NZURI PESA
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 5,958
- 2,954
Ndugu yangu, umeuliza tu ufanyaje lakini hujasema unachohitaji - unahitaji kupona tatizo au unahitaji kupata mtoto ndio unauliza ufanyaje?
Kama ni kweli madaktari wamethibitisha unatoa mbegu chache na zisizo na ute, na kwamba ni kwa sababu 'production site' is dead...nadhani kupona hilo tatizo itakuwa ngumu, au utafute msaada nje ya nchi.
Lakini kama unahitaji tu watoto...nadhani In-Vitro Fertilization (IVF) inaweza kukusaidia. IVF inahitaji tu uwe na uwezo wa kuzalisha mbegu zikakomaa, basi hizo zitavunwa na kurutubisha yai toka kwa mkeo, kisha linandwa kwenye kizazi na mimba inatunga na kukua kama kawaida, na mkeo anajifungua. Mnaweza zaa watoto kadhaa tu kwa njia hii, na wala haikuhitaji uende nje, kwani hii procedure inafanyika hapa Bongo.
Dokta wa ukweli nielekeze huduma hiyo hupatikana wapi nami naihitaji.Ahsante kwa maelezo yanayojitosheleza.