Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na pancreatic cancer stage 4.

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Bye bye Mother earth.
Blv in doctor but take god with you kwa kuwa doctor is just a normal human being alichokifanya ni probability huwezi jua inaeza pona au la just have faith :
Ila ugua pole mkuuu
 
Pole sana ndugu yetu hii ni njia yetu sote tutapita hapa
 
hakika sote tutarejea KWAKE YEYE PEKEE, usihuzunike ndugu yangu matatizo ni yetu sote.
 
Daktari sitegemei kama anaweza kutoa majibu ya aina hiyo kwa mgonjwa! Kuna lugha fulani ya jinsi ya kuhudumia na kutoa majibu kwa mgonjwa si rahisi rahisi namna hiyo. Watu wa kuhudumia wagonjwa wa ishi kwa matumaini wanalijua hili iweje daktari aliyesomea miaka mitano?
Kwa muafrika ndio huambiwa kwa style hiyo unayotaka.
Ila mzungu huelezwa kwa style ya mleta mada.
Style zote ni sahihi kwa mazingira yake
 
Mshukuru Mungu sana kakupa nafasi ya kujua siku yako ya kuondoka.

Pata muda wa kutengeneza roho yako ili ukapumzike huko maana pia umeteseka hapa duniani.

Pata nafasi ya kutubu dhambi zako, kusamehe majirani na ndugu ambao uliona wamekuroga kumbe ni kansa ilikuwa ikikukula, pata muda pia wa kujisamehe na kuomba msamaha wengine wote wa karibu yako.

Wote tutakufa tu ila hatuijui siku....huenda mie nikakutangulia ingawa hapa nakuonea huruma. Natamani sana nami niijue siku ya kufa kwangu.

Mtume Paulo alisema " kuishi kwetu ni Kristo na kufa ni faida"

Mungu akuwezeshe ufe kifo chema
 
Follk usiache kwenda kwenye makanisa ya kiroho hata kama imani yako haikuruhusu bali mwamini Mungu tu yote yanawezekana kwake aminiye
 
Linafiki lilikimbia magroup ya TMT kwa aibu kubwa!!!
Hahaha haha, credibility yako yooote ya mambo ya cryptos imeyeyuka kama barafu!!!
Mnafiki Spiritual. Sijui niweke na namba yako hapa watu walitambue linafiki.
Kwenye group linajifanya kumsifia Ontario, kwenye magroup mengine linamponda. Na kuwashawishi watu walifuate kwa nyuma. Utapakatwa!!
Braza hivi akili yako iko sawa kweli wewe? Wewe si unasema ni engineer wa UDSM first class? Hebu uwe na staha na ubinadamu basi mkuu hapa kuna mtu ana magumu kabisa anahitaji faraja na msaada wa kiroho wewe unaleta masuala ya utapeli Forex hapa.

Kwani huuoni Uzi wa Forex kule? Si ukayasemee haya kule?

Kuna vitu mtu anafanya hadi unahoji juu ya uzima wa akili yake!? Asee?
 
Pole sana kaka Mungu mwingi wa huruma na rehema akutie nguvu......na zaidi damu ya yesu kristo inaenayo mema ikanene mema juu ya afya yako.....waebr 12:24. Maana kwa kupigwa kwake yesu sisi tumepona......cha muhimu ni kumlilia Mungu maana anasema njooni kwangu ninyi wote mlemewao na mizigo nami nitawapumzisha
 
Kwakuwa hakuna kitu chenye nguvu kubwa kuzidi imani basi naweza kukubaliana nawe utakufa kweli baada ya miezi minne( 4)
Inawezekana kweli unaumwa na umeambiwa hivyo lakini imani yako kwenye kufa baada ya miezi minne ndio itakupeleka kaburini zaidi....
Imani ina nguvu sana pengine Mungu angeweza kukubakisha hata zaidi ya miaka 20 lakini kwa imani uliyo onesha juu ya kifo ni ngumu kuruhusu Mungu kukunusuru maana umeani sana kwenye kifo baada ya miezi minne na nina hakika daktari hakukutajia ni tarehe ngapi kwa sababu hata yeye hana uhakika...
Nina hakika kama leo hiyo imani yako juu ya kifo after four months ukiihamishia kwenye uhai zaidi bila shaka utakaa zaidi ya miaka 10...
Mimi naamini hutokufa baada ya muda huo unachotakiwa kufanya ni kuamini wewe utaishi na uendelee kuswali/kusali ukimtumaini Allah/Mungu....
Hakika amini kwenye kuishi kwanza...futa mawazo ya kufa ili mwezi wa 9 uje uandike thread nyingine hapa...

Naamini hutokufa kwani ajue muda wako ni Allah pekee...
Kama Mungu kakuweka tangu 2013 ulipoleta hapa habari yako na sasa ni zaidi ya miaka saba ..kwanini ashindwe kukupa tena miaka hata 30?
Tatizo lako pengine una hangaika kila sehemu pengine una kwenda kwa waganga huku unachanganya na kwa Mungu.....
Chagua moja kuanzia leo tegemea Mungu tuu na ushauri wa madaktari....
 
Daah,pole sana mdau mwenzetu wa jf
Sipingani na wataalamu hatakidogo ila Mungu mwenyeenzi yote anaweza kuzidisha miezi minne hata mara ishirini.

Nakuombea uugue pole na usitawaliwe na hofukuu(phobia) kwani hofu pia itauchochea ugonjwa upatenguvu zaidi ya kukushambulia

Nami ninasematu ugua pole na usijawe na hofu sana WAPO WANAOKUPA POLE LEO NAO WANAWEZA WAKATANGULIA KABLA YAKO
 
Kwakuwa hakuna kitu chenye nguvu kubwa kuzidi imani basi naweza kukubaliana nawe utakufa kweli baada ya miezi minne( 4)
Inawezekana kweli unaumwa na umeambiwa hivyo lakini imani yako kwenye kufa baada ya miezi minne ndio itakupeleka kaburini zaidi....
Imani ina nguvu sana pengine Mungu angeweza kukubakisha hata zaidi ya miaka 20 lakini kwa imani uliyo onesha juu ya kifo ni ngumu kuruhusu Mungu kukunusuru maana umeani sana kwenye kifo baada ya miezi minne na nina hakika daktari hakukutajia ni tarehe ngapi kwa sababu hata yeye hana uhakika...
Kwakuwa umenena na kuamini kwa kinywa chako basi sisi hatuna budi kukubaliana nawe kweli utakufa baada ya miezi minne.
uko sahihi mkuu. Hata sasa hivi akitaka kubadili imani yake kwa dhati atapata muujiza. Binadamu tuna nguvu Kubwa ila wengi hatujui Tu.
 
Hii ndiyo ilimuua Steve Jobs. Pamoja na kuwekewa ini jipya lakini alikuwa amechelewa kwa kujaribu kujitibu mwenyewe kwa kutumia vyakula, herbs na imani. Ni mojawapo ya kansa mbaya kabisa na ina ukawaida wa kugundulika ikiwa imechelewa kutokana na ukweli kwamba haina dalili zinazoeleweka. Watu wa tiba mbadala, maombi na madaktari...
Amekata tamaa,amechoka na maumivu ya mfululizo.Binadamu tunapitia magumu mengi,magumu mengine ni magumu sana kiasi kwamba unafikia hatua ya kukufuru.

Ndugu yetu anahitajika kumshukuru Mungu kwa kila jambo, ajikabidhi mikononi mwake na ajiweke tayari kwa lolote. Maombi ya shukurani ni muhimu sana kwake maana yatampunguzia mzigo wa mawazo ya hofu.
Kwa imani tu,Mungu anaweza kutenda ambayo hayakutarajiwa
"Amuachie Mungu aendelee kumtendea atakavyo ona ina mfaa"

Pole sana ndugu yangu mgonjwa,wewe ni mshindi.Hata ukiondoka leo,tupo tulio jifunza kutoka kwako.Nikiugua siku tatu mfululizo najiongelesha kwa maneno yasiyo faa,lakini mwenzagu ni zaidi ya miaka kumi.
"Mungu akiona inampendeza kukutwaa,basi,ikawe hivyo[emoji120] [emoji120] [emoji120] "

MIMI NI NANI BWANA MUNGU WANGU, HATA NIWE HAPA?...ni kwa neema na rehema.SHUKURANI.
 
Asante ndugu, Jana nimelia sana kwani nimemkosea nini Mungu Mimi.
Usilie bado mtetezi wetu yu hai kila binadamu hupitia mapito sali usikate tamaa hafu nime Ku PM naomba unijibu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom