Nimeahirisha kuoa.

Nimeahirisha kuoa.

Hela ninayo ya kutosha mahitaji ya kila cku, shule ninayo graduate, nafanya kazi, Si mlevi, usafi naujua kwa ujumla, ni mrefu c mfupi. Kanisani kwa sana. Pafomansi niko vizuri. Nina afya njema, si mropokaji,

Dah..! Sifa zote hizi ndugu umekimbiwa?? Mmmh..!!
 
Ndugu wapendwa wa MMU, Nimeona niahirishe kuoa baada ya kukutana na wapenzi 2 humu jf tukakubaliana na suala zima la ndoa lakini mwisho wake wananitosa. Mmoja tulifikia hatua ya kwenda kutambulisha dakika za mwisho akaingia mitini. Wa pili tulifikia hatua ya kuonana tufahamiane baada ya kuafikiana kila kitu kwenye mawasiliano nae akazamia kusikojulikana. Haikuishia hapo, mwingine nikakutana nae kanisani tukaweka mambo sawa mwezi sasa umepita kakata mawasiliano. Anadai suala la kuolewa halipo tena kwenye akili yake. Kwangu mimi umri unasogea lakini nimeona tu bora niahirishe kuoa niendelee na maisha ya peke yangu kama kawaida kuliko kuendelea kudanganywa na hawa wanawake. Kama kuna ushauri nipeni waungwana.
Cha msingi ni kwamba 'don't lose your hustle for fcking broad', works fine with me/
 
Jomba wapanga kuahirisha wakati wamekuahirishia? Pole jipe moyo.
 
Mimi naomba usiache kuoa mm niko nahitaji watu kama nyie mlokata tamaa,niko serious kama utanikubali.am 42yrs old
 
Hela ninayo ya kutosha mahitaji ya kila cku, shule ninayo graduate, nafanya kazi, Si mlevi, usafi naujua kwa ujumla, ni mrefu c mfupi. Kanisani kwa sana. Pafomansi niko vizuri. Nina afya njema, si mropokaji,

dahhhhhhh
hata mi ningekimbia..

we ni Mr. Perfect.
 
Hela ninayo ya kutosha mahitaji ya kila cku, shule ninayo graduate, nafanya kazi, Si mlevi, usafi naujua kwa ujumla, ni mrefu c mfupi. Kanisani kwa sana. Pafomansi niko vizuri. Nina afya njema, si mropokaji,

Huna sifa moja kubwa sana nayo ni uongo . Ukiwa mtu wa fix unaweza mkupata mtoto mkali . Madem always wanapenda kudanganywa.
 
Single life ndo dili sa hvi!achana na habari ya kuoa!make money kijana!Ndoa siyo issue!heshima pesa!ukiwa nazo watakuja wenyewe.
 
usikate tamaa. Yupo wa kwako wa u abavu wako. Trust in God.
 
Labda unatafuta watu sio type yako, jaribu kwenda kwenye nyumba za Ibada huko
 
pole sana,kila mtu kaumbiwa wake,amini hivyo...kama hapa umekosa jaribu kwingine i mean njia nyingine kama huko mitaani kanisani etc hutokosa
 
Back
Top Bottom