Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
uwiiiiiii"" huu Uzi sintoweza kuu handle " ...
 
Mbele yako nyuma yetu mkuu, kuwa karibu sana na maombi kwa kipindi hicho ili ujiandalie makazi ya peponi, kila kitu kitokeacho duniani Kina makusudi yake kwa Mungu,jitahidi sana kutenda yaliyo mema n'a kutubu dhambi zako, Uzuri wako unajua hatma yako kitu ambacho binadamu wengi hatujui kwa Hiyo wewe umepewa kitu cha Ziada, farewell mkuu, Msalimie sana baba Mungu huko utakapokutana nae juu mbinguni
aisee...najaribu kufikiria kama ningekuwa mimi ndiye na ambiwa maneno haya wakati...huuu"" kwakweli "" machozi yananitoka muda huu
 
KAKA YANGU MIMI ALIKIWA NA SARATANI YA KOO PALE MUHIMBILI DAKTARI AKAROPOKA HIVI....
"wewe ni wa kufa tu.... huna miezi miwili"

KWA HIYO USISEME MANENO HAYA KWA MADAKTARI WA TANZANIA LABDA KAMA UNATIBIWA ULAYA NA MAREKANI.
aiseeee"" Omg
 
Uzi huu umenifanya nimkumbuke marehemu mama yangu naye hana tofauti kabisa na maandiko yako, alijua atakufa baada ya miez kadhaa, alijitahidi kusali kwa bidii na naiman yuko mahala salama. Alifariki nikiwa kidato cha tano, hakika sitasahahu maana wiki moja kabla hajafariki aliniita nikaenda kumsalimia sikuamini km ni yeye alikuwa amekonda, sura haionekani vyema kabakiza mifupa tu hakika cancer stage 4 ni mbaya mno alipata maumivu makali chakula akila hakisagwi kabisa kinatoka haja kubwa kama kilivyoingia.

Naelewa maumivu yako ila neno langu kwako ni moja tu, sali omba makazi salama ya kiroho hakika Mungu yuko nawe, nitasali na ww kila siku kila saa naimani utapokelewa palipo salama.
Kila la kheri.
Aiseeee...""
 
aisee...najaribu kufikiria kama ningekuwa mimi ndiye na ambiwa maneno haya wakati...huuu"" kwakweli "" machozi yananitoka muda huu

Jamaa ana bahati sana,anajua hatma yake,sio kila mtu atapata bahati hiyo mkuu
 
Jamaa ana bahati sana,anajua hatma yake,sio kila mtu atapata bahati hiyo mkuu
mkuu" hapo bado hajaijua hatima ...kuna wanaumwa kama hivyo lakini kifo chao kina kuwa NI cha ajali ya moto ""...
 
Daah, very sad !! Machozi yakiwa karibu kwa uzi kama huu lazima yatiririke.
mimi nimeshindwa kuendelea kusoma comments "" nimeona nije tu katika page ya mwisho ....huko mwanzoni sinto paweza
 
Daaaah,, usikate tamaa mkuu unatakiwa kujaribu kila njia na ikishindikana hakikisha unaenda sehem salama..


Usijione kama huna cha kupoteza kwani uhai ulio nao bila juhali uko katika hali gani ni wa thamani kuliko kitu chochote duniani.

Ningepata kua karibu na wewe ninge hakikisha unakufa kwa tabasamu.
 
Duh! Pole sana mkuu! Nimesikitika ila ngoja nikwambie hivi;

Kwamba unapaswa kujua we are divine energy..sisi sio huu mwili sisi ni roho hivyo iandae roho yako kupata pumziko la milele na watu wengi walio experience near death situation wanaelezea how wonderful it is..maana kifo sio process bali its the state of changing from physical state kwenda spiritual blissful state yenye raha isiyomithilika we unadhani kwanini Mungu haishi mwilini na anaishi rohoni? Huku mwilini kuna uchafu na maumivu nenda tu into the real immortal part...the truest of all.

Kufa sio adhabu its the must process kwa kila kiumbe na hakuna maumivu kwani maumivu yako mwilini pekee sababu ya nerve, brain, neurons e.t.c but unaumiaje rohoni? Unaumiaje ubongo ukicease kufanya kazi? Haumii kabisa,Trust me!

Death is painless ndugu.

Tangulia mkuu, tunakuja!

Candle in wind.

Love you folk
Maneno yako yameniupunguzia uoga wa kifo nilionao kwa kiasi kikubwa sana mkuu
 
Saratani ya Kongosho:

Saratani ya kongosho hutokea katika tishu za kongosho, ogani iliopo karibu na sehemu ya chini ya tumbo. Kongosho hutoa vimeng'enya ambavyo husaidia usagaji wa chakula na pia hutoa homoni zinazosaidia kusimamia sukari iliyopo katika damu.

Saratani ya kongosho kawaida husambaa kwa kasi kuelekea katika ogani za karibu. Ni mara chache hugunduliwa katika hatua za awali. Lakini kwa watu wenye uvimbe wa kwenye kongosho au ambao wana historia katika familia juu ya saratani ya kongosho, baadhi ya taratibu za uchunguzi huweza kusaidia kugundua tatizo hilo mapema.

Mojawapo ya alama za saratani ya kongosho ni kisukari, hasa pale inapoandamana na upunguaji mkubwa wa uzito, manjano (Jaundice) AU Maumivu katika sehemu ya juu ya tumbo yanayosambaa mpaka mgongoni


ds00371_im00504_d7_digestionsystemthu_jpg.jpg



Matibabu yanaweza husisha upasuaji, mionzi ya kikemikali kwa njia ya dripu, mionzi au muunganiko wa vyote hivi vitatu


mcdc7_pancreaticcancer-8col.jpg



Dalili

Alama na dalili za saratani ya kongosho mara nyingi hazionekani au hazitokei mpaka pale ugonjwa unapokuwa umesogea katika hatua za juu. Zinaweza kuwa:

  • Maumivu katika upande wa juu wa tumbo yanayosambaa kwenye mgongo
  • Kukosa hamu ya kula au upunguaji usio wa mpangilio wa wa uzito
  • Depression
  • Mwanzo wa Ugonjwa wa Kisukari
  • Kuganda kwa damu
  • Uchovu
  • Ngozi kuwa ya njano na macho kuwa meupe

Wakati gani wa kumuona tabibu.

Muone tabibu kama unaona unapungua uzito sana bila ya sababu maalumu, au ikiwa una uchovu mwingi wenye kuendelea, maumivu ya tumbo, ngozi kuwa ya njano na dalili nyengine zinazokusumbua. Magonjwa mengi yana dalili hizi, hivyo daktari anaweza kuangalia magonjwa hayo pamoja na saratani ya kongosho.


Visababishi

Haipo wazi ni kitu gani hasa kinasababisha saratani ya kongosho , lakini matabibu wanatambua kuwa tabia kama ya uvutaji wa sigara, inaongeza hatari ya kuupata ugonjwa wa Saratani ya kongosho.

Sababu hatarishi

Sababu zinazoweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya kongosho inajumuisha:

  • Uvimbe sugu wa kongosho (pancreatitis)
  • Kisukari
  • Historia ya ugonjwa katika familia (genetic syndromes that can increase cancer risk, including a BRCA2 gene mutation, Lynch syndrome and familial atypical mole-malignant melanoma (FAMMM) syndrome)
  • Uvutaji sigara
  • Unene uliopitiliza (Obesity)
  • Umri (watu wengi huonekana na ugonjwa wakiwa na zaidi ya miaka 65)

ds00165_-ds00357_-ds00371_-ds00425_-ds00918_im04083_d7_ercpthu_jpg.jpg




Complications & Prevention

Diagnosis & Treatment

pancreatic-ultrasound-8col.jpg



Courtesy of Mayo Clinic

May Allaah almighty heal you from the adversity you are facing, like He cured Ayoub from what he was suffering with, and May Allaah spread his blessing and cures to all of us suffering from whatever form of illness. Get well soon folk

Further readings

Cholecystitis

Gallstones
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom