Nimeambiwa na madaktari sina uwezo wa kuzaa (mbegu hazina nguvu)

Nimeambiwa na madaktari sina uwezo wa kuzaa (mbegu hazina nguvu)

kwani wewe hujui michael jackson watoto wake aliwapataje?embu jaribu kuzi plant hizo mbegu zako kwa mkeo mbona hiyo ishu ndogo sana kama kumsukuma mlevi,alafu hao madaktari nao ni feki kwani hawakukupa alternative?
 
Nenda ukaombewe kwasababu muujiza wa kupata mtoto unatokea kirahisi sana, kwasababu ni agizo la Mungu watu kuzaa na kuongezeka. Amini katika sala utampata mtoto mapema sana.
 
Mimi ni kijana niliyeoa, niko kwenye ndoa sasa kwa miaka tisa (9) sijapata mtoto; vipimo vinaonyesha mke wangu hana tatizo lolote kwenye uzazi-ila tatizo ninalo mimi; nimeambiwa mbegu zinazozalishwa kwangu ni chache, pili hazina uteute utaozifanya ziteleze na kuweza kulifikia yai. Madaktari wanasema hakuna dawa ya kurekebisha hiyo kwani "production site ya viscosity is deady" Ila chakushangaza nina uwezo mkubwa wa kufanya tendo la ndoa hata mara tano kwa siku na zinatoka vizuri; na zilipimwa ni nzima kabisa tatizo ndio hilo "Uchache na no viscosity" Naombeni ushauri nifanyeje????????

Kwanza karibu sana jamvini.
Jaribu kuwaona madakatari bingwa zaidi ya mmoja na uweze kupata ushauri zaidi. Nadhani huo ushauri uliotolewa na dr. Riwa unafaa sana kufanyiwa kazi.
 
Last edited by a moderator:
pole sana mkuu kwa muda wa miaka 9 huna mtoto!
ila ningekuwa mimi wala nisingehangaika nimepunguziwa matatizo tu kizazi chenyewe hiki:
1.watoto wa kike wanajua mambo bado wadogo!
2.mtoto wa kiume unampa hela akasome yeye ananunua kondom
3.watoto wa kike umalaya na utoaji mimba ovyo hata kama unampa kila kitu!
4.watoto wa kiume ndo ushoga unawaandama!

wewe umeangukia kundi gani hapo?
 
Ndugu yangu, umeuliza tu ufanyaje lakini hujasema unachohitaji - unahitaji kupona tatizo au unahitaji kupata mtoto ndio unauliza ufanyaje?

Kama ni kweli madaktari wamethibitisha unatoa mbegu chache na zisizo na ute, na kwamba ni kwa sababu 'production site' is dead...nadhani kupona hilo tatizo itakuwa ngumu, au utafute msaada nje ya nchi.

Lakini kama unahitaji tu watoto...nadhani In-Vitro Fertilization (IVF) inaweza kukusaidia. IVF inahitaji tu uwe na uwezo wa kuzalisha mbegu zikakomaa, basi hizo zitavunwa na kurutubisha yai toka kwa mkeo, kisha linandwa kwenye kizazi na mimba inatunga na kukua kama kawaida, na mkeo anajifungua. Mnaweza zaa watoto kadhaa tu kwa njia hii, na wala haikuhitaji uende nje, kwani hii procedure inafanyika hapa Bongo.

Ndugu Riwa naomba kupata ufafanuzi wa hili suala la viscosity ya mbegu.. kuna watu wamewahi kuweka hapa jamvini confession za baadhi ya wanawake kupata mimba 'eti kwa kijifutia' taulo lililotumiwa na mwanaume guest/hotelini na wakapata mimba! Sasa najiuliza kama hilo linawezekana kwenye taulo kavu inakuwaje kwa hizi mbegu hata kama ute ni kidogo zisitungishe mimba!? Au la sivyo nashindwa kuamini huo ushuhuda wa baadhi ya ndugu hapa jf.
 
Mkuu naomba nikuulize kaswali. Ina maana ww hutaoa na kupata watoto kwa sababu hizi ulizozitaja hapa?

nitaoa na mungu akipenda nitazalisha watoto wawili tu sitaki timu ya mpira!
tangu utotoni mwanangu nitachunguza ana mwelekeo gani? nikiona simwelewi hata sipotezi hela zangu wala energy yangu kwa ajili yake!!!
 
Pole sana mkuu maana hayo matatizo yameshazoeleka kwa Wanawake tu kuwa wagumba ila sio kwa Mwanaume kuwa Tasa,,,Pole sana Mkuu maana Fahari ya ndoa ni watoto.
 
Mbulula ni mbulula daktari katoa hitimisho ss tufanyeje ambao si wataalamu labda unialile nimpe mimba mkeo tena atazaa dume!
Mimi ni kijana niliyeoa, niko kwenye ndoa sasa kwa miaka tisa (9) sijapata mtoto; vipimo vinaonyesha mke wangu hana tatizo lolote kwenye uzazi-ila tatizo ninalo mimi; nimeambiwa mbegu zinazozalishwa kwangu ni chache, pili hazina uteute utaozifanya ziteleze na kuweza kulifikia yai. Madaktari wanasema hakuna dawa ya kurekebisha hiyo kwani "production site ya viscosity is deady" Ila chakushangaza nina uwezo mkubwa wa kufanya tendo la ndoa hata mara tano kwa siku na zinatoka vizuri; na zilipimwa ni nzima kabisa tatizo ndio hilo "Uchache na no viscosity" Naombeni ushauri nifanyeje????????
 
Pole sana,cha msingi pitisha ata wiki ili mbegu ziwezekuwa nyingi na zenye nguvu pia mwombe sana mungu hakuna lisilowezekana atakupa mtoto siku ikifika,JIPE IMANI UTAFANIKISHA.MUNGU AKUBARIKI

Unaambiwa mahali pa kuzalishia pameingia ruba sasa hizo mbegu zitazalishwaje au ndio kutiana moyo
 
Nashukuru kwa maoni mazuri ya wana JF hapo juu.Kama hutojali jitahidi kupata annointed water toka kwa T.B Joshua.
 
umesahau kumwambia kuwa hiyo ni probability na anaweza kufanya/kujaribu zaidi ya moja kisha akafanikiwa au asifanikiwe.

Kumbe na wewe ni kadaktari.

Ngoja nikupm.
 
Ndugu yangu, umeuliza tu ufanyaje lakini hujasema unachohitaji - unahitaji kupona tatizo au unahitaji kupata mtoto ndio unauliza ufanyaje?

Kama ni kweli madaktari wamethibitisha unatoa mbegu chache na zisizo na ute, na kwamba ni kwa sababu 'production site' is dead...nadhani kupona hilo tatizo itakuwa ngumu, au utafute msaada nje ya nchi.

Lakini kama unahitaji tu watoto...nadhani In-Vitro Fertilization (IVF) inaweza kukusaidia. IVF inahitaji tu uwe na uwezo wa kuzalisha mbegu zikakomaa, basi hizo zitavunwa na kurutubisha yai toka kwa mkeo, kisha linandwa kwenye kizazi na mimba inatunga na kukua kama kawaida, na mkeo anajifungua. Mnaweza zaa watoto kadhaa tu kwa njia hii, na wala haikuhitaji uende nje, kwani hii procedure inafanyika hapa Bongo.

Fuata huu ushauri ni nzuri.andaa tu fungu la kutosha
 
Back
Top Bottom