Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
Pole sana kaka, hakika siyo jambo jepesi kulipokea kwa mwanadamu yeyote yule.
Saratani ikiwa hatua hiyo mara nyingi matokeo huwa kama alivyoeleza daktari wako hata hivyo
Hakuna awezaye sema kwa hakika muda halisi wa kuishi kwa mgonjwa wa saratani, ila anaweza kutumia utashi , uzoefu na matokeo ya tafiti za kisayansi kueleza matokeo ya ugonjwa husika kulingana na hatua ya ugonjwa
Hivyo siyo dhahiri kuwa utakufa ndani ya miezi minne , kila mtu mwili wake una namna ya kustahimili matatizo kwa namna tofauti na mwingine, na inawezekana kabisa ndani ya hiyo miezi minne ukapata ufumbuzi wa tatizo lako kwa namna Mungu atakavyo ona vyema.
Nakushauri ufike ocean road hospitalambapo matibabu ya saratani yanatolewa bure
Pia nakushauri utumie muda mwingi kufanya kusudi la Mungu katika maisha yako
Unaweza andika kwa kirefu ushuhuda wa maisha yako na namna ulivyo jitahidi na namna unavyoendelea kupambana kuhakikisha unaendelea kuwa hai
Ni dhahiri yako mengi ya kujifunza kutoka kwako,kwakuwa saratani nyingi zikigundulika mapema zinatibika na kupona kabisa
Ukiandika kwa kirefu ugonjwa ulipo anza mpaka tatizo kugundulika yaweza saidia watu wasipitie mtihani ulio pitia kwa kuwa nina amini ungalifanikiwa kufika hospital sahihi kwa wakati sahihi, kwa sasa ungekuwa unatoa ushuhuda wa jinsi ulivyo ishinda saratani
Pia naomba ushauri kwa uwazi kuhusu nini kifanywe na mtu mmoja mmoja , jamii na wizara ya afya na serikali kwa ujumla kuhakikisha wagonjwa wa saratani wanapata matibabu sahihi.
Mwisho nakushukuru kwa kuwa na uthubutu wakueleza hisia zako na kuwa tayari kwa matokeo yoyote, nina kuombea Mungu akupe jawabu sahihi kwa tatizo lako na kukuwezesha kutumia chabngamoto hii kama fursa yakuleta mabadiliko chanya kwa maisha yako na katika jamii, pia pitia shuhuda mbali mbali za wagonjwa wa saratani kujua namna walivyopokea na kuishi kipindi kama unachopitia sasa.