1:Mungu anaouwezo wa kuahirisha kifo chako ndugu yangu wewe sio wa kwanza. Tumekuja duniani kwa madhumuni maalum, tafuta muda zungumza na Mungu wako kama rafiki, ikiwa kuna vitu anahitaji ukamilishe hapa duniani HAUTA KUFA HAKIKA huo mwezi wa NANE hadi umalize majukumu hayo Mungu alilyokupatia(Yoshua 1:9). Lakini kumbuka hapa duniani hatujaja kukaa tunapita, tena haraka kama vivuli (1 Nyakati 29:15) hivyo maamuzi ya kuwa hai bila kujali hali zetu yako mikononi mwa Muumba wetu.
2:HOFU YA KIFO. Kama kuna kitu shetani amefanikiwa ni kutufanya tuogope kifo cha mpito(temporal DEATH) na Sio kifo cha Milele(ETERNAL DEATH). Mkuu miezi minne ikipita na Mungu akaruhusu ulale mavumbini, Jambo la maana kabisa ambalo hutajutia ni kulala ukiwa umejikabidhi mikononi mwake, Ukiamini Mauti ya Yesu kristo kama tiketi ya Uzima wamilele.
Yesu ameweka wazi tena kwa msimamo mkali...
"Kwa kuwa mapenzi yake baba yangu ni Haya, ya kwamba kila amtazamaye MWANa na kumwamini yeye, awe na uzima wa Milele, NAMI (Yesu) NITAMFUFUA SIKU YA MWISHO.
Yohana 6:40