Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Wote tutakufa hakuna hatakae salia, afadhali wewe unajua kitakacho kuua, wengine moto kama kipindi kile buguruni, wengine ajari mbaya uku unaona mwili wako ukiwa vipande vipande ndio unakufa.

Daima kumbuka maneno haya, Mungu ni mwema, huwezi jua pengine unaenda kwenye maisha mazuri kuliko haya ya ki Rodi lofa.
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na pancreatic cancer stage 4.

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Bye bye Mother earth.
Unatutangulia tu. Millions have gone before you so take heart. ALL MEN MUST DIE!
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na pancreatic cancer stage 4.

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Bye bye Mother earth.
Pole ndugu ila neno moja tu kazana kumuomba Mungu kwa maana yeye ndio daktari bingwa na pia Mungu wetu huishi katika sifa hivyo yu mkini umeshakiri ya kuwa madaktari wa dunia wameshindwa basi niwakati sasa wa Mungu kudhihirisha ukuu wake naamini hutakufa bali utaishi. Mungu akubariki sana na akulinde na mabaya.
 
Yupo mfalme mmoja wa Israel alitumiwa ujumbe kuwa "... weka mambo ya nyumba yako sawa kwamaana hakika utakufa hutapona kamwe" Lakini yeye badala ya kukaa na kusubiri kifo, aligeukia ukutani akamwita Mungu kwa nguvu zote. Mungu alisikia dua yake na kumwongezea siku nyingi za kuishi ili jina la Mungu liinuliwe kupitia uponyaji huo. Nenda kwa Mungu na matumaini makubwa Bwana atakunyanyua tena.
Mfalme Ezekia alitumiwa na nabii Isaya na alikuwa mgonjwa lakini alimkumbusha Mungu kwa kazi alioifanya na Mungu alisikia kilio chake na akamponya na kumuongezea miaka 15 ya kuishi
 
Duniani tunapita tu sio nyumbani kwetu, pole sana folks kwa yote unayopitia, Mungu akujalie ujasiri na wepesi kwa haya .
 
Duh! Pole sana mkuu! Nimesikitika ila ngoja nikwambie hivi;

Kwamba unapaswa kujua we are divine energy..sisi sio huu mwili sisi ni roho hivyo iandae roho yako kupata pumziko la milele na watu wengi walio experience near death situation wanaelezea how wonderful it was..maana kifo sio process bali its the state of changing from physical state kwenda spiritual blissful state yenye raha isiyomithilika we unadhani kwanini Mungu haishi mwilini na anaishi rohoni? Huku mwilini kuna uchafu na maumivu nenda tu into the real immortal part...the truest of all.

Kufa sio adhabu its the must process kwa kila kiumbe na hakuna maumivu kwani maumivu yako mwilini pekee sababu ya nerve, brain, neurons e.t.c but unaumiaje rohoni? Unaumiaje ubongo ukicease kufanya kazi?

Death is painless ndugu.

Tangulia mkuu, tunakuja!

Candle in the wind.

Love you folk
maneno yako yamenichoma sana
 
Pamoja Mkuu yeyote mbele sisi Nyuma

Nani ajuae
 
Nwanko kanu akiwa na umri wa miaka 11 au 9 aliambiwaa na dokta kwamba hawez kuishi mda mrefu kwan ana tatizo kubwa la moyo lakn ndiye tuliyeshududia akichezea tim kubwa dunian kama asernal etc na yupo hai stl. Unabii wa dokta sio last say sometimes huwez kutofautisha doctors na waganga wa kienyeji
 
mkuu folk hakuna atakayeishi milele, imagine wengine wamekufa wakiwa na miaka chini ya 28.je wazazi wanasemaje
 
Kwakweli mpaka nashindwa nikwambie nini ndugu yangu folk but don't loose hope Mungu ndiye anayejua siku, saa na majira. Mtumainie sana Yesu Kristo kipindi hiki tena ukipata msaada wa maombi katika kanisa la kiroho.
Kuna mdau amekushauri uende kanisa moja amelitaja na jina ambapo kuna uponyaji mkubwa kwa damu ya Yesu. Zingatia hilo kaka.
We all love you buddy
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom