Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Pole sana Mkuu. Tunakuombea na pia utuombee. Wewe umejua saa yako sisi hatujui. Haiyumkini tukatangulia kabla yako maana hatujui siku wala saa. Baba yangu alibahatika kuhisi kwamba siku zilikuwa zimekaribia. Katika maisha yake sikuwahi kuona amekanyaga kanisani. Lakini wiki moja kabla ya kuondoka duniani alifanyiwa sala ya toba akabahatika kulala katika imani. Hii ni miaka 22 iliyopita. Mungu akupe faraja na nguvu ya kupokea hali yoyote itakayofuata. Duniani tunapita maana hakuna mji udumuo.
 
Mkuu folk last seen may 14....say something bro.

Kimya sana mkuu unatutisha hata kama kuandika huwezi bonyeza tu nukta ipost hapa tujue kwamba bado upo!!!

Pole sana kwa maumivu,Mungu akugeuzie uso wake akupe faraja japo kwa muda huu ambao una walakini na maisha yako.

Ugua pole!
 
Hali hii halafu Mungu yupo anaona tu watu wake tunavyoteseka, why??
 
kuna mtu kanichefua sana hapo juu, sijui kafuturu bangi? unaleta udini mpk kwenye kifo? uwe mkristo, muislam, mpagan n.k utahukumiwa kwa matendo yako na si dini. We baada ya kumtia mtu moyo unamtisha, Nyie watu mnapenda kujiona nyie bora sana na asiyewafuata mnamtisha, ubaguzi umewajaa.
 
Duh! Pole sana mkuu! Nimesikitika ila ngoja nikwambie hivi;

Kwamba unapaswa kujua we are divine energy..sisi sio huu mwili sisi ni roho hivyo iandae roho yako kupata pumziko la milele na watu wengi walio experience near death situation wanaelezea how wonderful it is..maana kifo sio process bali its the state of changing from physical state kwenda spiritual blissful state yenye raha isiyomithilika we unadhani kwanini Mungu haishi mwilini na anaishi rohoni? Huku mwilini kuna uchafu na maumivu nenda tu into the real immortal part...the truest of all.

Kufa sio adhabu its the must process kwa kila kiumbe na hakuna maumivu kwani maumivu yako mwilini pekee sababu ya nerve, brain, neurons e.t.c but unaumiaje rohoni? Unaumiaje ubongo ukicease kufanya kazi? Haumii kabisa,Trust me!

Death is painless ndugu.

Tangulia mkuu, tunakuja!

Candle in the wind.

Love you folk
pole saana kwa haka kachangamoto unachopitia.

ushauri wangu ni mmoja na wa UHAKIKA kwa sababu nimeu prove mara mbili. (matukio ya kufa)

biblia inasema ''siku zetu duniani si nyingi ni miaka 70 tuu zaidi ni nyongeza'' sikumbuki mstari wa ngapi.

statement hio iliniokoa nikiwa nimezungushiwa pazia la kijani mwili wangu umekua wanjano na kuhisi kukauka mwili na GREAT kiza sijawahi kuliaona ever. madaktari wakiahangaika bila matumaini then nikashtuka ghafla nikilitaja jina la Yesu kutimiza ahadi ya neno hilo. madaktari walishangaa saana nikawa ushuhuda hata kwa wagonjwa wengine.

mara ya pili ilikua ajali pikpik na Fuso kubwa. niliiona ile ajali kabla ya kuipata na dakika kumi kabla mwili ulisisimka kwa hofu ya ajali.. i prayed na kukumbuka 70yrs kama ahadi ya Mungu katika maisha yangu (yetu). for sure tuligongana uso kwa uso na fuso nikaanguka kichwa nikapasuka kidogo na fuso likazima kichwani kwangu nikiwa nimezimia.

but i survived i am a live until to day mashuhuda ni watu wanashangaa mpaka leo hii.

Mungu ameweka kila kitu kwenye system ni jukumu lako na langu kufuata utaratibu wake ili upate haki yako. Utaratibu wake ni IMANI just only IMANI kwa neno lake you will survive.

si lazima uende maombezi maana uchungu hofu na mashaka uliyonao no one can bare hakuna hakuna isipo kua Yesu ambaye ndio Mungu aliyeuvaa ubinadamu kuokoa mwanadamu. Yesu alijua kua atauwa na akaiona siku yake ya kufa kwa ajili yetu, kama mwanadamu alipata wakiti mgumu kama wako lakini haku lose hope kwasabubu alijua anaye Mungu wa kweli and he will life again.

Maamuzi ya kufa after 4 months yapo juu yako kumkubali Kristo au Shetani kwakuruhusu hofu.

Nakuaona ukiishi zaidi ya miaka 40. be blessed!!
 
Nadhani ni mwanzo mzuri wa historia yako utakayoisimulia miaka 30 ijayo na watu hawataamini unachokisema.
Daktari ana mipaka yake kwenye suala la afya na uhai wa mtu.
Hata mimba inayoonekanahawana exactly time mtu atajifungua lini sembuse kifo!!
Hit a snage boy!! Bado una maisha sanaaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom