Close monitoring by medical personnel, aspirin in a higher dose eg 300mg a day can help to thin the blood and resolve the blockage. But hypertension can easily cause haemorrhage or blood vessels rapture while on aspirin ragime so doctors can priscribe ACE to manage hypertension while resolving the blockage.
1: Umeeleza kwa ufasaha juu ya kile kilichomtokea mwenzetu kikuu/tatizo Transiet Ischaemic Attack (TIA).
2: Matibabu yake kwa andiko hili hapa.
3: Ningenda kumuunga mkono pia yule alieandika juu ya kusitisha unywaji wa kahawa kwa husababisha moyo kwenda kasi na kutokuwa na mpangilio mzuri wa mapigo ya moyo.
4: Namuunga mkono yule aliyezungumzia lishe kwa kupunguza ulaji wa nyama nyekundu, maziwa, chumvi, mayai na wanga. Aongeze ulaji wa samaki, mboga za majani, matunda na protein za mimea. Haya yote unaweza kuyafanya vyema kwa kushauriana na daktari wako wa sasa.
5: Katika kufanya vipimo vya kutafuta chanzo, kuna issue ya Bp ambayo iko wazi, lakini sina uhakika kama ulifanya vipimo vya kuangalia kiasi cha mafuta na mgawanyo wake, ufanyaji kazi wa ini na figo. Hii yote ni kuangalia ni kwa jinsi gani hali hii ya presha inaweza kuwa imeleta madhara kwenye mwili. Lakini pia ningekushauri kuzingatia matibabu na kutokubadili au kuacha dawa yoyote pamoja na mfumo hapo juu wa maisha bila kushauriana na daktari hasa daktari bingwa wa moyo au wa magonjwa ya ndani.
6: Kuhusu mazoezi, ongea na daktari wako nae atakushauri kulingana na alivyoona uwezo wa moyo wako na mwili kwa ujumla.
7: Ukizinatia haya yote maisha yako uataendelea vyema na hiyo hali ya moyo kunenepa au kuwa mkubwa huweza kurudi vyema ikitegemea na nini hasa kilichoonekana kwa sasa.
8: Fahamu kuwa hii hali ya TIA huweza kujirudia kama usipozingatia taratibu na hii waingereza wanaita ni Warning sign ya kiharusi kama isipozingatiwa vyema.
Nimeona niyaweke yote pamoja ili iwe rahisi kwako kufuatilia.
Ahsante.
Pole na matibabu mema.