Ndiyo kuna namna unayoweza fanikisha kupunguziwa kodi kama unahisi kodi unayochajiwa si sahihi.
Kwanza unatakiwa uandike malalamiko yako na kuyatuma ndani ya siku 30(kwanzia siku uliyofanyiwa makadirio ya kodi).
Ila hakikisha ile kodi unayohisi ulitakiwa kulipa umeilipa (siyo ile waliyokukadiria)
Wasipo kusikiliza utakata rufaa kupinga kodi unayochajiwa. Wasipokusikiliza utasonga mbele hadi mwisho wa siku Mtaenda hadi mahakamani.
Na court of appeal ndiyo maamuzi ya mwisho yatatolewa.
Ukitaka namna na mahali pakuanzia niambie.
Ila kama unahisi ni kodi sahihi wewe lipa tuu . Hata kama ni kubwa.
USHAURI.
Kabla haujaagiza kitu nje ya nchi, fanya research ujue kabisa utaki import kwa gharama gani. Tena hususani kwa bidhaa ambazo zina patikana Tanzania (zinazalishwa Tanzania pia). Maana ukiziingiza kwa bei ndogo viwanda vyetu vitakufa.
The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.