Nimeambiwa moyo wangu umetanuka

Nimeambiwa moyo wangu umetanuka

kedekede

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
5,313
Reaction score
7,714
Salaam Doctors, na wana JF.

Niende kwenye tatizo.

Mnamo tarehe 31/12/2019 nikiwa kwenye kikao cha management chenye idadi ya watu sita pamoja na Mimi, kikao ambacho huwa kinakuwepo kila siku asubui saa mbili na mbali na mambo mengi kila mtu kuzungumzia idara yake kama manager ilipofika zamu yangu mtu wa tano kauli iligoma kutoka.

Nikarukwa akapewa nafasi mtu wa sita alipomaliza nikapewa nafasi tena lakini nikashindwa na hata nilipojilazimisha kuongea ni kama nilikuwa nimelewa na maneno kuyarudia rudia mara kadhaa kama mtu ambaye ameparalize.

Kabla ya hali hii sijawahi kuwa na tatizo hili.kila siku huwa mmoja wetu anatoa topic ya afya/usalama nakumbuka niliweza kumuuliza swali aliyekuwa anatoa topic.

Baada ya hayo kutokea na kikao kuisha nilinyanyuka lakini kwa kupepesuka sana kupita sehemu kwenda kwenye mess watu wanayokula kuwafikishia ujumbe staff wangu. Mguu wa kulia na mkono wa kulia nilikuwa kama naulazimisha ilikuwa hainipi support.

Nilifanikiwa kufika nilipokuwa naenda lakini Kwa taabu na kupepesuka. Wakati naenda kwenye kikao nilikiroga kahawa yangu light Kama kawaida ila niliweka maziwa kuifanya nyepesi zaidi.

Hapo awali Kama mwezi nyuma nilipima presha ikawa 139/90 nikamuhoji Dr akasema with my age of above 45 ni sawa.Nilijitahidi kuishusha kibinafsi mwisho Kama wiki mbili Kabla ya tatizo hili ilikuwa 122/70.

Nilisaidiwa kufikishwa clinic kwa kushikwa na watu.nilipimwa,pressure ilikuwa 153/81, PR 96beats/minute, Rr24/mn temp 37.3, mrt NegativeRBS5.7mmol/1 (clinic y'all kazini) walinipa aspirin).

Nilipelekwa hospital ya 'amtumbo nikatibiwa muda huo pressure ilikuwa 145/75. Waliniacha niwe karibu na huduma za matibabu japo sikulazwa.

01/01/2020 nikarudi kambini job nikafika jioni saa 12 nikiwa tu vizuri, lakini baada ya nusu saa hali ikawa mbaya sana nikarudishwa clinic ya kazini, lakini this time mkono na mguu vilikuwa stable. Lakini nikiwa siwezi kuongea na nikuongea nina rudia rudia ndio unielewe.

Nilifanyiwa vipimo tarehe hii ikawa Kama ifuatavyo, BP 178/116,PR91/minRR 22/min, Temp 37.1. Nilichomwa sindano1/m 10mg stat, dispensable aspirin 75mg stat. Nikapumzishwa clinic baadaye nikaruhusiwa kwenda chumbani.

Kesho yake nikapelekwa hopitali ya mkoa wa Ruvuma, nikapimwa BP 131/75.
Nikashauriwa nifanye kipimo cha ECG nikaambiwa moyo una shida lakini maelezo hayakuwa yamenyooka. Nilipewa dawa za kushusha presha aspirin.

Nilikaa songea siku mbili 02/01/2020 na 03/01/2020.maana shule zilikuwa zinafunguliwa. Nilisafiri jumamosi na kufika nyumbani Mkuranga. Jumapili nikapumzika, Jumatatu nikaenda hospital ya wilaya Mkuranga yaani Mkwalia.

Niliandikiwa kipimo cha ECHO ambacho nilifanya tarehe 09/01/2020 nikaambiwa msuli wa moyo umetanuka kidogo. Kipimo hiki nilifanyia St Monica darajani Manzese badala ya Temeke nilipoandikiwa maana kuna Dr bingwa moyo wa Muhimbili aliniandikia dawa.

Pia Niliandikiwa kufanya brain CT scan ambayo nilifanya pale hi-tech, sikukutwa na kitu, haya ni maelezo kwa kirefu tu. Nachanganyikiwa nikisoma kwenye internet je moyo unaweza kurudi Kwa Dawa? Inachukua muda gani?

Nawaomba mnipe ushauri kutokana na matatizo haya. Mara nyingi naumwa na kichwa hadi sasa kinaniuma.
 
Wakati ukisubiri majibu ya Dr's sisi wa tiba mbadala tunakushauri kwenye hbr ya menu punguza vyakula vyenye mafuta mengi, punguza kiasi cha chumvi na sukari, punguza vilevi kama unatumia,

anza mazoezi kama ulikuwa hufanyi, ikiwezekana nyama nyekundu pia upunguze, kula sana nyanya, matunda na mboga za majani, maji kwa wingi lakini pia kaa sehemu yenye hewa ya kutosha afya yako itaanza kuimarika.
 
Pole sana kiongozi
Madokta watakuja kutoa mwongozo.

GOD is GOOD
 
Unaambiwa Usipende mtu zaidi ya mmoja ..sasa wewe kila binti unamuweka moyoni,,ndo madhara yake ayo sasa
 
Pole kaka yangu,
Kwa maelezo yako ulipata TIA (Transient Ischaemic Attack) au minor stroke. TIA inaweza kuwa noticed au unnoticed ila mwili unakuwa kwenye hatari ya kupata 2nd attack katika muda wa masaa 72.
Tiba/Ushauri?
 
Back
Top Bottom