Nimeambiwa moyo wangu umetanuka

Nimeambiwa moyo wangu umetanuka

Mama yangu mdogo alishawahi kupata hili tatizo nakumbuka Ni miaka ya 2006 2007.
Alitumia dawa za hospital pia alizingatia kanuni za lishe..
Kwa Sasa anaendelea vizuri..tatizo halijaisha kabisa Ila n kidogo Sana.

Huwa anatumia pia vitunguu saumu..
Anatafuna au kumeza kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu napata matumaini
 
Kwa maelezo mafupi uliyotoa inaonesha una heart failure. Kuanzia sasa achana na mambo ya kahawa and the like.

Pia inawezekana una hypertension[pressure kupanda].

Haya matatizo ya moyo na pressure yakishaanzaga huwa hamna kurudi nyuma kimatibabu. Kama umeanza dawa ndio hamna tena kuacha.

Jitahidi kuzingatia maelekezo ya madaktari naamini utakuwa vizuri tuu.


Unforgetable
 
Pole sana.Jamaa zangu wawili pia walipata shida hi. Mdomo kwenda upande,mkono na mguu kuparalise. walienda hospital ila baadae walipona kwa tiba mbadala. Jaribu usikate tamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujanja ujanja..kwa nini usimtibie humu kwa kumuambia cha kufanya.. tamaa ya pesa inafanya jamiiforums ionekane taasisi ya utapeli.. why hutaki mshauri chochote.. unaweka namba za simu tu.. halafu umdanganye wewe umwambie dawa milion 5 huku hata ofisi haipo MziziMkavu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kedekede ndio kwanza nagundua ulikuwa mgonjwa/ni mgonjwa.
Pole sana. Unaendeleaje sasa?
Again pole sana kwa unayopitia nitahidi sana kuwa imara. Yote yatapita.
 
pole sana
epuka mawazo nasisitiza
ishi kama vile huna tatizo
fanya mazoezi
epuka vyakula vyenye mafuta
epuka hasira za mara kwa mara
ukiweza hayo utakuwa umedhibiti tatizo kwa kiasi fulani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Close monitoring by medical personnel, aspirin in a higher dose eg 300mg a day can help to thin the blood and resolve the blockage. But hypertension can easily cause haemorrhage or blood vessels rapture while on aspirin ragime so doctors can priscribe ACE to manage hypertension while resolving the blockage.

1: Umeeleza kwa ufasaha juu ya kile kilichomtokea mwenzetu kikuu/tatizo Transiet Ischaemic Attack (TIA).
2: Matibabu yake kwa andiko hili hapa.
3: Ningenda kumuunga mkono pia yule alieandika juu ya kusitisha unywaji wa kahawa kwa husababisha moyo kwenda kasi na kutokuwa na mpangilio mzuri wa mapigo ya moyo.
4: Namuunga mkono yule aliyezungumzia lishe kwa kupunguza ulaji wa nyama nyekundu, maziwa, chumvi, mayai na wanga. Aongeze ulaji wa samaki, mboga za majani, matunda na protein za mimea. Haya yote unaweza kuyafanya vyema kwa kushauriana na daktari wako wa sasa.
5: Katika kufanya vipimo vya kutafuta chanzo, kuna issue ya Bp ambayo iko wazi, lakini sina uhakika kama ulifanya vipimo vya kuangalia kiasi cha mafuta na mgawanyo wake, ufanyaji kazi wa ini na figo. Hii yote ni kuangalia ni kwa jinsi gani hali hii ya presha inaweza kuwa imeleta madhara kwenye mwili. Lakini pia ningekushauri kuzingatia matibabu na kutokubadili au kuacha dawa yoyote pamoja na mfumo hapo juu wa maisha bila kushauriana na daktari hasa daktari bingwa wa moyo au wa magonjwa ya ndani.
6: Kuhusu mazoezi, ongea na daktari wako nae atakushauri kulingana na alivyoona uwezo wa moyo wako na mwili kwa ujumla.
7: Ukizinatia haya yote maisha yako uataendelea vyema na hiyo hali ya moyo kunenepa au kuwa mkubwa huweza kurudi vyema ikitegemea na nini hasa kilichoonekana kwa sasa.
8: Fahamu kuwa hii hali ya TIA huweza kujirudia kama usipozingatia taratibu na hii waingereza wanaita ni Warning sign ya kiharusi kama isipozingatiwa vyema.

Nimeona niyaweke yote pamoja ili iwe rahisi kwako kufuatilia.

Ahsante.

Pole na matibabu mema.
 
Back
Top Bottom