Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Daah nakumbuka miez 7 iliyopita nilivyopita kwenye wakati wa mateso hadi nikakata tamaa ya kuishi. Kama ashafariki Mungu amrehemu..
Aisee kila nikiupitia huu Uzi nz kuusoma huu ugonjwa basi namkumbuka mshkaji wangu kipenzi ambaye wiki 4 zilizopita nilienda DSM kwa ajili ya mambo yangu na baada ya kufanya yangu nikasema ngoja nikamsalimie mshkaji ofisini kwake maana nilikuwa na muda sijawasiliana nae,Dah baada ya kufika naambiwa mshkaji alishazikwa toka 10 Feb mwaka huu kutokana na Cancer ya Ini aisee niliingiwa na ganzi maana kila nikivuta kumbukumbu namuona mshkaji alivyokuwa strong vya kutosha na kamwe hakuwahi kusumbuliwa na magonjwa ya ajabu ajabu but ukweli ukabaki kuwa mshkaji alishafariki and no more stories about him.Yaa Allah tunusuru na Adhabu ziumizazo Yaarabbi.
 
Huyo daktari amekosea..kwa technology tulionayo hapa bongo so far ni ngumu kujua zimebaki siku ngapi kulingana na ugonjwa husika..ula km yeye ameweza haya ni kheri..

I believe wote tutasherehekea mwaka mpya mkuu..i believe
 
Kukutana na huu uzi tena na kuona last seen yake ni May 14th.. nimetokwa na machozi.

Natamani kujua anaendeleaje jamani.. last posts zake zinanitoa chozi

I hope upo na hauna maumivu tena.. bado unasoma kama guest humu..
Usilie mkuu km yupo basi Mungu amtilie wepesi ktk maradhi haya na kama kaishatangulia basi tuseme tu kuwa hiyo ndio njia sahihi ambayo sote tutapita humo wala hakuna mjana katika hilo hata Jiwe naye atapita humo.
 
Daaah nataman kujua kama bado yupo, ivi haya magonjwa mbn zaman hayakwepo au ndo sababu ya uwepo wa serikali zaifu ya CCM
 
Neno lako limenibariki, ubarikiwe Mkuu.
 
Jamaa huenda hakuwa na rfk humu wa karibu..kiasi kwamba anaweza akayumegea updates.
Kujua muda wako wa kufa nao pia huleta shida kwa wengine.
 
marehemu baba yangu alifariki na ugonjwa huu Kansa ya kongosho(CARCINOMA HEAD OF PANCREASE) mwaka Jana mwezi wa kumi..kwakweli alipitia maumivu makali sana yan alikongoroka akawa kama MTU anayeugua UKIMWI alibaki mifupa tupu hata kukaa ilikua shida mana nyama matakon hamna kwahiyo alikua anaumia muda mwing alikua analala huu ugonjwa ni hatar tulitafuta tiba lakn ikashindikana akafia muhimbili...huu ugonjwa unamfanya mgonjwa apoteze hamu ya kula,inasabisha nyongo kutoingia tumboni kwahiyo choo kinakua cheupe kama chokaa,yan akila muda huo huo kinatoka,weight loss hii kila siku anapungua bila Ku notice,baba yangu alikua na 100kg siku ya mwisho tunampima alikua na 43kg yan kuna muda nlikua nalia nasema mungu ampumzishe mana alikua amechoka sana,kumbu kumbu zilishaanza potea...niliweza Ku google ugonjwa huu nikaona moja ya chanzo cha maradhi haya ni MTU kuwa na mawazo au msongo mkali wa mawazo na nikalinganisha na mzee wangu nikagundua ni kweli mana baba alikua ametengana na mama aliishi maisha ya upweke mpaka hapo ugonjwa huu ulipoonza na ilimchukua mwaka 1 na nusu mpaka anafariki dunia
 
Pole sana mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…