Nimeambiwa nimejifukuza kazi, nina haki ya kudai kisheria?

Nimeambiwa nimejifukuza kazi, nina haki ya kudai kisheria?

Kwa enzi hizi makazini, kama hutaacha mambo haya utapata shida.... umefanya vema kuuliza. Maana ungeacha kuuliza inamaana ungeendeleza malumbano nao wakati uliachakazi mwenyewe.Achana nao tafuta maisha mbele------ usihofu kwa kukosa ajira hapo, WANAUME WANAFIA NJE
 
Nilikuwa nafanya kazi kampuni flani ivi,

Nilivyoskia nafas za JKT nikatuma maombi nikaenda kwenye usaili takribani week nzima na nimepata kufaulu ngazi ya wilaya.

J3 naenda kazini HR ananiambia hauna kazi umejifukuzisha.

Naomba msaada wa mawazo na kama kuna haki ya kisheria ya kuwadai au wao wananidai naomba kujuzwa
Hapo huna chako..
 
Yani unaondoka kazni bila kuaga?asa huko jeshini utapaweza kweli ndugu?
 
Sheria ya kazi inasema kama mfanyakazi akiondoka bila taarifa mda wa siku tano mfululizo amejifukuzisha kazi mwenyewe kwa hiyo jamaa wako sahihi.
 
sikutoa taarifa mkuu .maana nlipigiwa cm ya gafla niende mkoani kwenye usaili kwamba kuna shortage huko ya form six
naomba kusaidiwa kama nna haki yoyote kujua hapo
Hapo huna kazi!!!
 
Wewe unaondoka kazini bila hata kutoa taarifa - hata kwa simu hukuweza kuwajulisha !! kweli maadili ya kazi bado
 
kampuni gani mbona jina uweki, unaweza kuwapata wazako waliotendewa hivyo kwenye hiyo kampun wakakusaidia
 
wiki haupo kazini unategemea nn? tena bila taarifa yoyote we mbabe kinoma ungekuwa hr ungejipa na mapumziko baada ya huo usaili.
 
Ulikiuka aisee, umejifire mwenyewe. Anyway JKT bado ni probabillity coz bado hujamaliza usaili, kuna vipimo, PT nk, ukifeli utasugua bench mtaani.
 
Hakuna kitu kinaitwa kujifukuzisha kazi wasikudanganye awa wapuuzi.

Either unaacha kwa hiari au wanakupa barua ya kukuachisha. Bado unatakiwa upewe mshahara wa mwezi mmoja na huyo mwajiri na barua ni lazima akupe sio ombi.

Akigoma kukupa barua usipotezee nenda idara ya mediation kama upo dsm nenda wizara ya kazi opposite na cbe chuo kama ni mkoani nenda mahakama ya kazi.

Ukikwama kabisa niPM nikusaidie upate stahiki zako.
 
Nyie ndie mnatakiwa jf....mnajua kujib kile mtu ametaka...wengine wanajib kejeli tu ili tuone na wao wamecommeent ama na wao tuone wapo Jf.
Hongera kaka mkubwa...msaidie mtanzania mwenzetu huyu....ni safari za maisha tu haya
 
Hakuna kitu kinaitwa kujifukuzisha kazi wasikudanganye awa wapuuzi.

Either unaacha kwa hiari au wanakupa barua ya kukuachisha. Bado unatakiwa upewe mshahara wa mwezi mmoja na huyo mwajiri na barua ni lazima akupe sio ombi.

Akigoma kukupa barua usipotezee nenda idara ya mediation kama upo dsm nenda wizara ya kazi opposite na cbe chuo kama ni mkoani nenda mahakama ya kazi.

Ukikwama kabisa niPM nikusaidie upate stahiki zako.
Uko sahihi mdau, kama mtu amekosea kwa mara ya kwanza huwa kuna barua tatu za kuonywa kabla ya kufikia hatua ya kumfukuza mtu labda kama mkataba umeisha.
Kwa walichomfanyia mleta mada ni uonevu na unyanyasaji wa hali ya juu.
Ila kwa kumsaidia mleta mada atutajie hiyo ofisi ili tuweze kumshauri.
Kwani hapa ni jukwaa huru
 
Sahihi kabisa, ana haki zake za msingi anatakiwa apewe.
 
Sahihi kabisa, ana haki zake za msingi anatakiwa apewe.
Ni kweli haki zake inabidi apewe.
Haki zake ni
1. mshahara wa mwezi mmoja
2. Barua ya huduma(letter of service)
3. Termination letter ili aweze kupata mafao yake kwenye mfuko wa jamii.
4. Na kama hakuna kipengele katika mkataba kinachoonesha muajiriwa atafukuzwa kwa kosa kama hilio inatakiwa alipwe faini.
5. Kama amefanya kazi zaidi ya mwaka mmoja katika hiyo kampuni anatakiwa alipwe kiinua mgongo n.k
 
anataka nimpe mshahara wa mwezi 1 je nihaki niwape au wao niwape
Andika barua wewe ya kuacha kazi,then mengine yatafuata.Na barua watakupa.Wape na mshahara wa mwezi mmoja sababu wewe ndo umeacha kazi.
Kama wanamwambia kazi imeisha, kwamba kajifukuzisha mwenyewe, kwa nini aandike barua ya kuacha kazi? Kwa nini wao wasimpe barua nakumwambia vile amevunja mkataba then automatically amejifukuzisha!!?
 
Nilikuwa nafanya kazi kampuni flani ivi,

Nilivyoskia nafas za JKT nikatuma maombi nikaenda kwenye usaili takribani week nzima na nimepata kufaulu ngazi ya wilaya.

J3 naenda kazini HR ananiambia hauna kazi umejifukuzisha.

Naomba msaada wa mawazo na kama kuna haki ya kisheria ya kuwadai au wao wananidai naomba kujuzwa
Kabla ya kudai hizo haki zako, unatakiwa ujuwe mkataba wako na muajiri unasemaje juu ya kipengele cha kuto kuhudhuria kazini bila ya kutoa taarifa, kinasemaje?
Lakini kiuhalisia mikataba mingi ya kazi kutokuhudhuria kazi kwa siku 3 au zaidi ya bila ya taarifa ni sababu ambayo utakuwa umejifukuzisha kazi wewe mwenyewe.
Kilicho muhimu katka hali yeyote iwe umefukuzwa kazi au umejifukuzisha kazi ni lazima upewe barua ya kuachishwa kazi kama wewe ulikuwa muajiriwa, hivyo basi lazima wakupe barua ili ufuatilie mafao yako katika hifadhi yako ya jamii, vinginevyo huyo muajiri atakuwa ni mbabaishaji.
 
sikutoa taarifa mkuu .maana nlipigiwa cm ya gafla niende mkoani kwenye usaili kwamba kuna shortage huko ya form six
naomba kusaidiwa kama nna haki yoyote kujua hapo
Hatua aliyochukua mwajiri ni sahihi.
 
Back
Top Bottom