcd zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe wewe wewe heeeeeeeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante je kuna ofisi maalum hapo tra inayodeal na hizi bargain za kodi, walikupunguzia tsh. Ngapi.

Na mwisho mimi nimetumia agents wa clearance Ndio nimepeleka details za mzigo maana upo njiani kuja baada ya kuwapa wameweka kwenye system ya tra ndio nikaambiwa kodi ninayotakiwa kutoa.
 
Mambo? Cute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…